Meeting with Mr. President

Ni vyema tukasubiri kitakachosemwa kwanza ndipo tuanze kutoa maoni yetu. Tusianze kukandia hapa bila hata kujua atakachosema. JK is your president, whether you like it or not.
 
Haya kulikoni au ndio time za kiafrika wakisema saa saba na nusu they mean saa kumi na nusu? Kweli tuna safari ndefu haahaa haaaaa....................................
 
Ndio maana naendelea kusisitiza kuwa, wabunge waanze kuomba kichwa cha JK ili kabla ya 2010 wawe wamemng'oa. Bila ya hivyo tutakesha naye hadi 2015, halafu wote tutabaki hoi bin taabani.
 
sasa kama alitaka kuwajulisha ratiba ya safari zake akiwa kama mwenyekiti wa AU si angesema agenda ya kikao,huyu jamaa msanii sana,kama ni hivyo basi angemueleza mwaandishi wake akutane na wanahabari,inna maana hao wanahari hawakumpa hata vijembe vya hapa na pale au ndio wote wana nidhamu ya uwoga?
 
Au anataka kuongelea mchele wa bure Tanzania? au pale UDS, hapana yawezekana ni uteuzi wa kanafasi ka miundombinu.
 
Kumbe aliwaita waandishi ili kuwapa ratiba ya safari zake kama chairman wa AU

Hakuongea JK... Salva ndiye kaongea! Hili halikuwafurahisha waliofika.

Mkuu nadhani tushakwambieni nini kimeongelewa na nani kaongea.

Kwa kirefu ni kuwa JK anaondoka nchini Kesho kwenda Ethiopia kwenye makabidhiano ya nafasi aliyo nayo na baadae ataelekea Uganda kwenye suala la amani ya Kanda ya Maziwa makuu maalum kwa ajili ya amani ya Burundi ambayo sasa inaelekea kutetereka.

Nadhani umenisoma!
 
Hakuongea JK... Salva ndiye kaongea! Hili halikuwafurahisha waliofika.

Kazi ipo, ndio maana nchi yetu ni maskini. Kama unaweza kupoteza muda wa waandishi wa habari wote ili tu kuwaambia ratiba za safari zak0 kama chairman wa AU, kweli tuna rais!

Wacha niende park mimi maana jua kali leo hapa. Nimesubiri nikidhani kuna jambo la maana, kumbe ubabaishaji tu!
 
Ni vizuri tukijua Raisi wetu yuko wapi na anafanya nini. Nakumbuka kuna mmoja wetu hapa alikutana na Raisi Mikumi akaileta hiyo story hapa, wengi wetu hapa tukaja juu eti kwanini ameenda kisirisiri, huenda alitusoma!
 
Mkuu nadhani tushakwambieni nini kimeongelewa na nani kaongea.

Kwa kirefu ni kuwa JK anaondoka nchini Kesho kwenda Ethiopia kwenye makabidhiano ya nafasi aliyo nayo na baadae ataelekea Uganda kwenye suala la amani ya Kanda ya Maziwa makuu maalum kwa ajili ya amani ya Burundi ambayo sasa inaelekea kutetereka.

Nadhani umenisoma!

Hivi kwa nini asipewe tena na Uwaziri wa mambo ya nje? naona huyu anajisahau bado anafanya kazi alizokuwa anazifanya wakati wa Mkapa.
 
Zimbabwe issue lazima ipo, Mafisadi wake nao wamo.

Heheheh

Tangu lini?yeye mwenyewe fisadi au hamjui?hivi watz mbona mnapenda kutufanya wengine mazuzu?hivi huyu jamaa hajawahi kuwa kwenye baraza la mawaziri?amezuka tu akawa rais?huyu jamaa anahusika kwa namna moja au nyingine kwenye mikataba yote inayoinyonya hii nchi!

Huyu jamaa yeye ndie aliekuwa minister wa foreing affairs zilipoidhinishwa pesa kununulia nyumba Italy bila kuuona mkataba wa ununuzi.

Huyu jamaa yeye ndie alikuwa minister wa nishati na madini wakati mkataba wa IPTL unasainiwa.

Huyu jamaa kwa maneno yake mwenyewe alisema kuwa hukutana na baraza lake kila alhamisi ya mwanzo wa mwezi. Swali hawakemei?hawaulizi mbona hawafanyi kazi ipasavyo? namjua huwa anafanya nini akikutana nao kila hiyo alhamisi?ahhh msijifanye hamjui? hehehe huwa nachekacheka na kukuna utosi! Juzi kwenye maziko ya Rafiki yake mpenzi walietoka nae mbali Bro Ditto watu walikuwa wanamshangaa maana alikuwa haonyeshi huzuni kabisa alikuwa nachekacheka tu utadhani yupo kwenye beuty contest! Huyu ndio Jakaya bwana mtu wa mizaha mizaha! Msitegemee chochote kutoka kwake!

Ole wenu mnao sema huyu chaguo la Mungu mtaangamia! shauri yenu!
 
Ndio maana naendelea kusisitiza kuwa, wabunge waanze kuomba kichwa cha JK ili kabla ya 2010 wawe wamemng'oa. Bila ya hivyo tutakesha naye hadi 2015, halafu wote tutabaki hoi bin taabani.

Mmmh....Kubwajinga, mbona unaomba lisilowezekana? Kwa misingi ipi? Na wabunge wapi? Kutoka chama kipi? Hilo liliwahi kutokea wapi katika Africa yetu hii!

It is all the way to 2015. Labda Kikwete aamue mwenyewe kuachia kwa sababu zake binafsi, kitu ambacho kitakuwa ni cha kushangaza ulimwengu mzima. Hata ikiwa hivyo, patakuwa na 'smooth transition' kwa uteuzi wa mrithi kwa utaratibu wa kichama tunaoufahamu.
 
Back
Top Bottom