Mei Mosi 2020 inakuja vyama vya wafanyakazi mnanini cha kuwambia wafanyakazi

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,449
9,372
Sote tunajua dunia sasa ipo kwenye mapambano ya covid-19, gonjwa ambalo limeathiri mfumo wa maisha ya binadamu kwa namna moja ana nyingine, lakini pamoja na gonjwa hili maisha inabidi yaendelee na ndio maana tunambiwa tuchukue tahadhari

Turudi kwenye hoja ya msingi bado siku chache dunia ihadhimishe siku ya mfanyakazi duniani, siku ambayo wafanyakazi wanapataga matumaini mapya ya usalama wa kazi zao na matumaini ya maslahi yao, kwa miaka mitano hapa kwetu Tanzania tumeshuhudia watumishi wa umma wakiahidiwa kuwa wachape kazi mambo mazuri yanakuja kwa bahati mbaya mwaka huu sherehe za mei mosi hazitokuwepo

Swali kwa kiongozi wa vyama wafanyakazi je mnanini cha kuwambia wafanyakazi 2020?
 
Tusubiri Mai mosi tutakuwa na REJESHO HURU

Sent from my Infinix X650B using Tapatalk
T
😀😀😀😀😀 kumbuka secta binafsi watu wanapoteza ajira tena kihuni huni vyama vipo kimya michango yao wanachukua je sasa wanawambia nini maana hii hali ya corona inatoa picha mpya ya jinsi mikataba yetu ya kazi iwe
 
Sote tunajua dunia sasa ipo kwenye mapambano ya covid-19, gonjwa ambalo limeathiri mfumo wa maisha ya binadamu kwa namna moja ana nyingine, lakini pamoja na gonjwa hili maisha inabidi yaendelee na ndio maana tunambiwa tuchukue tahadhari

Turudi kwenye hoja ya msingi bado siku chache dunia ihadhimishe siku ya mfanyakazi duniani, siku ambayo wafanyakazi wanapataga matumaini mapya ya usalama wa kazi zao na matumaini ya maslahi yao, kwa miaka mitano hapa kwetu Tanzania tumeshuhudia watumishi wa umma wakiahidiwa kuwa wachape kazi mambo mazuri yanakuja kwa bahati mbaya mwaka huu sherehe za mei mosi hazitokuwepo

Swali kwa kiongozi wa vyama wafanyakazi je mnanini cha kuwambia wafanyakazi 2020?
Ungeandika "kuadhimisha kimyakimya".

Ulitegemea wakutangazie nini?

Chapa kazi.
 
Naomba niseme ivi,mfanyakazi hana matumaini na wala hana mtetezi anachosubir yeye ni upendeleo tu.

Lakin kingine watu wa mtaani wanawatazama wafanyakazi wa serikali kwa jicho hasi,wanaona ni wezi,wengine wanawaona masikini(ombaomba).

Ndio maana hata serikali ikiwanyima mshahara wafanyakazi hata kwa miezi 2 tu,kuna watu wataona kawaida na pengine wengine watafurahi na kuipongeza serikali kwa walichofanya.

Nihitimishe kwa kusema mfanyakazi Tanzania hana mtetezi liwe baya liwe zuri ni lake tu ndio maana muda mwingine nakaa nasema uwizi serikali ina uhalalisha wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwani Rais ndo kaleta mei mosi,kama vile ambavyo hakuleta tetemeko la kagera na ajali ya st lucy na meli ukerewe ndivyo ambavyo hakuleta mei mosi,msisumbue ana kazi nyingi za maana zaidi
 
REJESHO HURU, Inamaana hufuatilii vyombo vya habari!!.

Anyway, ni hivi mkuu, serikali haina pesa kwa sasa; Nguvu yote imeelekezwa kwenye mapamabano dhidi ya corona.

Bila kusahau mwaka huu HAKUNA sherehe za MEI MOSI.

Hivyo ni vema mkaanza kujiandaa kisaikolojia mapema enyi wavuja jasho na walipa kodi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Corona tayari imeshampa mtu kisingizio cha kuuendeleza ule uovu wake dhidi ya watumishi wazalendo wa nchi hii. Inauma kweli.
 
Na mwaka huu ndo kapata cha kusingizia yaani. Tutaambiwa hakuna nyongeza kwakuwa kuna Corona,wakati hakuna wanachofanya kwenye corona na hakuna lockdown ya biashara wala Watu.
 
Q-liner
Hao watu wa mtaani kushangilia kuminywa kwa wafanyakazi ni ujuha tu, wafanyakazi ndio wateja kwenye magenge na viduka vya mtaani.... neema kwao hugusa maisha ya wengi kirahisi.

Naungana na wewe kusema hawana mtetezi.
 
Back
Top Bottom