Meghan Markel na Mwanamfalme Harry wajaaliwa kupata mtoto wa kiume.

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
4054784e-f8da-4df6-8b9a-b32828087c67_800.jpg


Mwanamfalme wa Uingereza na mjukuu wa Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza, Harry pamoja na mkewe Meghan wamejaaliwa ku[pata mtoto wa kiume mapema asubuhi ya leo.

Meghan au kwa jina la kifalme la Duchess wa Sussex aliingia kwenye hali ya kijifungua mapema siku wa jana na baadae asubuhi ya kuamkia leo kujifungua mtoto huyo wa kiume mwenye uzito wa kilo 3.5

Bibi yake Harry Malkia Elizabeth na mumewe Phillip, baba yake Harry Charles na mkewe Duchess wa Cornwall Camila, kaka yake Harry William na mkewe Duchess wa Cambridge Kate wote wamefurahishwa na ujio wa kitukuu hicho.

Harry na Meghan pia walitangaza ujio huo wa mtoto wao wa kiume kwenye akaunti yao ya Instagram ambayo ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho "Its a Boy!"

ef6e1a3b-13ae-488f-b1bd-8987a5b5899b_800.jpg


Mtoto huyo anakuwa wa saba kwenye orodha ya urithi wa kiti cha ufalme wa Uingereza na ataishi kijijini Windsor ambako kuna kajumba ka maana kaitwacho Cottage ne kidogo na shamba la babu na bibi yake Harry.

Kwa kweli msemo wa "tutabanana hapahapa" umetimilika.
 
Back
Top Bottom