Media Plan ya CCM Mtandao dhidi ya Zitto

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,860
Ujumbe huu chini nimetumiwa na ndugu Mchambuzi na ameonelea ni vema wadau mkaupitia kwa umakini.

Mchambuzi said:
Below ni interesting peace ambayo naona bado haijafika JF. It should be informative to many.

Siku njema
From: (User ID reserved)
Date: Oct 19, 2007 11:46 AM
Subject: Rostam Aziz anaongoza mtandao maslahi dhidi ya Zitto Kabwe
To: (ID Withheld)

Ndugu Wanazuoni,

Kuna mdau kanitumia email ambayo nimeipaste hapa chini. Binafsi nina uzoefu wa kutosha na vyombo vya habari nchini na ninafahamu kampeni za chini kwa chini na ushawishi alionao Rostam Aziz. Sio mtu mdogo katika mtandao wa vyombo vya habari.

Usishangae kusikia amekeza share nyingi sana katika baadhi ya vyombo vya habari (bahati mbaya ni vyombo ambavyo tulikuwa tunaviamini sana). Kuwa na share sio tatizo sana kwangu, ila kinachonitia wasiwasi ni ushawishi alionao; na jinsi anavyovitumia vyombo hivyo. Nadhani hutanipinga nikisema kuwa kwa mfano; Rai sio kama lile la utawala wa Jenerali Ulimwengu.

Limepoteza ladha, na wasomaji kibao wameanza kulistukia. Rai nalo linaandika habari kama gazeti la udaku. Mara Magufuli ana dem; hiyo si habari ya kuandikwa na chombo maarufu kama hicho; kumbe lengo lao ni kummpunguza nguvu na makali Mh. Magufuli ambaye (pamoja na mapungufu yake) ana nafuu fulani. Soma email hiyo hapa chini

(ID Withheld)

.......................................................................................................


Kuna habari za kuaminika kuwa Mhe Rostam Aziz maarufu kama RA amekuwa akihaha katika vyumba vya habari na kufanya vikao mbalimbali na baadhi ya wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kumtengenezea mabomu Zitto Kabwe ili jamii iache kuamini kile ambacho amekuwa akikisimamia katika siku za hivi karibuni.

Kumbukeni kuwa RA ndiye alikuwa mmoja wa wakuu wa idara ya propaganda wakati wa kampeni za urais ndani ya CCM mwaka 2005.

Kwa kutumia waandishi mbalimbali ambao wengi wao tayari wameshatajwa hadharani huyu jamaa ndiye alikuwa chanzo cha habari nyingi nyeti za serikali ambazo zilipelekea kuanguka kisiasa kwa mawaziri kadhaa wa serikali ya tatu ambao walikuwa wakonekana tishio kwa JK ambaye walitegemea kupata ride yake kuneemesha maslahi yao binafsi.

Huyu jamaa ambaye kwa sasa ndio anaonekana kama KING MAKER nchini mwetu na kiongozi wa pili katika kundi la MTANDAO MASLAHI akifuatiwa na mshirika wake kibiashara na tajiri mwenzake Nizar Karamagi amekuwa mwiba mkubwa kwa JK kutokana na uroho wake wa kutaka awe katika kila deal inayoendelea nchini. Rostam ni mtu mwenye upeo mkubwa sana wa kiakili na mjanja kibiashara na asiye na simile katika kulinda maslahi yake. Mbinu chafu ndio jina lake la pili na unafiki ndio middle name yake.

Katika hali inayojitokeza sasa inaelekea RA anapigania maslahi ya kundi ziima la MTANDAO MASLAHI kutokana na dalili kuwa limekuwa mzigo mzito kwa JK kufikia mahala kuonyesha dalili zote za kushukiwa na nyundo kali hata kabla ya uchaguzi wa ndani wa chama kufanyika.

Pamoja na kuwa maslahi katika makampuni mbalimbali miliki ya vyombo vya habari kama Habari Corporation ambayo hutoa magazeti ya RAI, MTANZANIA na vilevile share ndogo katika umiliki wa gazeti la MWANANCHI na THE CITIZEN ambako amekuwa akizidiwa nguvu na Wakenya, RA anaushawishi mkubwa kwa waandishi wengi wa magazeti yetu kufikia wakati fulani kuwa akiwalipa mishahara tena mikubwa kuliko wapatayo kutoka kwa waajiri zao.

Moja ya kazi inayoendelea ni uandishi wa makala mbalimbali za kuwahadaa watanzania kutomuamini Zitto kabwe akiwatumi watu kaka Dr Gideon Shoo na Muhingo Rweyemamu ambao kwa miaka mingi sasa wamekuwa watumishi wake waaminifu katika kazi ya UHANDISI WA HABARI. Hawa ni vinara tu lakini wapo wengi wengine. ngome yake nyingine ni Gazeti la MAJIRA.

Kwa hali inayoendelea ni wazi mtasikia mengi kuhusu Zitto Kabwe lakini kuweni makini na kujaribu kujua vyanzo vya habari hizo. Cha ajabu ni kuwa huyu jamii wakati wote hupenda kujifanya ni rafiki wa Zitto na kujigamba kuwa anamkubali na misimamo yake lakini ukweli ni kuwa akipata nafasi tu hataacha kummaliza ndugu yetu na kijana mwenzetu Zitto Kabwe. Ukweli ni kuwa RA ameshiriki hata kupanga njamaa za kuwaundermine baadhi ya wanamtandao wenzake ambao wanonekana kuelemea kundi la MTANDAO MATUMAINI linaloongozwa na Waziri MMoja mwandamizi Nchini ambalo liliweka imani ya matumaini ya watanzania kwa JK ambaye anaonekana kuelemewa nguvu na mafisadi waliojikita katika mpango wa kula hadi kusaza utajiri wa watanzania.

Zaidi sintashangaa kuwa hili likawa kosa la mwisho la RA ambalo sio tu litamrudi yeye binafsi lakini pia lina hatari ya kuzua hasira za watanzania wengine dhidi ya watanzania wenzao wenye asili ya asia (mnapenda waita wahindi) ambao RA anaonekana kama kinara wa maslahi yao katika ngazi ya kisiasa ingawa yyeye ni Muiran (mbulushi) zaidi ya uhindi
 
Kwanza huyo Mchambuzi mbona haleti matokeo ya poll yake aliyoianzisha kabla ya kung'atuka. bado hatujasahau , kama yupo anapitia pitia mdau ninamkumbusha vip POLL yetu kuhusiana na matatizo ya WATZ imefikia hatua gani mbona Updates hakuna?
 
Mi naona kuwa dawa yake RA ni kuweka hdharani kazi alizokuwa anafanya. Anajiona spin doctor but what he's doing is 2nd grade stuff! Hata wakati wa uchaguzi ilikuwa wazi that it was d-class spinning. Lakini tatizo waTz tunaogopana, dawa yake ni kumwanika. Ngoja apewe dawa hiyo na Mwanahalisi. BTW nilisikia alhamisi Kulikoni yote ilinunuliwa na 'somebody' kwani ilichapisha in detail masuala ya Richmond! Ni rumours au la? Mwuza gazeti niliyemwuliza aliniambia hivyo!
 
Same old spinning....

si wameona kasi yao imepungua so they had to make something up ! ilivyotolewa ile email kuhusu slaa watu wakasema imeandikwa na ccm tena RA, jk, na el. watu walivyokuwa wajinga bana. sasa kila mtu anajua hapa ni kama sehemu ya waropokaji na sio kama zamani. Reputation Lowered to below standards !
 
si wameona kasi yao imepungua so they had to make something up ! ilivyotolewa ile email kuhusu slaa watu wakasema imeandikwa na ccm tena RA, jk, na el. watu walivyokuwa wajinga bana. sasa kila mtu anajua hapa ni kama sehemu ya waropokaji na sio kama zamani. Reputation Lowered to below standards

Usitumie implication ya kile unachokiamini kujenga conclusion ya kile ambacho "hakiexist"

Mimi ninadhani JF bado iko makini, na kadri siku zinavyokwenda ndo naona uwanja wa mijadala unavyopanuka, ipo mijadala mizito ambayo kina karaghabaho hawatii mguu, ipo mijadala ya kati, ambayo watu pia hawajivungi kushiriki, wengine hata kwa kucheka (kwi, kwi, kwi) tu, lakini nao wanaonyesha kuwa wanafuatilia mijadala. na ipo mijadala ya kawaida kabisa ambayo walalahoi wengi Wa Tz hushiriki vijiweni, au akina dada wanaposukana nywele salon ambayo watu wengine huita ni UDAKU. Watu nayo watachangia tu.

Sasa kujaribu kuishusha Forum kwa sababu mijadala inaelekea kupiga nyundo zaidi kile usichopenda kusikia ,si tu kwamba "unagenerelize", bali unakuwa unashindwa kutofautisha lipi ni lipi katika wakati upi na upi.

Lawama pekee hazitoshi ,bali inabidi tulete mijadala mizuri ya kuelimishana, hata kuburudishana.

Siyo lazima every time iwe ngunguri nguri tu na siasa za wanasiasa , hata vituko vyao pia kama vipo vinajulikana lazima tuviangalie, hawa ni role models bwana lazima jamii iwakodolee macho.

Pia nimuombe admistrator afanye juhudi za kipekee kuwashawishi wadau wachangie na forums nyingine, hii ya siasa imenona sana, nyingine nazo zinahitaji pia kuchangiwa changiwa ili nazo zizidi kutoa wigo mpana kwa wana JF.
 
Usitumie implication ya kile unachokiamini kujenga conclusion ya kile ambacho "hakiexist"

Mimi ninadhani JF bado iko makini, na kadri siku zinavyokwenda ndo naona uwanja wa mijadala unavyopanuka, ipo mijadala mizito ambayo kina karaghabaho hawatii mguu, ipo mijadala ya kati, ambayo watu pia hawajivungi kushiriki, wengine hata kwa kucheka (kwi, kwi, kwi) tu, lakini nao wanaonyesha kuwa wanafuatilia mijadala. na ipo mijadala ya kawaida kabisa ambayo walalahoi wengi Wa Tz hushiriki vijiweni, au akina dada wanaposukana nywele salon. Watu nayo watachangia tu.

Sasa kujaribu kuishusha Forum kwa sababu mijadala inaelekea kupiga nyundo zaidi kile usichopenda kusikia ,si tu kwamba "unagenerelize", bali unakuwa unashindwa kutofautisha lipi ni lipi katika wakati upi na upi.


sikusoma jibu lote uliloandika bali nimesoma hiyo mistari niliyounderline, na wewe usitumie OPINION yako kuweka conclusion ya vitu ambavyo watu wanaona tofauti ! kama wee unaona hivyo, ok, and i said what i thought ! theres more to come !
 
halafu naona unatetea pumba tu mzee, ulikuwa wapi ile thread ya email ya ccm ilivyotundikwa hapa ? mbona sikukuona ukiitetea ? ndio kwanza watu wakaanza kumkandia yule ambaye aliyeiweka hapa ( sikumbuki ni nani )wakaanza kusema yeye ni ccm just because ameweka ile email hapa, sasa unaona wapi forum inakoelekea huko ? kila kitu ccm, mtakuwa waongo na wadaku kama kila kitu kinatokea mnasema ccm !
 
Pamoja na yote yaliyosemwa kwa sababu tofauti ama pengine kwa kuwa amejitokeza Mchambuzi, jambo la msingi hapa ni kwamba tujiulize kama ni kweli RA ana mkakati dhidi ya Zitto? Je, ni kweli hizo tabia za RA kwamba amewaweka mfukoni waandishi ni za kweli?

Binafsi naweza kusema kwa asilimia sabini na tano (75%) kuhusu RA ni ya kweli. Naomba niishie hapo
 
Tumesikia mengi kuhusu Rostam Azizi na Uharamia wake katika vyombo vya habari.

Tumesikia jinsi aidhoofishavyo, kuidharirisha na kuiburuza taaruma nzima ya Habari kwa manufaa yake na kundi la Mafisadi wengi ndani ya SISIEMU, kma si Wakoloni Mambo leo na maharamia wote wa ughaibuni.

Tumesikia jinsi MH huyu atawanyavyo sehemu ya ufisadi wake kama majani ya miti wakati wa kipupwe katika mifuko ya Wahariri wa magazeti nchini Tanzania ili kuwalegeza misimamo,mawazo,mwelekeo na kuwaziba midomo na kuwapa kigugumizi cha mikono.

Tumesikai watu kadhaa ndani na nje ya JF wakitetea juu ya utajiri wa RA kwamba ni wa asili na hauna uhusiano wowote na njama za kuhujumu na kudhurumu Utu wa Watanzania kupitia chama cha Kifisadi SISIEMU na vikaragosi wao wote wa ndani na nje ya Tanzania.

Rostamu Azizi ni nani?

Sasa ni wakati wa Kumpa Mshindo Nyuma na kula naye sahani moja na jamvi moja kwa kupata undani na ukweli juu ya Uvunda na Uoza wote ausambazao katika vyombo vya habari.

MH RA anatwanya sehemu ya ufisadi wake ili kutawanya Roho ya Umasikini kwa watanzania wengi kama si wote kwa lengo la kuimarisha utawala wa kifisadi wa wachache na kujenga imani kwa Watanzania wote kwamba Umasikini wetu ni Hurka ya Mwenye enzi Mungu na ni Amana yetu.

Uharamia huu wa RA unafanywa kwa gharama ya jasho na maumivu yetu sisi Watanzania wenyewe. Kwa lugha nyepesi anatukaanga kwa mafuta yetu wenyewe.

Wana JF na Watanzania wote kwa ujumla ili kumjua hasidi wetu huyu na namna ya kumzingira na kumnyofoa manyoya kinenani mwake na kukata kende zote mbili ni lazima tufahamu wasifu wa RA.

Nilazima tujue historia yake yote Tangu babu yake,baba yake na yeye mwenyewe.

Ni lazima tuwajue ndugu zake kama kaka Dada Wajomba Shemeji na marafiki wa nasaba yake ili kujua mduara na ufanikishaji mzima wa uovu na ujenzi wa uhasama kwa kisingizio cha siasa.

Ni vema tuzijue Shughuli zake za kiuchumi katika kila kona nchini Tanzania na nje ya nchi zinazo daiwa kumwingizia fedha nyingi na kumpa kiburi cha kudharau Watanzania na Tanzania.

Ni lazima tujue tangu aingie katika siasa miaka ya 90 kasi ya Ukuaji wa himaya yake, utajiri wake na zidaiwazo kwamba ni nguvu za ushawishi wa vyombo vya habari imeongezeka kwa asili mia ngapi.

Tuitajapo nguvu ya ushawishi wa vyombo vya habari ni vizuri kujua Siri ya nguvu hiyo.

Je ni ushawishi ni Blackmailing au ni matumizi mabaya ya nguvu za dola yaambatanayo na kutia hofu wahariri kama watu binafsi na famila zao? Kutia hofu ya kufungwa na kufungiwa biashara vyombo vya habari na wanahabari??

Itakuwa vema pia kufahamu Historia yake nzima ya elimu mahali aliposoma na kiwango cha juu cha Elimu yake.

Marafiki zake ndani na nje ya serikali wanajishughulisha na nini.

Alijiingizaje katika siasa pia kabla ya kuingia katika siasa alikuwa ni mtu wa namna gani.

Je kuna mkono wa mtu kutoka ughaibuni ndani ya himaya na shughuli zote za RA.

Who is Rostam Azizi!?

Who does he think he is?
 
Msitake kudanganywa na manazi hapa kuhusu RA na utajiri wake. hakuna mwarabu wala mjomba wake alokuwa na urithi wa utajiri mkubwa ndani ya Utawala wa Mchonga tena tokea Igunga! jamani mweee kwa investment gani na wateja gani hasa alokuwa nao huko. Familia yake walikuwa nazo za Usalama tu wa maisha ya Mtanganyika hata akina Bomani walokuwa matajiri toka Mkoloni hawana Utajiri unaoweza kulingana na huyu jamaa. Kifupi matajiri wameanza kuonekana miaka ya Mkapa, nyuma ya hapo ni kufungana kamba tupu.

Kitu muhimu ktk mada hii sio utajiri wala nafasi yake serikalini inayotusumbua wananchi isipokuwa ni utaratibu unaotumika leo hii na chama tawala kuwatumia hawa matajiri kununua madaraka, kura za wananchi. Vyombo vya habari vinatakiwa kuwa free of political tie!..

Tazama katika kila mkoa, wilaya utakuta ni matajiri wanaoshika nafasi za juu ktk chama CCM. Hawa wamekuwa Untouchables na kama tukifuatilia maneno ya Gen. Ulimwengu utakuja amini kwamba huko vijijini ndiko kunakotokea mengi mabaya zaidi. na huko ndiko CCM imejijenga kwa kutumia mifuko ya matajiri hawa.

Maradhi yetu makubwa ni Umaskini na hakuna dawa ya masikini kilema wa kufikiri kama FEDHA!.. Rostam anayo dawa hiyo....
 
Kada

samahani mzee..............hiyo email ya ccm iko wapi.............sikubahatika kuiona
 
Wanapotumbua pesa ya walipa kodi hawafikirii ya kuwa wanawaumiza WTZ walalahoi ambao hawawezi kukwepa kodi. Hawa mafisadi siku yao inakuja tena imekaribia kuliko wanavyofikiri.
 
si wameona kasi yao imepungua so they had to make something up ! ilivyotolewa ile email kuhusu slaa watu wakasema imeandikwa na ccm tena RA, jk, na el. watu walivyokuwa wajinga bana. sasa kila mtu anajua hapa ni kama sehemu ya waropokaji na sio kama zamani. Reputation Lowered to below standards !

Dua thanks....................hiyo niliyopaka rangi nyekundu ndio email ninayoitafuta
 
hata sijui ipo wapi lakini hapa waliitoa baada ya siku 1 tu ! itafute usipoiona nijulishe !
 
Kabwe Zitto ni msaliti wa Upinzani?

na Dk. Gideon Shoo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilifanya kikao cha Kamati Kuu (CC) mwishoni mwa wiki iliyopita, na ajenda kuu ilikuwa ni kumruhusu au kutomruhusu Zitto Kabwe kushiriki katika Kamati ya Madini iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete.

Uamuzi wa kulifanyia kikao suala hilo la uteuzi wa Zitto kuingia kwenye Kamati ulitokana na hali ya mvutano iliyojitokeza ndani ya chama hicho hususan miongoni mwa viongozi.


Viongozi wa CHADEMA waligawanyika katika suala la Zitto. Mgawanyiko huo ulisababisha kurushiana vijembe na tuhuma zisizokuwa za moja kwa moja, lakini zililenga katika kufanya uteuzi wa Zitto uonekane kuwa na hitilafu ulizua mjadala ambao hatima yake ndiyo kikao hicho cha Kamati Kuu.


Ingawa si rahisi kusema kwamba Zitto aliteuliwa kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini na / au Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, kwa hakika aliyekuwa amelengwa zaidi katika mvutano huo ni Zitto mwenyewe ambaye upande uliopinga kuingizwa kwake katika kamati hiyo ulijitahidi kujenga taswira isiyopendeza ya mwanasiasa huyo.


Zitto, ametuhumiwa kinamna kwamba amerubuniwa, kuhongwa na hata kulainishwa ili ‘awasaliti' wanachama wenzake wa CHADEMA.


Uteuzi wa Zitto ulifanywa na Rais Kikwete na ingawa hakutaja sababu ya kumwingiza katika Kamati hiyo lakini ni wazi kwamba kutokana na mchango wake katika mjadala wa mikataba ya uchimbaji wa madini na hasa suala la Mkataba wa Mradi wa Buzwagi ilikuwa si rahisi kutokumwingiza humo.


Baadhi ya viongozi wa CHADEMA, hata wale ambao walisikika hadharani wakikubaliana na uteuzi wa Zitto, walijitokeza hadharani na kupinga uteuzi huo tena kwa kelele nyingi.


Viongozi hao hata hivyo walikuwa wakimsukuma Zitto ajing'atue kutoka katika Kamati hiyo ili kumpisha mtu ambaye baadhi yao walimwona kwamba ndiye anayefaa zaidi. Hata hivyo, vigezo vilivyotumiwa kuonesha kwamba huyo ‘aliyetakiwa' kuingia katika Kamati hiyo bado ni kitendawili.


Aidha, kumekuwapo malalamiko kwamba eti hadidu za rejea zilizopewa kamati hiyo na Rais Kikwete zilikuwa hazitoshelezi.


Malalamiko mengine ni kwamba baadhi ya walioteuliwa walikuwa ‘si wasafi' kwa vigezo visivyo vya kuthibitika kisheria bali kwa hisia na dhania.


‘Uchafu' wa baadhi ya wateule wa Rais Kikwete kuingia katika Kamati hiyo ni kuhusishwa kwao katika mikataba iliyokwisha kutiwa saini miaka ya nyuma. Mikataba ambayo inadaiwa kwamba ni mibovu na inayoliumiza Taifa letu.


Turudi katika hili la Zitto na nafasi yake katika Kamati ya Madini ya Rais Kikwete. Baada ya mjadala mkali na wakati mwingine uliojaa jazba kilichojitokeza wazi wazi ni kwamba baadhi ya viongozi wa CHADEMA wameonesha wazi kutoridhishwa kwao na uteuzi wa kijana huyo na wamekosa imani naye kama mwakilishi wa umma.


Hata baada ya kuwa kikao cha Kamati Kuu kilimazilika na kuonekana kwamba kuna aina fulani ya muafaka iliyokuwa imefikiwa bado ngurumo za chini ya ardhi ziliashiria kwamba hali si shwari.


Katika jitihada za kutuliza mzuka ambao ulikuwa umewapanda viongozi wa chama hicho kumekuwapo na jitihada za haraka za kumtafuta mchawi.


Pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutangaza kwamba kimekubali na kuridhia Zitto kuingia katika Kamati hiyo ya madini lakini kwa namna tangazo la kuridhia huko lilivyotolewa ni wazi kwamba hilo limefanyika shingo upande.


Mbowe anazungumzia chama hicho kumruhusu Zitto kushiriki katika Kamati hiyo kama vile kijana huyo ameteuliwa kama mwakilishi wa chama hicho kwenye kamati hiyo.


Siamini kwamba uteuzi wa kuingia katika kamati hiyo umefanyika kwa misingi ya vyama kwa sababu kama ndivyo basi tungelikuwa na sura takriban kumi na ushei.


Awali nilisema kwamba sijui vigezo alivyovitumia Rais Kikwete kufanya uteuzi lakini naamini kwamba kwa kumwingiza Zitto moja ya sababu za msingi sana ni mchango wake katika mjadala huu muhimu wa nafasi ya Taifa letu katika sekta ya madini.


Lakini pamoja na Mbowe kuafiki kijana huyo kushiriki katika Kamati hiyo, (na siamini kwamba anao ubavu wa kumzuia) jambo jingine lililojitokeza ni mlolongo wa masharti ambayo mwanasiasa huyo anayatoa kuzuia chama chake kutoikataa moja kwa moja matokeo ya kazi ya Kamati hiyo.


Kitendo cha Mbowe kutaka wananchi waamini kwamba Kamati hiyo haiwezi kutoa ripoti yoyote ile ya maana kama masharti ya chama chake hayatatimizwa ni cha kuupotosha umma.


Masharti ya Mbowe ni pamoja na kuwekwa hadharani kwa ripoti za Tume na Kamati zilizotangulia, suala la uharibifu wa mazingira, haki za binadamu katika maeneo ya machimbo, kutenguliwa kwa wajumbe 'wachafu' n.k.


Orodha hiyo ndefu ya masharti ya kiongozi huyo wa CHADEMA yameelekezwa kwa Rais Kikwete.


Tatizo hapa si masharti kwa Rais Kikwete. Pengine hayo masharti yangeweza kupuuzwa tu. Lakini ukweli ni kwamba Mbowe anahusisha masharti hayo na kazi ya Kamati. Yaani Rais Kikwete asipotimiza masharti yote nane aliyoyatangaza Mbowe kwa waandishi wa habari basi hiyo Kamati haina sababu yoyote ile ya kukutana kwani haiwezi kutoa matunda yoyote yale ya maana.


Mbowe anataka watu waamini kwamba Kamati iliyoundwa na Rais Kikwete ni ya kupoteza wakati tu na kwamba ili isiwe hivyo, masharti aliyoyataja yatimizwe.


Lakini katika kuthibitisha kwamba CHADEMA ilikuwa inajiandaa kuchomeka sana katika spoku gazeti la Tanzania Daima toleo la Jumapili Novemba 25 liliandaa njia kwa ajili ya Mbowe kupita.


Tanzania Daima Jumapili lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na wasomaji wake kujua nini maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu. Gazeti hilo lilitoka na habari kubwa ukurasa wa kwanza; ‘Zitto aruka kihunzi.' Habari hiyo ilikuwa ikielezea kwa kina kwamba kikao kilikuwa kimeridhia Zitto kuendelea na uteuzi katika Kamati ya Madini.


Sanjari na habari hiyo hata hivyo, kulikuwa na habari nyingine iliyokuwa na uzito karibu uliolingana na hiyo hapo juu. Habari hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho ‘CCM, JK waitega CHADEMA kinamna.'


Wakati habari ya kwanza inazungumzia Kamati Kuu ya CHADEMA kuhitimisha ‘mvutano wa viongozi wa chama hicho uliodumu kwa siku kadhaa kuhusu ushiriki wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto, katika kamati ya kupitia upya mikataba ya madini iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, habari hiyo nyingine ilikuwa ikisema: ‘Sasa ni dhahiri kwamba jitihada za vyama vya upinzani kukipoka madaraka Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 au hata 2015 zipo kitanzini.


Ni wazi kwamba habari hiyo ya kuonyesha kwamba kuna njama dhidi ya upinzani na hasa dhidi ya viongozi wanaoinukia wa CHADEMA inalenga katika kuhalalisha mgogoro ulioanzishwa na viongozi wenyewe wa chama hicho.


Katika migogoro ya kisiasa jambo moja huweza kufanyika, nalo ni kuibua mgogoro mpya wa nje kama njia ya kufunika mgogoro wa ndani.


Hatari ya kutumia mbinu hiyo ni kwamba katika kuhalalisha kuwapo mgogoro kutoka nje, unaweza kujikuta ukiibua mgogoro mzito ndani ya chama husika.


Habari hiyo ni dhahiri kwamba inatoa tuhuma nyingi, si kwa chama tawala tu bali kwa viongozi ndani ya CHADEMA.


Lililo baya zaidi ni kwamba habari kuhusu kile kinachoitwa mtego walioingia CHADEMA inazungumzia kwamba Zitto amerubuniwa na Serikali, na hiyo imefanyika kutokana na ushauri wa magwiji wa fitina za kisiasa ndani ya CCM walioshauri "kumsogeza karibu zaidi na Serikali, Zitto, mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi kwa kumpangia majukumu mengi mazito ya kitaifa, lakini yenye maslahi bora kwake binafsi."


Maneno yaliyonukuliwa hapo juu ni yaliyochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima.


Tuhuma zinazorushwa kwa Zitto na gazeti hilo ni nzito. Kwamba sasa ‘Zitto ambaye nyota yake inang'aa, ndiye anayelengwa kwa nia ya kumfanya silaha muhimu ya kuisambaratisha CHADEMA…si suala la mjadala wa siri.'


Kwamba kwa Zitto kushirikishwa katika shughuli kama vile Kamati ya Madini ni kumtumia ili kuisambaratisha CHADEMA, pengine hili linahitaji ufafanuzi wa kina kutoka kwa wanaozirusha tuhuma hizo.


Kinachotokea hivi sasa ni kwamba Zitto anatupiwa lawama nzito na viongozi wanaotanguliza maslahi binafsi mbele katika chama chakeKwa nini leo hii kuteuliwa kwa Zitto kuchukuliwe kwamba ni kurubuniwa na kuteuliwa kwa mtu mwingine iwe ni sawa na halali na busara isiyomithilika? Kuna jambo limejificha hapa ambalo halizungumzwi.


Si tu kwamba katika habari hiyo ya gazeti Zitto alifanywa kuonekana kama msambaratishaji wa CHADEMA ambaye anatumiwa na CCM, bali pia ilijengeka taswira nyingine kwamba kijana mwingine wa chama hicho naye amepangwa ‘kushughulikiwa kwa staili ya Zitto'. Kijana huyo ni Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA, John Mnyika.


Kwa kujaribu kueneza habari za kuonyesha kwamba CCM inalenga kuwarubuni vijana hao ni kuwajengea woga ili washindwe kujipembua kitaifa, kwani pamoja na kujitokeza na kuonyesha vipaji vyao katika majukwaa ya siasa, ni wazi kwamba kwa kushiriki katika shughuli za kitaifa kama vile tume na kamati teule za Rais vijana kama hao watapaa maradufu katika ulingo wa siasa. Jambo hilo bila shaka linawatisha baadhi ya viongozi katika chama hicho.


Ni wazi kabisa kwamba hicho kinachoitwa njama za CCM ni jitihada za baadhi ya viongozi ndani ya CHADEMA kutaka kuzuia kuibuka kisiasa kwa baadhi ya vijana ambao wana uwezo wa kujieleza, uwezo wa kuchambua mambo kwa uyakinifu na hivyo kuwa na mvuto kwa wanachama wa chama hicho na wananchi wengine sawia.


Ni wazi kwamba kama ndani ya CHADEMA hakutatokea watu walio jasiri na kumulika kwa undani mwenendo mzima wa baadhi ya viongozi, basi hakuna uwezekano wa kukipoka Chama Cha Mapinduzi madaraka, si kwa sababu ya ghiliba na ujanja ujanja wa chama hicho, bali kutokana na kupoteza muda katika masuala yasiyokuwa na maana. Kutangaza kwamba CCM inatumia ghiliba na mbinu kuwarubuni vijana ndani ya CHADEMA ni kuanzisha mgogoro ndani ya chama. Huo ni mgogoro ambao unalenga ama katika kuwaengua vijana hao kutoka katika safu za uongozi wa chama hicho au unaolenga kuhalalisha kushindwa kwa uongozi wa chama kuwa na mikakati endelevu ya kupambana na CCM.


Unawezaje usiwe na mgogoro wa uongozi ndani ya chama kama wale wanaoibuka na kuanza kujipembua kutokana na umahiri wao katika siasa na hususan katika kujieleza kwa umma wanaonekana kwamba ni watu wa kurubuniwa?


Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili kuhusu njama za CCM za kuwarubuni vijana wa CHADEMA unahitaji kuanikwa kwa kina zaidi. Kama ni kweli, CCM imemrubuni Zitto na ameingia kwenye mtego wao basi ijulikane hivyo lakini kama si kweli basi aombwe msamaha. Au ni dhambi kuwa kijana mwanachama wa CHADEMA na halafu ukajipembua kama muweza wa masuala ya kisiasa? Kama ni hivyo, basi na ijulikane hadharani.


Kuna dhana inayojengwa na Mbowe na wenzake kwamba kuna wapinzani wa kweli na wapinzani feki. Wapinzani wa kweli ni wale wanaokubaliana na Mbowe na fikra zake na walio feki ni wale ambao wana fikra tofauti. Aidha, hata uzalendo nao unazungumzwa katika kutaka kuonyesha kwamba kuna watu wanaipenda Tanzania zaidi ya wengine.


Source: Rai 29 Nov 2007

Huyo ni Dr Gideon Shoo. Simfahamu sana huyu jamaa zaidi tu ya kusoma makala zake kwenye Rai kwa miaka mingi. Wenye data zake hasa kuhusu wasifu wake, hebu tupatieni itusaidie katika kulinganisha yanayosemwa na credibility ya msemaji. Mwauonaje huu mjadala anaouanzisha Dr Shoo?
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom