Media zetu kwanini havijalipa attention kwa mauaji ya Pwani kama kwa Scorpion, Mwanafunzi wa Mbeya?

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Vyombo vya habari kwa nini havijalipa attention kwa mauaji ya Pwani kama kwa Scorpion, mwanafunzi wa Mbeya, Roma, Faru John na matukio mengine yaliyokuzwa kupita kiasi

Mauaji haya yalianza kitambo ,tangia mwaka jana ndio naweza nadhani ila hayakupewa coverage wala attention kubwa, yameanza kuangaliwa mwezi April baada ya askari 8 kuuwawa, wasingeuawa wale askari 8 kwa mkupuo basi hata hiyo kanda isingefanywa kanda maalum hata kama viongozi wangeendelea kuuwawa

serikali na polisi wana share yao ya lawama, ila siwalaumu peke yao maana serikali hufanya mambo saa nyingine kutokana na lilivyoripotiwa na waandishi

Mauaji Pwani yalikuwa yamemaliza viongozi takribani 20 lakini yalikuwa hayajapewa attention yoyote ya maana mpaka walipouawa polisi 8
Sasa waandishi wa habari imekuaje hilki tukio wakaliona ni la kawaida hadi wakafikia viongozi zaidi ya 20?

Maana kuna matukio yanatokea halafu yanapewa attention kubwa hadi unajiuliza yanastahili kupewa attention hii na mengine yanapuuziwa?

Mfano wa matukio ni kama lile la mwanafunzi Mbeya kupigwa na Mwalmu Frank Msigwa, tukio hili lilitikisa mitandaoni na tv na magazeti na hadi mwalimu huyo kuwa maarufu

Tukio linguine ni la kutobolewa macho kwa kijana mmoja na mtu anayitwa Scorpion, nyie pia ni mashahidi tukio hili lilivopewa attention na kijana Yule kuitwa kwenye interview mbalimbali na kupewa misaada

Roma Mkatoliki alitekwa na pia tuliona attention iliyokuwepo, lakini pengine huyu alikua msanii so lazima attention kubwa iwepo

Faru John pia aliripotiwa sana na vyombo vya habari japokuwa kuna ujangili mwingi unafanyika na hadi mfanyabiashara mmoja ndugu na mbunge wa CCM huko Iringa kutuhumiwa kuuwa watu walioripoti ujangili wake polisi lakini tukio lile halikupewa attention iliyostahili hata kidogo

Sasa hili la Pwani ningetegemea media kama za tv, radio na mitandao waende kuweka kambi na kuwahoji wananchi wa huko lakini huwa wanasukumwa na nini ku cover tukio fulani kupita kiasi na kuacha mengine yanayohitaji kupewa coverage kubwa zaidi….
 
Siku zote hizi vyombo vya habari vinapenda kutangaza mabaya ya serikali mazuri ya serikali kwao ni mwiko
 
Unataka wa-draw attention ya killers kwao? Je, wakiweka hiyo kambi watarudi wenyewe walikotoka au wakiwa kwenye state nyingine?
 
Unataka wa-draw attention ya killers kwao? Je, wakiweka hiyo kambi watarudi wenyewe walikotoka au wakiwa kwenye state nyingine?
Mbona matukio mengine ya mauaji wanaripoti tu, na sio lazima kuweka kambi hapo nimesema, wanaweza kumuita viongozi na kuwahoji kisha wananchi wakajua kinachoendelea kinaga ubaga, mfano yule jamaa aliye aliyechomwa macho aliitwa clouds akahojiwa, mitandao ikarusha mahojiano yake, magazeti yakaandika sana,
 
Siku zote hizi vyombo vya habari vinapenda kutangaza mabaya ya serikali mazuri ya serikali kwao ni mwiko
Hata hayo ni mabaya, kutangaza mabaya sioni kama ni tatizo ila kuna mambo mengine ni mabaya halafu hayatangazwi na wanachi wanapoteza maisha
 
Kuna habari huwa zinateka hisia za watu zaid kuliko habari zingne kama habari ambazo sio za kawaida kutokea ata kama zote ni mbaya bt zingne zitareportiwa zaid
 
Serikali haitaki kuyapa nafasi matukio kama hayo, Na lengo la magaidi siku zote uovu wao usikike.

Hivyo ni bora Polisi ikapambana nao kimya kimya hivyo mpaka dakika ya mwisho.

Nashauri hata polisi wakiua gaidi wasitangaze kabisa iwe kimya kimya....!
 
Labda wamechukizwa na polisi wa arusha kuwakamata wananchi walioenda kutoa rambrambi arusha
 
Haya ni matukio ambayo inasemekana wakikujua unawadiss wanakuua(hao wauaji). Sasa nani yupo tayari kufa, Mimi au wewe
 
Wameshachoka.kila siku misiba inatokea huko.
Alafu ni vifo vya aina moja.
Hizo habari haziuzi
 
Serikali haitaki kuyapa nafasi matukio kama hayo, Na lengo la magaidi siku zote uovu wao usikike.

Hivyo ni bora Polisi ikapambana nao kimya kimya hivyo mpaka dakika ya mwisho.

Nashauri hata polisi wakiua gaidi wasitangaze kabisa iwe kimya kimya....!
Kwani ni magaidi?
 
Serikali haitaki kuyapa nafasi matukio kama hayo, Na lengo la magaidi siku zote uovu wao usikike.

Hivyo ni bora Polisi ikapambana nao kimya kimya hivyo mpaka dakika ya mwisho.

Nashauri hata polisi wakiua gaidi wasitangaze kabisa iwe kimya kimya....!
Kwani ni magaidi?
 
Kuna habari huwa zinateka hisia za watu zaid kuliko habari zingne kama habari ambazo sio za kawaida kutokea ata kama zote ni mbaya bt zingne zitareportiwa zaid
Watu wakiuawa hisia hazitekwi mkuu? ila faru akiuawa ndio zinatekwa?
 
Back
Top Bottom