Mei Mosi 2020: Rais Magufuli atuma salamu za siku ya wafanyakazi, asisitiza waendelee kufanya kazi na kujiepusha na Corona

Wafanyakazi hawataki hizo blah blah zake za miaka yote. Wafanyakazi wanataka mkwanja mezani. Wameshamchoka.

Sasa Mzee meko atoke huko mafichoni aje naye kuchapa kazi. Aache kuwatumia wenzie kama chambo.
 
Na aje afanye kazi yeye, hii ndio hali ya Dar ambapo hata usiku saa 9 huwa pako bize
IMG-20200501-WA0008.jpeg
IMG-20200430-WA0055.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli amewapongeza na kuwatakia heri Wafanyakazi wote hapa nchini ambao leo Mei 01,2020 wanaadhimisha siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), mwaka huu sherehe za Mei Mosi hazitafanyika ili kuepusha mikusanyiko katika kujikinga na corona, JPM amewataka pia Waajiri kutotumia kigezo cha corona kuwanyanyasa Wafanyakazi.

Rais Magufuli amesema licha ya kwamba sherehe za Mei Mosi hazitafanyika mwaka huu, Serikali inatambua mchango unaotolewa na Wafanyakazi katika ujenzi wa Taifa na itendelea kusimamia maslahi yao na kuboresha mazingira ya kazi>>“endeleeni kuchapa kazi huku mkijikinga na corona”

“Wafanyakazi wenzangu nawapongeza sana kwa kuchapa kazi, nipo pamoja nanyi na natambua kazi nzuri mnayofanya, katika kipindi hiki ambacho Dunia inakabiliana na corona sisi tuendelee kuchapa kazi, kamwe ugonjwa huu usiwe sababu ya kurudi nyuma na kuacha kuwahudumia Watanzania, naamini Mungu atatuvusha”-JPM
#MillardAyoIkuluUPDATES
 
Nyongeza ya mshahara unajipa mwenyewe kwa kufanya nyongeza ya kazi zingine kama bustani, ufugaji nk
 
Kuna wakati inabidi usimamie msimamo wako hata kama utabaki peke yako!
 
Bado analeta tena yale ya mungu atatuvusha? Haha kama mungu yupo basi anajiambia kua nimewapa akili, mikono, miguu, wakae waitumie vizuri kupambana sio kuniomba niondoe kijirusi kimiujiza. Maombi hayafanyi kazi. Maombi hayafanyi kazi. Endeleeni kufata kilaza hili
 
cha1509,
Watu wachape kazi yeye kakimbilia Chato. Huyu Rais hatufai kabisa. Kipindi cha matatizo anatukimbia. Kwa nini asibaki Dodoma kuchapa kazi kama kweli anamwamini Mungu.

Watanzania tutumieni Logic zaidi. Tujilinde fanya kazi kwenye ulazima kabisa. Kama una vijisenti vya kukulisha miezi nne walau. Chukua likizo bila malipo.
 
Salaam hizi zinatumwa kutoka wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app

SALAMA HIZI ZAWEZA ATHIRIWA NA UTAMBULISHO KWA MAANA YA IDENTITY.
Utambulisho wa sehemu au identity hubadilika kutokana na mazingira, muda, hali, umri, rika, hadhi, mtazamo, kundo la watu, na kadha wa kadha.

Ipo hivi ukiwa nyumbani kwako utambulisho wako hubadirika kutokana na sababu nilizo ainisha hapo juu. Ukiwa nyumbani waweza tambulika kama "Jirani", "Baba", "Mume", "Mke", "Mama", "Mkwe", "Mtoto", "Kaka", "Dada" na kadha. inategemea upo katika kundi la namna gani.

Ila ukitoka na ukiwa watembea kwa miguu utambulishi wako utabadilika tena, hapa utatambulika kama "mwenda kwa miguu" au "mpita njia" au "mwananchi" au "raia" nk.

Ukipanda daladala au bodabaoda utambulisho wako pia utabadilika na kuwa "abiria". kwa bahati isio njema ukipata ajali na kunusurika basi utambulisho wako utabadirika pia na kuwa "manusura wa ajari" au "majeruhi" na ukienda lazwa hospitali basi utambulisho wako pia utabadirika na kuwa "mgonjwa". Ikitokea umeaga basi utambulisho wako utakuwa "marehemu".

Kwa hali hiyo hiyo ya tabia ya utambulisho, huenda basi huathiri eneo alilopo rais kwa wakati huo, na shughuli aifanyayo.

Kama ulivyo mwenge wa uhuru ile risala ya utii husamwa kwa kuelekezwa kwa Mh Rais so inamaana uonapo mwenge wa uhuru unaashiria uwepo wa rais.
 
Back
Top Bottom