Meeting with Mr. President

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Leo mida ya saa nane kamili (14:00 EAT) Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete atakuwa na mkutano na waandishi (wachache) wa habari Ikulu. Ajenda kuu ikiwa ni kuongelea uongozi wa nchi chini yake ndani ya miaka miwili.

Nitakuwepo? Sijui, ndo naelekea huko. More info to follow...
 
we nenda kanywe chai tu huko na kumpigia makofi jk. Halafu tuletee umbea wa kawaida wa hapa kuhusu fanicha za Ikulu, unene wa JK, vikombe vya Ikulu nk.
 
we nenda kanywe chai tu huko na kumpigia makofi jk. Halafu tuletee umbea wa kawaida wa hapa kuhusu fanicha za Ikulu, unene wa JK, vikombe vya Ikulu nk.

Can you clarify that? Unaona moderator wetu ni mtu ambaye hajawahi kuona samani za kisasa au hajawahi kunywa Chai kama wanayokunywa ikulu? Au unaona yeye ni mtu wa udaku tu! NI vema usim-judge kabla hajafanya alichosema ataka kufanya, just for the sake of fairness!
 
we nenda kanywe chai tu huko na kumpigia makofi jk. Halafu tuletee umbea wa kawaida wa hapa kuhusu fanicha za Ikulu, unene wa JK, vikombe vya Ikulu nk.

Naona humtendei haki bwana Invisible maana sio mtu wa hayo unayoyaandika hapo juu.

Chai anaweza hata kunywa nyumbani kwake na sio lazima aifuate chai Ikulu. Hata siku moja sijawahi kuona Invisible analeta Umbeya hapa JF.
 
we nenda kanywe chai tu huko na kumpigia makofi jk. Halafu tuletee umbea wa kawaida wa hapa kuhusu fanicha za Ikulu, unene wa JK, vikombe vya Ikulu nk.

Bila shaka jina lako linasadifu maandiko yako pia. Jaribu kumfahamu Invisible kabla hujakengeuka kwa maoni ya kumhukumu bila ya ithbati yoyote.
 
we nenda kanywe chai tu huko na kumpigia makofi jk. Halafu tuletee umbea wa kawaida wa hapa kuhusu fanicha za Ikulu, unene wa JK, vikombe vya Ikulu nk.

We shetani una matatizo gani? yani umeshindwa hata kusubiri ushaanza kutuonyesha jinsi usivyo na busara, sasa invisible kakukosea nini? kama hupendi alichoandika kwa kuona kinagusa maslahi yako we tulia tupo tunaopenda kujua, hayo ya chai na vikombe vya ikulu tunakuachia wewe coz inaonekana ndo mambo yanayotawala ubongo wako, yamtokayo mtu ndo yalomjaza. btw ikulu kwani kuna nini cha ajabu? au kuna vikombe vya dhahabu?
Big up Invisible, dont let them shut you up, tunangojea mkubwa atasemaje, how i wish amfute kazi karamagi, msolla na wengineo wengi.
 
...acheni hizo nyie mbona inaonekana kama joke tuu au ni zile tabia za kiswahili za kujipendekeza tuu maana mnachomshambulia huyo jamaa wala sikioni,jokes ni muhimu hata kama zinaudhi
 
nadhani mambo yote kuhusu kubadili baraza la mawaziri inaweza kuwa Leo,Navyomfahamu DR. Kikwete,atazungumzia hoja dhaifu na mafanikio ya safari zake alizofanya kwa miaka miwili.na hili suala alilozungumzia mama sitta jana kuhusu asilimia 90% kwenda shule za sekondari,hapa ndipo aytaweka mkazo sana sababu alishasifiwa na jumuia ya kimataifa kasaidia maendeleo ya Elimu ya Msingi..
 
joke nyingine bwana, watu wanaongea vitu serious wengine wanaleta utani, au unatamani nafasi hiyo ungepata wewe, tabia zako ni kama jina lao nini?? jaribu kuwa na busara bwana. invisible eeh tafadhali nenda na uje utueleze yaliyojili achana na huyo shetwani.
 
Shetani wewe!! shetani shetani shetani katika jina lipitayo yote nakuamuru legea!

Huu siyo wakati wa kuleta utani.. ni kumkoma nyani kweupeeeee
 
Leo mida ya saa nane kamili (14:00 EAT) Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete atakuwa na mkutano na waandishi (wachache) wa habari Ikulu. Ajenda kuu ikiwa ni kuongelea uongozi wa nchi chini yake ndani ya miaka miwili.

Nitakuwepo? Sijui, ndo naelekea huko. More info to follow...

mrekodi kisha lete video then sisi tutafanya the rest...
 
nadhani mambo yote kuhusu kubadili baraza la mawaziri inaweza kuwa Leo,Navyomfahamu DR. Kikwete,atazungumzia hoja dhaifu na mafanikio......

oh kumbe mheshimiwa ni Doktori..?! Sikuwahi kujua. Pls Invisible mpelekee pongezi kwa hiyo taito ya udakta pia!
 
Jamani, nilikua huko, kimefanyika kituko, Ikulu wamegawa makundi mya watu wanne wanne, sisi tumerudishiwa getini tumepangiwa muda mwingine (sitaji muda watanijua)... kwa hiyo hiyo ndio hali halisi, kwamba leo kutwa nzima Rais atakua na kazi ya kuzungumza na waandishi wa habari
 
SIpendi na nachukia tabia ya kupeana udaktari wa kwenye bahasha!!

Wengine ulitusotesha na bado wengi wapo wana usotea hadi vipala, wengine wanagawiwa tu kama peremende!! huku ni kuushushia hadhi udaktari!
 
Nahisi muungwana anatafuta Kina Rweyemamu wengine! kwanini wanne wanne?? mwaenda lishwa yamini ama?? haya tusubilie
 
Jamani, nilikua huko, kimefanyika kituko, Ikulu wamegawa makundi mya watu wanne wanne, sisi tumerudishiwa getini tumepangiwa muda mwingine (sitaji muda watanijua)... kwa hiyo hiyo ndio hali halisi, kwamba leo kutwa nzima Rais atakua na kazi ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Vituko na maajabu ya Mussa, huyu ndiye rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaona aibu hata kuongea na waandishi wote wa habari kwa mara moja kwani hoja ikipamba moto hataki wengine wakoleze. Hiyo ndio style mpya ya kugawa bahasha, courtesy ya EL na RA na bado mwaka huu tutaona mengi.

Maji yakimwagika hayazoleki.
 
...acheni hizo nyie mbona inaonekana kama joke tuu au ni zile tabia za kiswahili za kujipendekeza tuu maana mnachomshambulia huyo jamaa wala sikioni,jokes ni muhimu hata kama zinaudhi

sasa Koba, what do you need to discover that, the guy was not joking, Mbona hiyo iko wazi au tuunde tume tuchunguze? Usiwambie watu wanajipendekeza, who needs kujipendekeza kwa mtu asiyemjua? ili nini? au ndo zako mkuu, may be huwa unachangia mada kwa kujipendekeza,enjoy.
 
SIpendi na nachukia tabia ya kupeana udaktari wa kwenye bahasha!!

Wengine ulitusotesha na bado wengi wapo wana usotea hadi vipala, wengine wanagawiwa tu kama peremende!! huku ni kuushushia hadhi udaktari!

Mkuu Rwabugiri, heshima mbele,
unashangaa ndugu yetu smiling boy kuwa dr. (waitaliano huita dottore),ni udokta wa nini kwanza?literature,sanaa,utalii,uchumi,sayansi,it,au?hata mama rwakatare naye si walimpatia?kuna dr.mkapa,soon tutaweza kuwa na dr. salma kikwete (joke)...

cha muhimu tunataka kujua kuwa waliompa huo udoctor (bila shaka wa heshima) wangekuwa waungwana na kutuelezea ni kwa jambo gani (moja tu) ambalo limemfanya astahili kuwa dr. wa heshima.
 
He, sijui kama THISDAY na Mwanahalisi wapo, maana Mwanahalisi leo hata mitaani halipo....
 
Back
Top Bottom