Kwanza nikiwa kama mzazi niwape pole sana mamia kwa maelfu wa vijana wanaomaliza udaktari katika vyuo mbalimbali hapa nchini,kwa sababu ni wahanga wakubwa wa hii kitu inaitwa MCT.
Mchakato wa kumpata daktari unajulikana na ni mgumu sana kwani mtu kufikia kumaliza miaka mitano ya udaktari wa binadamu anakuwa amepitia mitihani mingi ya theory na practical.
Sasa hawa MCT wamekuja na kitu kinaitwa pre internship na post internship, kichekesho zaidi ni hiyo pre internship, ndugu zangu duniani kote na hata hapa Tanzania kwenye baadhi ya mabaraza kama famasia, maabara, na wauguzi, hamna kitu kinaitwa pre internship exam, unampima nini kijana ambae anatarajia kufanya mafunzo ya internship mwaka mmoja??? Lengo lenu katika hili ni nini?, Ina maana nchi hii madaktari wametosha kiasi hicho mnaamua kuzima ndoto za vijana??.
Maombi yangu kwa hawa wakubwa;
Waziri wa afya na naibu wake,
Na kwa unyenyekevu Mh. Rais wetu Mama Samia, naomba kuagizwa kufutwa mara moja kwa hiki kitu kinachoitwa pre internship na pia kukiangazia kwa jicho la tatu post internship kama inafaa kuendelea kuwepo kwenye kada hii ya udaktari.