Media ya Tanzania haiwezi kuset agenda

Ekyoma

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,177
2,803
Habari za wekendi wana JF.

Vyombo vya habari hapa nchini asilimia 99.999 vinaendeshwa na upepo. Hawana uwezo wa kuset agenda ndo mana habari ni majipu tu. Hawajadili hali tete ya zanzibar, hawaoji kwa nini majipu ya wizara ya ujenzi hayatumbuliwi wala nyumba za serikali zilizouzwa.

Hawaoni hasira ata uhuru wa habari ukibakwa shame! Kuelekea siku 100 za Magufuli magogoni badala ya sifa za kijinga tungetegemea waonyeshe hatari ya kuleta udikteta nchini.

Kwa maoni yangu mm nafikili yapo mambo mengi nje ya bunge tunatakiwa kupambana nayo mfano kuzuia matangazo live ni lazima kila mtu mmojammoja, asasi na makundi mbalimbali iwe kwenye daladala, makongamano , mimbali nk sauti ipazwe tulikatae.

La polisi kuingia bungeni na kuwadharirisha wabunge kisheria maana yake bunge limenyang`anywa nguvu ya kuisimamia serikali na vyombo vyake kama isemavyo katiba ibara ya 63 ya mwaka 77

Aidha ni njia ya kuondoa kinga ya bunge chini ya ibara ya 100 ambayo kimsingi ilinukuliwa na katiba yetu toka ktk tamko la haki za binadam la uingereza 1689.

Suala hili linaweza kufikishwa mahakamani. Ila angalizo ni kwamba ufanisi wa mahakama ni mdogo mno. Hili liwe chachu ya kudai katiba ya wananchi.
 
Kwa mkt chenge sio, sahau kama tulivyosahau mabilion ya vroba.

Kuhusu media za bongo uko sawa kwa asilimia mingi Ila mwananchi/citizen wanajitahidi kuweka ajenda
 
Hofu ni kwamba nia nzuri ya Raisi Magufuli na Kassim Majaliwa inaweza kutafsiriwa cibaya na watendaji wa chini kwa kuwaumiza wengine kwa manufaa yao binafsi.
Ni muhimu pia kwa serikali kuliacha bunge lifanye kazi yake na iliheshimu, isiliingilie!
Nchi hii ni yetu sote, wapinzani na CCM wote ni watanzania, Kilicho na manufaa kwa taifa ni vyema kikasikilizwa na kufanyiwa kazi!, at the end of the day serikali itakumbukwa kwa mazuri iliyowafanyia watanzania na si mabavu itakayotumia kuzima sauti za wananchi au kuwaziba masikio wasisikie madudu yake!
 
hii ndio tanzania yangu jamani...looh wahat a shame and cowardy media
 
Hofu ni kwamba nia nzuri ya Raisi Magufuli na Kassim Majaliwa inaweza kutafsiriwa cibaya na watendaji wa chini kwa kuwaumiza wengine kwa manufaa yao binafsi.
Ni muhimu pia kwa serikali kuliacha bunge lifanye kazi yake na iliheshimu, isiliingilie!
Nchi hii ni yetu sote, wapinzani na CCM wote ni watanzania, Kilicho na manufaa kwa taifa ni vyema kikasikilizwa na kufanyiwa kazi!, at the end of the day serikali itakumbukwa kwa mazuri iliyowafanyia watanzania na si mabavu itakayotumia kuzima sauti za wananchi au kuwaziba masikio wasisikie madudu yake!
 
Watanzania hawajiamini hata kidogo. Awe amesoma au asiwe amesoma wote waoga. Hakuna anayefanya kazi kwa misingi ya taaluma yake. Angalia huko kwenye mawizara, vyombo vya habari ndio zero kabisa. Sisi wananchi ndio tunaolalamika kuhusu uhuru wa vyombo vya habari ila wao wenyewe hakuna kitu. Waoga na wanafiki. Waangalie jirani zetu wakenya, ndio maana wanatuzidi kila kukicha. Na kwa hii serikali ya JPM ndio atawafunga midomo kabisa.
 
Back
Top Bottom