Media kukampenia CCM, Mbinu gani mbadala itumiwe na CHADEMA?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Media kukampenia CCM, Mbinu gani mbadala itumiwe na CHADEMA??

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nicky82, Sep 2, 2010.

 1. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika kipindi hiki cha kampeni ambapo vyombo vyingi vya habari vikiwemo vya umma vimeamua kuegemea upande wa CCM, na vikipotosha habari dhidi ya upinzani, CHADEMA wanapaswa sasa kutafuta njia mbadala ya kufikisha ujumbe kwa wananchi badala ya kutegemea vyombo vya habari vilivyopo kwani ni wazi kuwa nyingi ya media zmeegemea upande wa CCM na pale inapotangaza habari za upinzani basi ni zile zenye negative impact kwa wananchi.

  Hapa ndipo umuhimu wa CHADEMA kutumia website yao, pamoja na blogs kama njia mbadala unapoonekana. Kama nilivyowahi kusema kwenye post moja juu ya swala hili, CHADEMA waweke picha za mikutano,Audio na Video za hotuba za mikutano ya kampeni ya Dk. Slaa.

  Sisi wachace tulio na access ya internet na wenye nia ya kuisuport CHADEMA, tutadownload baadhi ya hizi audio hizi na kuzisambaza kwa watanzania wenzetu kama vile nyimbo za bongo fleva zisaambavyo kwenye viselula vyetu. Na kwa vile simu za kichina zipo hadi vijijini, maneno hayo ya hotuba hata kama ni ya dakika moja yatasambaa kwenye simu za watz nchi nzima kwa muda mfupi sana.

  Wengine tutadown hizo video na kuziburn na kuwapa wamachinga wazigawe cd bure mitaani. Kampeni hii itakuwa na nguvu kuliko kutegemea airtime kiduchu ya vyombo vyetu vya habari. Natamani kuona CHADEMA wakitumia mbinu hii kama njia mbadala ya kusambaza habari, lakini speed yao katika hili bado ni ya polepole.
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hili jambo zuri wanaweza hata Slaa akarekodi point muhimu ama kurekodi moja wa mikutano mahiri na kutuma sehemu waizo fika au hata kabla hawajafika kuwapatia wananchi wasikilize either kwenye mikutano au hata nyumbani .
  Wananchi waeleze kwa nini CCM hii sio ile waliyoitegemea kabla ya Mafisadi tena zipelekwe kule ambako wameshapita pia.
  Kufyotoa CD sio gharama kihivyo kwa sasa please Chadema fanyani hivyo ,its a WAR.
   
 3. e

  emalau JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu Vicky82 umetumia muda kufikiri kitu bora, Usishangae CCM wadesaji na walivyokosa ubunifu wakaidaka juu kwa juu wakaitumia wao. Strategist wa CHADEMA inabidi waende kwa spidi kali kuitumia.
   
 4. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuko pamoja mkuu, marekebisho kidogo tu hapo kwenye color, ni Nicky82.

  CHADEMA we are waiting for this!!
   
 5. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
 6. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Rutunga M, nimecheki hapo kidogo nitapike! Kichefuchefuuuuuuuuuuuuuu!
   
 7. comp

  comp Member

  #7
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo idea ni nzuri. leo nimenunua nipashe pale juu kuna picha ya Dr Slaa lakini ndani sijaona hata habari yake moja, wakati tunafaham jana kafanya mikutano.Its like alikwenda kiteto akapiga picha tu then akaondoka bila kucampaign. inasikitisha sana. Hawa watu wa media sasa wanapoelekea ni kubaya. wawe fair kidogo.
   
Loading...