Media Tanzania bado ni dhaifu sana. Kuna haja ya kujifunza kutoka wa wenzao wa Kimataifa

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Nimejaribu kufuatilia habari mbalimbali zinazotoka katika vyombo mbali mbali vya habari (Media) hapa nchini hasa katika kipindi hiki cha Msiba wa Mkapa.

Jambo la kusikitisha ambalo mimi binafsi nimegundua ni kwamba bado wapo mbali saana (nyuma) katika weredi wa jinsi gani ya kuandaa taarifa kutokana matukio (hakuna ubunifu kabisa) na mbaya zaidi uwezo mdogo wa kuelewa ni kipi kinatakiwa kitolewe kwa wananchi na wakati gani.

Kuharibu zaidi wote wamejikita katika "copy and paste" yaani kwa ufupi kwa wiki hii yoote ukifungua redio karibia zote na au hata magazeti (Haya ndio tena yameathirika zaidi) utakuta habari ni ile ile ikitangazwa kwa "style" ile ile moja na hakuna ubunifu hata kidogo tofauti na pale unaposikiliza vyombo vya habari vya Nje kama DW au Sauti ya Ujerumani.

Tisa, kumi leo ndio wamelikoroga zaidi nimejaribu kutathimini ni jinsi gani kama wataweza kubalance matukio mawili yanayolikumbuka nchii kwa sasa yaani msiba wa Mkapa na Ujio na mapokezi ya Tundu Lissu. Ni aibu saana aisee.
 
Hayo yote i jinsi uonavyo wewe, isitoshe Media za Tanzania zinahudumia Watanzania na haziwezi kuwa jinsi utakavyo wewe kama za nchi nyingine kwani sisi hatuishi hizo nchi, ...
 
Tisa, kumi leo ndio wamelikoroga zaidi nimejaribu kutathimini ni jinsi gani kama wataweza kubalance matukio mawili yanalikumbuka nchii kwa sasa yaani msiba wa Mkapa na Ujio na mapokezi ya Tundu Lissu. Ni aibu saana aisee.
Kwa ujumla wetu watanzania tunaugua ugonjwa unaitwa "Ukondoo wa Nyerere". Huyu baba kwa njia moja au nyingine alifanikiwa (sijui kama alidhamiria au la) kutufanya watanzania tusiwe watu wa kuhoji au kuonyesha hisia zetu (hasa pale tunapokuwa hatukufurahia kitu) na kuwa waoga wa dola.

Walioshika dola wanalijuahili na wanalitumia kisawa sawa nasi tunajifanya hatuoni kinacho endelea. Bahati mbaya ugonjwa huu huambukiza ingawa kuna dalili za wachache kati yetu kuamua vinginevyo. Waandishi wa habari na vyombo vyao kama watanzania wengine wengi nao huugua gonjwa hili. Hivyo basi hakuna cha ajabu kutokusikia habari za urejeo wa Lissu na walozileta zimewekwa huko ndani.

Wakina Lissu ni wachache sana na wenye ujasiri wa kuleta taarifa zao ni wachache zaidi. Kwangu mimi isingekuwa JF naamini ningekuwa gizani potelea mbali wale waliojivika jukumu la kutuambia Lissu si chochote. Bila Upinzani Imara.............
 
Kumbe ndo maana ukiwa mjanja mjanja wakudadisi na kuhoji mambo unahojiwa uraia wako.Aise huu ukon doo huu basi kwakweli umetufanya tumekua viazi kwakweli.
Kwa ujumla wetu watanzania tunaugua ugonjwa unaitwa "Ukondoo wa Nyerere". Huyu baba kwa njia moja au nyingine alifanikiwa (sijui kama alidhamiria au la) kutufanya watanzania tusiwe watu wa kuhoji au kuonyesha hisia zetu (hasa pale tunapokuwa hatukufurahia kitu) na kuwa waoga wa dola.
Walioshika dola wanalijuahili na wanalitumia kisawa sawa nasi tunajifanya hatuoni kinacho endelea. Bahati mbaya ugonjwa huu huambukiza ingawa kuna dalili za wachache kati yetu kuamua vinginevyo. Waandishi wa habari na vyombo vyao kama watanzania wengine wengi nao huugua gonjwa hili. Hivyo basi hakuna cha ajabu kutokusikia habari za urejeo wa Lissu na walozileta zimewekwa huko ndani.
Wakina Lissu ni wachache sana na wenye ujasiri wa kuleta taarifa zao ni wachache zaidi. Kwangu mimi isingekuwa JF naamini ningekuwa gizani potelea mbali wale waliojivika jukumu la kutuambia Lissu si chochote. Bila Upinzani Imara.............
 
Wengi wapo kwa ajili ya kuwafurahisha watu fulani..kwa ajili ya maslahi yao,.ila sio kuandika habari ambazo zitaelimisha na kuburudisha jamii inayowazunguka
 
Nlishaacha kununua magazeti ya kibongo tangia mwaka 2000.na channel yangu Ni cnn
 
Hayo yote i jinsi uonavyo wewe, isitoshe Media za Tanzania zinahudumia Watanzania na haziwezi kuwa jinsi utakavyo wewe kama za nchi nyingine kwani sisi hatuishi hizo nchi, ...
Interesting
 
Mimi habari za Tanzania huwa naangalia kwenye vituo vya kenya hasahasa Citizen TV na KTN. Huwa wanawaleta waandishi wao huku kufanya coverage bila kuegamia chama chochote. Nisiporidhika saana basi ntaangalia kupitia BBC Swahili. Imeisha hiyo.
 
TCRA ndio wanataka hivyo, ukichepuka tu kidogo unalimwa barua, faini au kufungiwa.

Watanzania ukiwaacha huru pengine hata coverage ya huo msiba msingeipata.

Media zinatafuta pesa kama machinga, usiwaone wajinga ni censorship ya TCRA inawalazimisha kufanana.

Unadhani kunafaida yoyote wanaipata kwa kurusha coverage ya msiba wa Mkapa?!

Hizo hizo media zinaweza kuandaa tamasha la Lulu ukadhani uko Hollywood, wanajua kazi yao vizuri ila hakuna faida yoyote kwenye hili.
 
Back
Top Bottom