Media(magazeti,radio na television,) zinazofungiwa na serikali zinapaswa kuwa zimekiuka haya

Samweli Mathayo

JF-Expert Member
Aug 1, 2017
1,577
1,700
Hivi sifa la gazeti linalopaswa kufungiwa ni kama hizi
Mosi
*likichochea ugaidi au likaonekana linasapot ugaid katika nchi husika*

Pili
*ikigundulika linatumiwa Na wahujumu uchumi ilo ni la kufunga, siyo wahujumu uchumi kwa tafsiri ya watanzania no, ni kwa wahujumu uchumi kwa tafsiri ya kweli*

Tatu
*Ikigundulika linasapot ushoga ilo ni la kufunga kabisa*

Nne
*ikigundulika lina ondoa maadili, linatuma picha za uchi Na zisizo faa ilo la kufungwa,*

Tano
*kama linatumika kutangaza matapeli ilo linafungwa*

Sita

*kama linatumiwa Na watu wa nje kuhujum taifa ilo lifungwe*

GAZETI LINALOMSINGIZIA RAIS, AU LINALOSEMA UDHAIFU WA RAIS, AU UDHAIFU WA SERIKALI, AU LINALOSINGIZIA MALI ZA NCHI KUKAMATWA ILO LIACHWE MAANA HAYO YANAELEZEKA NA YANATHIBITISHWA KUWA SIYO, UWEZO WA KUTHIBITISHA UPO*

Kwa dunia ya sasa wajanja hawaangaiki Na magazeti au kufungia media, wajanja uangaika kujibu hoja zilizoibuliwa Ama za ukweli Ama uongo,

Upotoshaji unafaida yake, upotoshaji ufanye serikali iwe makini kwa majibu inayotoa, ufanya hata kupata sifa ya ziada kwa aliyesingiziya maana kupitia kuchunguza utagundua yaliyosemwa siyo,

Wakuu narudia kwa suala la *globalization* ni vigum mno kucontroll media,

Wajanja hawaangaiki Na magazeti,,kipindi Cha nyuma nilikuwa naudhuria sehem wanuza magazeti napingana na watu sana, Na kipindi hicho nilikuwa napinga habari za MAWIO, lakin sikuwahi kuomba lifungwe,
Maana dunia ya utandawazi sasa huwez zuia watu kupata habari hata kupotosha,

Mpaka sasa ukienda TCRA
1. Hawajui idadi ya blogs zilizoanzishwa Na watz
2. Baadhi ya server za Media haziko Tanzania, hata upotoshe vip hautajulikana ,

3. Wamiliki wa media wengine wamesajiri Na kuajiri watu wasio na weledi eti kisa aliwahi kuwa mwanamziki au mchekeshaji tumuajiri, au anachambua sana mpira tumuajiri, Tanzania this is nonsense ndo wanaandika uongo, upotoshaji,
Pamoja Na kwamba huwezi zuia madhara ya globalization lakin unaweza regulate,

4. Facebook Na Instagram limejaa watu wanatangaza uchangudoa hawafuatiliwi kuna watu wanawarubuni watoto wa shule hayo kwa serikali ya Tanzania si makosa, makosa ni kujadili serikali tuwe wakweli

Madhara ya upotoshaji ni mabaya kama aliyesingiziwa Hana uwezo wa kujitetea au Ku proove kwa alichosingiziwa, lakin upotoshaji ni mtamu mno kama alosingiziwa Na chombo Cha habari ana uwezo wa kuprove kuwa kasingiziwa


Haya sasa

KOSA LA TANZANIA TCRA HAWAFANYI HAYA
1. Anayeanzisha gazeti au radio anapaswa kupresent hata cv za alio waajiri

2. Apewe mwongozo wa nchi

3. Pili anayesajiliwa ale kiapo Cha kutolitumbukiza taifa katika matatizo,

4. TCRA wapange faini kwa atakaye bainika kupotosha, asifungiwe Ila asaidie kuongeza makusanyo ya TRA hii inasaidia sana maana mmiliki akilimwa milion 80 kwa kupotosha, naye atakuwa makini Na waajiri wake , kwanza hata mafao ya aliyeandika uzushi uo atayasikilizia kwenye bomba,

Makala zote zinazoandikwa wanaoandika wasitumie majina fake, yawe majina halisi kwenye magazeti, hapo tutasonga,

5. Portal ya ufunguzi wa website Na YouTube application iwe Na sehem ya utambuzi wa mmiliki halali, Na gateway imtambue, hapo tutafika,
 
Back
Top Bottom