Media kususia habari za fulani: Je, Tanzania tuna Independent Media yenye jeuri hiyo?

Mkuu Waberoya, wako wengi tuu, sio busara kuwataja kama una access na mtandao wa NECTA, fuatilia mwandishi huyu mwenye Index No. S. 347/120 alisoma O-Level Tambaza akatoka na Div 1 kali, akaenda A-Level Ilboru kwa Index No. S. 110/539 pia akatoka na Div 1, akaenda TSJ akatoka na Diploma in Journalism No 0000670 yenye 1st class na baadaye akajinga UDSM kusomea sheria LL.B na kutoka na Upper 2nd!.

NB. Journalism is a noble profession, umahiri wa mwandishi kuwa mwandishi/ mtangazaji mzuri ni kipaji binafsi cha mwandishi husika na sio vyeti. Kipindi chote cha Nyerere, na Mwinyi, kusomea journalism ilikuwa mwisho ni Diploma tuu, degree zilitolewa kwa waliosoma nje ya nchi enzi hizo USSR, walirudi na Masters, lakini wengi kwenye performance walikuwa hakuna kitu!.

Wakati the best in the industry wengi wao ni shule za kuunga unga na elimu za hapa na pale!. Hata Ben Mkapa, Prof. Palamagamba Kabudi, Dr. Sengodo Mvungi, Dr. Harrison Mwakyembe, Dr. Aggrey Mlimuka, wote walikuwa ni waandishi wa habari.

Paskali
Umehakikiwa lakini?
 
Yangu ni mafupi tu.

Tangu Mhe. Paul C. Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam atuhumiwe kuvamia kituo cha radio na runinga cha Clouds, mengi sana yameibuka. Muhimu kwa muktadha wa bandiko langu ni kuwa Jukwaa la Wahariri Tanzania lilitoa tamko (ingawa siyo la kisheria) kwa vyombo vya habari kutoandika wala kutangaza habari zozote za Mh. Makonda. Hata humu wanachama wengi (ambao naamini kwa itikadi za kisiasa) waliunga sana mkono tamko hilo la Jukwaa la Wahariri. Juma lililopita kituo cha runinga cha Star cha Mwanza kikato tangazo la kuandaa kipindi maalum na Mh. Makonda. Kama kawaida humu kukajaa kejeli na kashfa kibao dhidi ya Dr. Anthony Diallo, mmiliki mmojawapo wa Sahara Media Group utadhani yeye ndiye muandaa vipindi. Wanachama wengi sana ukiwasoma walikuwa wanamsimamo kwamba wasingetazama kabisa wala kufuatilia mjadala huo. Asubuhi hii ya leo, mwanachama mwenzetu akatuletea uzi wa moja kwa moja kuhusu mahojiano hayo. Ile uzi umefika nadhani ukurasa wa 10 au 12, ukaondolewa bila maelezo. Naamini hii kwa JF kuungana na tamko la Jukwaa la Wahariri. Hata hivyo habari za Makonda zimeendelea kujaa humu na kumbe kilicho wazi ni kuwa hao waliosema hawatazami kipindi ndiyo wanaleta taarifa za kumtukana tena Mh. Makonda kwa mahojiano yake ya leo.

Hii inatufunza nini? JF sasa nayo inakosa mizania katika maamuzi. Inaonekana kabisa kuwa Mh. Makonda ni habari (iwe hasi au chanya) na anafuatiliwa sana wan wanachama wengi humu. Sasa kwa nini JF itunyime haki ya kufuatilia uzi mubashara wa tukio la leo? Kumbuka kaulimbiu ya humu "Where We Dare To Talk Openly", zamani tukisema "kumkoma nyani giladi" enzi za Jamboforums.

Wanachama wengi humu wanamaanisha wasichosema. Tumeshuhudia mara kwa mara wakisema hawatazami TBC, wao wakiita TBCCM, lakini ndiyo wa kwanza kuja kukosoa habari zinazotangazwa TBC. Hivyo hivyo wengi wamekuwa wakiitukana sana Clouds Media kabla ya mtifuano wao na Mh. Makonda, ajabu baada ya mtifuano, Clouds Media imekuwa pendwa, ingawa leo tena wametukanwa humu. Habari ni hiyo hiyo kwa Star TV, n.k.

Uongozi wa JF bana msijiingize kwenye siasa za vyama. Sisi wanachama wenu tunataka habari. Kusimamia mambo yasiyokuwa na msingi wa sheria ni kubagua habari. Natoa tu mfano wa nyuzi za leo kuhusu mjadala wa Makonda na Star TV mjue kuwa hata hao mnaodhani mnao msimamo pamoja, wamekuwa wakifuatulia mjadala huo kwenye tv na radio.

Bashite/Startv: Waandishi wa habari mjiepushe na utakatishaji habari/taarifa(news laundering)

Bila unafiki; Makonda leo Sikutegemea haya kuyafanya wewe!!

Tunakosea kumchukulia "serious" RC Makonda

https://www.jamiiforums.com/threads...ina-mengi-muongezeeni-mzigo-mwingine.1254638/

Sakata la Bashite: TLS nendeni Mahakamani mapema

Uhuru wa habari: Je, TEF na MOAT kumfungia RC Makonda ni sahihi?

Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF

Kwa uchache nimetaja tu hizo nyuzi ambazo hazina juma moja tangu ziwekwe humu. Ninaamini uongozi wa JF una cha kujifunza. Usichukue upande katika maswala haya ya kupashana habari. Mona wamiliki mmeakamatwa na Polisi mara kwa mara na hamjazuia taarifa za kuhusu Jeshi la Polisi kuandikwa humu?

Si ajabu hao kina Deo Balile na wenzake wa Jukwaa la Wahariri walikuwa wanafuatilia mjadala huu na kesho watoe taarifa "in details" kupinga mjadala huo hala nyinyi humu mnatuzibia.
 
JF wanafanya vizuri kufuata maazimio ya wahariri Tanzania kwa kuwa wao ni chombo cha habari huyu MTU ni adui wa tasnia ya habari acha atumikie adhabu yake ili iwe fundisho kwa wengine wenye madaraka ya kulevya
 
Diallo amempa home boy wake kamba ajinyonge mwenyewe, naamini kuanzia sasa hata Magufuli mwenyewe hatomchukulia jamaa serious.
 
Naendelea kusema mnaotumwa na serikal yakiikuta family yako ndo utajifunza kutumia ubongo
Tz umaandaz unasumbua sana an ww unatetea mtu hata milion yake hajawai kukupa
nmezoea matus ila nmekustahi
 
Naunga kwa nguvu zote hoja yako. na ninakubaliana na mtoa mada bila kukosa % yoyote. ila sisi wana jamvi ikumbukwe si waANDISHI WA HABARI. bali ni wasema" ovyo" nikimaanisha kuiunga ile rai ya jf isemayo" ...umesikia au kuona chochote weka hapa..." so, jf inapojiambatanisha na waandishi binafsi nashangaa.
 
Ikumbukwe kuwa jf ni mtambo wa kurekebisha tabia na vile vile kufundisha. kwa hili la kutoa thread kisa makonda. Ah!
 
Mleta mada umemsaidia mhusika katika kuboresha kitabu chake na mkewe cha vita ya madawa na changamoto zake.

Elewa tu kitu kimoja kwamba mwenyewe leo amezungumza kwa jazba juu ya kupuuzwa kwake na wakati huo huo akiendeleza ubabe wake.

Kwa kuwa umeamua kumsemea elewa tu kwamba huyo bwana ameshindwa kuwa muungwana hivyo asilazimishe watu wafuate njia anayoitaka yeye.
 
Back
Top Bottom