Media kususia habari za fulani: Je, Tanzania tuna Independent Media yenye jeuri hiyo?

Mimi pia nashangaa Sana, hivi inakuwaje vyombi vya habari eti vinasusia kuandika habari za kiongozi wa kitaifa kisa kavamia kituo cha habari, cha muhimu hapa si kususa bali ni kumuandika zaidi na kumkosoa kwa alichofanya na ikibidi kumshtaki mahakamani, lakini kususia kuandika habari zake kwanza ni kuwakosesha wananchi kupata habari za kiongozi wao ambazo ni haki yao kikatiba.
Hapa naona hivi vyombo vya habari vinavunja katiba kwa kuwanyina watz habari za kiongozi wao, Kama mimi ningekuwa na mamlaka ningezifutia leseni zao halafu tuone watakula wapi.
Nawapongeza Sana Sahara media Kama wameamua kuachana na upuuzi, duniani kote sijawahi kusikia kiongozi Fulani kasusiwa kuandikwa habari zake kwa sababu yoyote ile, juzijuzi tu hapa Trump wa Marekani alivishutumu vyombo vya habari sana na kuvituhumu kuwa vinaandika fake news na alidiriki hata kutoviruhusu baadhi ya vyombo vya habari tena vikubwa Kama BBC na CNN kutohudhuria kwenye sherehe iliyofanyika white house kwa sababu alivituhumu, mbona hivo vyombo vya habari havijamsusia kuandika habari zake? Huu ni upuuzi Mkubwa wa vyombo vyetu, sijui nani aliwashauri ujinga huu, najua mapovu yatawatoka.
 
kinachofanywa na hao waandishi kinanikumbusha kuwa jamii yetu bado haijavuka karne ya 12; huko kwa wenzetu mfano mzuri ni Trump; amefungia baadhi ya media kwenda white house lakini hatujasikia ujinga kama huu.
 
KIONGOZI WA KITAIFA KUSUSWA NA VYOMBO VYA HABARI ALIKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI WAKATI WA KIKWETE KAMA SIJAKOSEA.
SASA MWINGINE WA KITAIFA ALIYESUSWA NI NANI?
 
kinachofanywa na hao waandishi kinanikumbusha kuwa jamii yetu bado haijavuka karne ya 12; huko kwa wenzetu mfano mzuri ni Trump; amefungia baadhi ya media kwenda white house lakini hatujasikia ujinga kama huu.
ANGEVAMIA KWA MTUTU AONE.
 
Mkapa alikuwa akiwaita ''makanjanja wa habari''...na takwimu kwa mujibu wa Dr.mwakyembe zinaonyesha 90% ya wanaojiita wanahabari hawana taaluma ya habari. Eti ''wamesusa''.....!!!!bure kabisa.
Kwahiyo unashadadia upumbavu pole yako;!
 
kinachpendelea kwasasa no vita kati ya balile na makonda ,naikumbukwe kuwa balile inasemekana kuwa balile amepokea 14.2ml kutoka umoja wa wauza unga ili kumdhoofisha makonda kupitia Vyombo vya habari.
 
nitafutie mwanahabari mwenye div 1 ya chochote kile
Mkuu Waberoya, wako wengi tuu, sio busara kuwataja kama una access na mtandao wa NECTA, fuatilia mwandishi huyu mwenye Index No. S. 347/120 alisoma O-Level Tambaza akatoka na Div 1 kali, akaenda A-Level Ilboru kwa Index No. S. 110/539 pia akatoka na Div 1, akaenda TSJ akatoka na Diploma in Journalism No 0000670 yenye 1st class na baadaye akajinga UDSM kusomea sheria LL.B na kutoka na Upper 2nd!.

NB. Journalism is a noble profession, umahiri wa mwandishi kuwa mwandishi/ mtangazaji mzuri ni kipaji binafsi cha mwandishi husika na sio vyeti. Kipindi chote cha Nyerere, na Mwinyi, kusomea journalism ilikuwa mwisho ni Diploma tuu, degree zilitolewa kwa waliosoma nje ya nchi enzi hizo USSR, walirudi na Masters, lakini wengi kwenye performance walikuwa hakuna kitu!.

Wakati the best in the industry wengi wao ni shule za kuunga unga na elimu za hapa na pale!. Hata Ben Mkapa, Prof. Palamagamba Kabudi, Dr. Sengodo Mvungi, Dr. Harrison Mwakyembe, Dr. Aggrey Mlimuka, wote walikuwa ni waandishi wa habari.

Paskali
 
Heshima ya uongozi wa maRC na maDC imepotezewa na sifa au wasifu usioendena na uelewa wa majukumu yake.
 
Mkuu Waberoya, wako wengi tuu, sio busara kuwataja kama una access na mtandao wa NECTA, fuatilia mwandishi huyu mwenye Index No. S. 347/120 alisoma O-Level Tambaza akatoka na Div 1 kali, akaenda A-Level Ilboru kwa Index No. S. 110/539 pia akatoka na Div 1, akaenda TSJ akatoka na Diploma in Journalism No 0000670 yenye 1st class na baadaye akajinga UDSM kusomea sheria LL.B na kutoka na Upper 2nd!.

NB. Journalism is a noble profession, umahiri wa mwandishi kuwa mwandishi/ mtangazaji mzuri ni kipaji binafsi cha mwandishi husika na sio vyeti. Kipindi chote cha Nyerere, na Mwinyi, kusomea journalism ilikuwa mwisho ni Diploma tuu, degree zilitolewa kwa waliosoma nje ya nchi enzi hizo USSR, walirudi na Masters, lakini wengi kwenye performance walikuwa hakuna kitu!.

Wakati the best in the industry wengi wao ni shule za kuunga unga na elimu za hapa na pale!. Hata Ben Mkapa, Prof. Palamagamba Kabudi, Dr. Sengodo Mvungi, Dr. Harrison Mwakyembe, Dr. Aggrey Mlimuka, wote walikuwa ni waandishi wa habari.

Paskali

Asante kwa kunitoa ujinga, ila umetaja waliojiendeleza, maaba hata degree yake imeanzishwa karibuni tu

kikubwa wenye passion na hiyo kazi wako vizuri, wengi wao bado hawajielewi
 
Haya yote,ni wananchi walio wengi na taasisi kadhaa, kuichoka ccm !

Haya yote,ni kwaajili ya upendeleo,na wengine wakibaguliwa kwa uwazi kabisa,mabavu yanayo lazimisha watu wampende/wamkubali magufuli,unyimi wa haki
za msingi kama huduma za jamii,elimu ya juu,miundombinu kama barabara katika sehemu nyingi za nchi ni mbaya mno ! ,njaa,matiibabu,ambavyo vyote hivi vinagusa kila mtu,na zaidi sana maskini.

Hivyo kuona mwana ccm mmoja au wachache kama bashite,na wasiokaguliwa vyeti kwa visingizio vya kijinga,hii inazidisha chuki kwa ccm na utawala wake.

Sasa sio kunyimwa hayo tu ya habari,atanyimwa hata salamu.na akifiwa ataomboleza na ccm wake tu !

Sio siri mnajua kabisa hamkubaliki,ila ni kwakua mnatumia nguvu tu ya majeshi,bila hivyo,hali ingesha badilika siku nyingi sana !
 
Wanabodi,

Nikiwa mwana wa tasnia ya habari, leo nimelisikia tangazo la Jukwaa la Wahariri kususia habari za fulani. Swali ni Jee Tanzania tuna independent media yenye jeuri ya kuweza kususia habari za mtu fulani? .

Jibu ni hapana, hatuna hizo media japo nakiri tuna magazeti machache independent yenye jeuri hiyo ambapo hata mfalme akifanya vibaya yatasema loud and clear bila kumung'unya maneno na jf ni one of them.

Only some few media zenye independent editorial independence ndio zita implement hili la kususia kwa sababu wanayo jeuri hiyo ya kususa. Media nyingine zote zikiwemo media zote za umma, media zote za serikali, media za chama na media zenye njaa, zote hazina jeuri hiyo ya kususia.

Tusitegemee media kama TBC, RTD, Daily News, Habari Leo, Uhuru, Mzalendo, Radio Uhuru, Idara ya Habari Maelezo na mitandao ya kijamii, kususia.

Jambo kama hili limeishatokea huko nyuma baada ya kifo cha Daudi Mwangosi, kwa kuuliwa na polisi, ikaamuliwa habari za polisi zisuswe. Kususa huko kulidumu kwa siku moja tuu, na kesho yake walianza kugeukana.
Sababu ni hizi.
1. What is News?.
Kazi ya media zote ni kutoa kutoa habari, yaani kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha kwa lengo la kuihudumia jamii. Katika kufanya hayo, zikomedia zinayafanya hayo kama huduma (not for profit) na ziko media zinayafanya hayo ili kuishi, yaani ili kuuza gazeti, sasa kama huyo fulani ndio habari ya mujini inayouza gazeti, huwezi kuacha kumripoti utalala njaa, utakuwa hujatimiza wajibu wako na kubwa zaidi ni kuitendea haki jamii unayowajibika kwake.Hivyo hata leo mtashuhudia headlines zenye hilo jina.

2. Kwenye tasnia ya habari, kuna kitu kinaitwa "pressures shapping the news", hizi sio habari bali determinant factors zinazofanya habari fulani iandikwe na habari fulani isiandikwe!. Moja ya factor kubwa kuliko zote ni "money matters"!. Survival ya vyombo vingi vya habari sio circulation, sio readership, sio viewership au audience bali ni matangazo!. Watangazaji wakubwa wanaitwa sponsors ndio waamuzi wakubwa wa what is news na media lazima ziwasikilize. Hawa sponsors are the ones calling the shots!. "He who pays the piper, may call the tune". Huko ndiko mshahara utokako.

3. Big Names Make News, yaani jina kubwa linatengeneza habari kubwa. Sasa nyuma ya huye anayesuswa kuna "jina kubwa lipitayo majina yote" (Not Jina Kubwa Lipitayo Majina Yote) ambalo ni jina la yule 'malaika mlinzi' wake, hivyo kama atahakikisha kila tukio lake, atakuwa na 'mwanae mpendwa wake anayependezwa naye' na ndiye atakayekuwa akiongea kwa niaba yake kwenye kila tukio, nani atakuwa na jeuri ya kususa? au kumkwepa? ,atakuwa hakwepeki!.

4. Aandishi wa habari ni nobel professional yaani kazi ya wito, na kwa wengi ni kazi ya kuakuajiriwa, ni kazi ya kutumwa au kitumwa, waandishi ni watumwa tuu, kazi yao ni kutumwa!. Mtumwa hana uhuru wala ridhaa jukumu lake ni kutekeleza tuu matakwa ya masters wake!.Hivyo mtumwa akitumwa na bosi, ana jeuri gani ya kususa?
Kumlaumu mtumwa ni kumuonea bure!. Mtumwa ni mtu wa kutumwa tuu kuhurumiwa!.

Wengi wa waandishi ni watumwa tuu, hawafanyi kazi kwa utashi wao bali hufanya kwa utashi wa editor na editors ambao sio wamiliki wa vyombo vyao, nao pia ni watumwa tuu wa wamiliki, au waajiri wao, hivyo nao hawafanyi kazi kwa utashi wao bali utashi wa wamiliki "he who pays the piper may call the tune"!.

Taarifa zozote muhimu za msuswa sasa zinaweza zikaletwa kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, je nani watakuwa na jeuri ya kususa? .

Huko nyuma tuliwahi kujadili hili kwenye mada hiiWaandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya

Hivyo waandishi wa habari waajiriwa, hawana jeuri ya kususia habari za mtu yoyote kwa sababu ni watumwa, huko kususa, ni hasira za uchungu wa Clouds kuvamiwa, hasira zikipoa, wataendelea kuandika!.

Waandishi wa kujitegemea, tuko wa aina mbili, aina ya kwanza ni "freelance journalist", hawa wanaandika na kuitegemea hiyo habari ndio imlipe, newsroom nyingi zinalipa 3,000, 5,000 kwa habari moja itakayotoka, na labda 10,000 kama habari itakuwa ndio lead story!, huyu mwandishi akifanikiwa ku file story 1 tuu kwa siku na ikatoka, mwisho wa mwezi atavuta 90,000 tuu!. Waandishi wa kada hii ndio hutegemea "bahasha" to survive!.

Kada ya pili ni "independent journalists", kada hii ndiko mimi niliko, inahusisha kuandika just for the love of it, wengi wa kada hii tunazo shughuli zetu nyingine za kufanya kuendesha maisha yetu and to make our living, hivyo hatutegemei malipo yoyote kwa stories tunazotuma, mfano mimi silipwi hata senti tano kwa stories ninazofile kwenye media. Kundi hili ndio kundi kama la kina Mjengwa, Mzee Mwanakijiji etc, etc, enzi zile Mwanakijiji akitoa kile kijarida cha Cheche, alikitoa bure nasi tulikitawanya bure!. Kwa sasa Mjengwa, Mwanakijiji na wengine, ni waandishi wa makala mbalimbali kwenye magazeti mbalimbali. Kwa kawaida magazeti yanapaswa kuwalipa, sidhani kama wanaandika ili kujipatia hivyo vijisenti na I doubt hata kama wanachukua!. Kundi hili ndilo hatutumwi na mtu na hatumtumikii mtu zaidi ya jamii!.

Ila watu kama mimi kama Paskali, ni mwandishi wa kujitegemea, sijaajiriwa na yoyote, wala situmwi na yoyote, na siitegemei media yoyote kutumia habari zangu kwa sababu mwamuzi ni mimi ndio ninaamua habari gani niandike na media ipi nipeleke, kama ni gazeti, huamua gazeti gani nipeleke, au kama ni kwenye TV na redio, mimi mwenyewe ndio huamua pa kuipeleka!, hivyo nikiamua kugoma, naweza kugoma kiukweli kweli!, hivyo waandishi wenye uwezo wa kususia habari zozote ni wale tuu ambao sio "watumwa" yaani wale waandishi wanaojitegemea na sio hawa "watumwa" wanaotegemea vyombo vya habari!.

Bado naendelea kulia kuwa tuna tatizo kubwa humu jukwaani jf, kwa watu wengi humu tuna tatizo la kuukubali ukweli halisi unaitwa "is" na kuukumbatia ukweli tunaoutaka uwe unaitwa "ought". Mimi ni mtu wa mkweli wa ukweli halisi "is" na sio so "ought" ambao ndio ule ukweli ambao wengi wanaupenda use, yaani ukweli wa kujifurahishia.

Kususia huko kulidumu kwa siku moja tuu ya uchungu ule, amini msiamini kesho Bashite akiitisha Press Conference, hamtaamini macho yenu.

Let's hope for the best ya hiki kisuso this time, sijui kitadumu kwa muda gani na ni media zipi bold enough kususa!.

Hongera JF nilinote hili jina la Bashite limefutwa.
Paskali.
Mahojiano ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Daudi Albert Bashite, na kituo cha Star TV ni uthibitisho tosha wa hoja za uzi huu kuwa Tanzania hatuna media zenye jeuri hii. Hawa Star ndio wameonyesha njia, wengine watafuatia.

Na kesho ni front za magazeti yote.

Paskali
 
Back
Top Bottom