Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,567
- Thread starter
- #241
Nafanya follow up ya kususia habari za fulani.Wanabodi,
Only some few media zenye independent editorial policy, ndio zita implement hili la kususia kwa sababu wanayo jeuri hiyo ya kususa. Media nyingine zote zikiwemo media zote za umma, media zote za serikali, media za chama na media zenye njaa (ambazo ndio nyingi zaidi), hazina jeuri hiyo ya kususia habari za fulani!.
Tusitegemee media kama TBC, RTD, Daily News, Habari Leo, Uhuru-Mzalendo, Radio Uhuru, Idara ya Habari Maelezo na mitandao ya kijamii, kususia.
Huko nyuma tuliwahi kujadili hili kwenye mada hiiWaandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya
Hivyo waandishi wa habari waajiriwa, hawana jeuri ya kususia habari za mtu yoyote kwa sababu ni watumwa, huko kususa, ni hasira za uchungu wa kuvamiwa kwa Clouds media, hasira zikipoa, wataendelea kuandika habari za huyo msuswa.
Waandishi wenye jeuri ya kususia kuandika au kuripoti habari fulani ni ama sisi waandishi wa kujitegemea, au waandishi ambao ndio media owners kama kina Manyerere na Balile ambao wanamiliki gazeti.
Kwenye hii kada ya waandishi wa kujitegemea, tuko wa aina mbili, aina ya kwanza ni "freelance journalist", hawa wanaandika na kuitegemea hiyo habari ndio imlipe, newsroom nyingi zinalipa 3,000, 5,000 kwa habari moja itakayotoka, na labda 10,000 kama habari itakuwa ndio lead story!, huyu mwandishi akifanikiwa ku file story 1 tuu kwa siku na ikatoka, mwisho wa mwezi atavuta 90,000 tuu!. Waandishi wa kada hii ndio hutegemea "bahasha" to survive!.
Kada ya pili ni "independent journalists", kada hii ndiko mimi niliko, inahusisha kuandika watu wanaoandika habari au makala just for the love of it, wengi wa kada hii tunazo shughuli zetu nyingine za kufanya kuendesha maisha yetu and to make our living, hivyo hatutegemei malipo yoyote kwa stories tunazotuma, mfano mimi silipwi hata senti tano kwa stories ninazofile kwenye media. Kundi hili ndio kundi kama la kina Mjengwa, Mzee Mwanakijiji etc, etc, enzi zile Mwanakijiji akitoa kile kijarida cha Cheche, alikitoa bure nasi tulikitawanya bure!. Kwa sasa Mjengwa, Mwanakijiji na wengine, ni waandishi wa makala mbalimbali kwenye magazeti mbalimbali. Kwa kawaida magazeti yanapaswa kuwalipa, sidhani kama wanaandika ili kujipatia hivyo vijisenti na I doubt hata kama wanachukua!. Kundi hili ndilo hatutumwi na mtu na hatumtumikii mtu zaidi ya jamii!. Sisi ndio wenye jeuri ya kususa.
Ila watu kama mimi kama Paskali, ni mwandishi wa kujitegemea, sijaajiriwa na yoyote, wala situmwi na yoyote, na siitegemei media yoyote kutumia habari zangu kwa sababu mwamuzi ni mimi ndio ninaamua habari gani niandike na media ipi nipeleke, kama ni gazeti, huamua gazeti gani nipeleke, au kama ni kwenye TV na redio, mimi mwenyewe ndio huamua pa kuipeleka!, hivyo nikiamua kugoma, naweza kugoma kiukweli kweli!, hivyo waandishi wenye uwezo wa kususia habari zozote ni wale tuu ambao sio "watumwa" yaani wale waandishi wanaojitegemea na sio hawa "watumwa" wanaotegemea vyombo vya habari!.
Bado naendelea kulia humu jukwaani jf, tuna tatizo kubwa la kuukubali ukweli halisi "is" na kuukumbatia ukweli tunaoutaka "ought". Mimi ni mtu wa mkweli wa ukweli halisi "is" na sio so "ought" ambao ndio ule ukweli ambao wengi wanaupenda kuusikia, yaani ukweli wa kujifurahishia.
Kususia kifo cha Daudi Mwangosi kulidumu kwa siku moja tuu ya uchungu ule, hivyo amini msiamini kesho Bashite akiitisha Press Conference, hamtaamini macho yenu.
Let's hope for the best ya hiki kisuso this time, sijui kitadumu kwa muda gani na ni media zipi bold enough kususa!.
Hongera JF nilinote hili jina la Bashite limefutwa.
Paskali.
Paskali