Media Inapodhihaki Shida Za Watu Kwenye Siku Ya Wajinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Media Inapodhihaki Shida Za Watu Kwenye Siku Ya Wajinga

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by maggid, Apr 1, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  LEO NI SIKU YA WAJINGA, hata hivyo, ninachoandika hapa si utani wa Siku ya Wajinga. Ni jambo linalonikera, naamini, tuko wengi tunaokerwa juu ya namna media ya Tanzania inavyoitumia Aprili Mosi kuwasumbua wananchi wengi kwa utani unaowapelekea wananchi hao , wengi wao wakiwa na unyonge wa kiuchumi, kutaabika zaidi. Hii ni cynicism kutoka upande wa media.

  Nitoe mifano michache; asubuhi hii Redio Country FM hapa Iringa imekuja na taarifa yenye kuwataka wananchi kuitikia ‘ofa’ iliyotolewa na Redio hiyo kwa watu kusafirishwa kwenda Loliondo kwa Babu juma lijalo. Kwamba watu hao waripoti kwenye ofisi za redio hiyo ifikapo saa nne asubuhi. Masikini, kuna wataohangaika kuiwahi ‘ ofa’ hiyo.Cynicism.

  Televisheni ya Channel Ten wao wamewataka vijana wafike kwenye ofisi zao ifikapo saa nne ili wafanyiwe usahili kwa kazi ya utangazaji. Masikini, katika kipindi hiki cha mahangaiko ya vijana kutafuta ajira, kuna walio kwenye Daladala asubuhi hii kuwahi zilipo ofisi za Channel Ten. Cynicism.

  Na magazeti nayo hakubaki nyuma. Kuna yaliyoripoti kuwa Babu wa Loliondo katua Dar. Lingine likachagiza kuwa Babu ameamua kutoa kikombe leo kwenye viwanja vya Jangwani. Kuna wagonjwa na wenye kuuguza wagonjwa watakaotaabika na taarifa hii. Cynicism.

  Bila shaka kuna mifano mingine ya namna media inavyoitumia siku hii kudhihaki shida halisi za watu wetu walio wengi. Tabia hii ikemewe vikali. Si maadili mema.

  Haya mambo ya kuiga kama Siku ya Wajinga yana wenyewe. Na wanapoyafanya wanatanguliza utu pia. Hata habari kuwa “ Kikombe Cha Babu” kinatibu UKIMWI na Saratani kwa wenzetu wangeisoma leo magazetini wangesema ni utani wa ‘ Siku ya Wajinga Uliokosa Ladha!|” Cynicism.


  Media yetu inapaswa kuwa makini. Hili la kudhihaki na matatizo ya watu ikiwamo masuala ya afya linaweza kuwa na athari mbaya kwa media yenyewe. Watu wakakosa imani na media. Inatosha kwetu kusoma na kusikia mara kwa mara habari zinazofanana na za ‘ Siku ya Wajinga’.

  Watu wakichanganywa zaidi na habari zisizo za kiweledi na utu katika siku kama ya leo, basi, watashindwa kutofautisha ipi ni habari ya kweli na ipi ya uongo hata katika siku za kawaida. Na huu ni ukweli wangu niliotaka kuusema. Ni mtazamo wangu .  Maggid
  Iringa,
  Aprili Mosi, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  I second you.
   
 3. haibreus

  haibreus JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 296
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  For sure i support you,unajua unapoamua kutumia media kutangazia umma ujinga si kitu kizuri hata kama ni utani,wananchi walio wengi hawana habari na hata baadhi tarehe hawazijui kulingana na hali iliyopo ya ki maisha,hivyo ningependa kuungana na ndugu yangu juu hapo kukemea vikali hii tabia,nadhani kama unataka kutania watu au kuwafanya wajinga basi tumia njia ambayo haitakuwa na madhara kwa uchumi wao.
  Naunga mkono hoja.asenti
   
 4. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2011
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Ki ukweli mi nimewaambia wa2 atakaenidanganya nikabaini kwel tutagombana
   
 5. EMM_411

  EMM_411 Member

  #5
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mmeshadanganywa wote....... Fooools day!
   
 6. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwenyewe nimeuliza swali hivi chanzo cha hii siku ni nini na km ni sikukuu inasherehekewa wap kitaifa? Majid naona unasema sikukuu hii ina wenyewe, wenyewe ni kina nani?
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  nimepigiwa simu usiku wa leo kama saa kumi hivi na mdada mmoja tunao ofcn......ananiambia kuwa mke wangu amepata ajali ya gari na kuwa wamekilbizwa hosp....ki ukweli mke wangu yuko safarini....huyu dda anasema ameona breaking news kwenye tiv usiku huu.....akaniambia kaka fatilia ujue wifi kama yuko hai au la......ndugu zangu nimekurupuka nikaanza kupiga simu hadi kwa wazazi wake huko (poland).....ndipo mdogo wangu yuko bukoba akaniambia..unajua kaka leo ni tar 1 siku ya wajinga huenda anakutania huyu.....baada ya kumpata kwenye simu my wife wangu....tukaongea na kuniambia yuko amelala na yu salama......

  sikuweza kulala tena ila nilianza kufanya mazoezi nikaoga na nikaja ofcn..moja kwa moja hadi ofc ya yule dada aliyenipigia simu....sikumkuta..nikasubiri hapo nje...baadae akaja aliponiona akaanza kucheka.....mi nilikuwa nimevaa sura ya mbuzi (hasira) nimemtandika makofi ya haja nimempiga sana......kuna utani jamani lakini sio kama huu wa kufiwa na kupata ajalia hata kama leo ni siku y wajinga......amerudi hosp na hapa ofcn nimewaleza sababu za kumpa kichapo ....hata HR na MD wamesema amekosea kusema uongo wa aina ile....kikubwa ameambia akapumzike home nami nikojob napiga kazi
   
 8. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Ni ujinga na sidhani kuwa ni maadili/sheria kwa chombo cha habari kuudanganya umma kwa kukusudia. Sidhani kama wataweza kubeba gharama za uharibifu/madhara yatakayotokea.
  Je siku hii rasmi? Kama ni ndio ni wangapi wanajua kuhusu hilo!
  Yafaa kuzingatia maadili kila wakati kuepusha usumbufu kwa watu. Tusiweke nayo kuwa siku kuu ya kitaifa. Labda tunataka kudhihirisha kuwa tu wajinga kiasi gani.
   
 9. chloe.obrain

  chloe.obrain JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!!! hii sio nzuri kabisaa, pole sana kaka.
   
 10. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #10
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja!
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Huyu ndugu ana bifu na kikombe cha babu tokea siku nyingi
   
 12. s

  sawabho JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280


  Hata wewe hapa umedanganya, hakuna ofisi yoyote inayoruhusu mtu kujichukulia sheria mkononi kiasi cha kumtandika mwnigine makofo halafu aendee kuchapa kazi, sasa hivi ungekuwa unawapigia wenzako kuja kukutoa polisi post. HATA KAMA MTU KUUDHI NAMNA GANI KWA SHERIA ZA KAZI KUPIGANA UFISINI NI MARUKUFU. USIWADANYE WATU WAJECHUKUA SHERIA MGUUNI SIKU NYINGINE, WEEEE, UTAVUA MKANDA. Halafu, huyo mkeo kutoka Poland ulimwoa lini vile? Ina maana yule classmate wangu ulimwacha na kuchukua Mtasha!!! Na kwa nini useme poland, mke si mkeo tu kwani lazima cc tufahamu kuwa ni Mpolish. YOTE HAYO NI APRIL MOSI TU.
   
 13. S

  Songasonga Senior Member

  #13
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Edson ungeua wewe ndio ungekua mjinga tujifunze pia ku control Hasira zetu pole lakini
   
 14. H

  Haika JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  hii siku ya wajinga watu wanaojuana, au marafiki ndio inafaa wafanyiane, si media hata kidogo.
   
 15. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #15
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakushangaza TCRA wametulia tuli kama hawapo juu ya upotoshaji unaofanywa na media kwa jamii ktk hii siku ya april1.
   
 16. P

  PWERU Member

  #16
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri kujali shida za wengine,Wanahabari kuweni makini wagonjwa wanahitaji faraja na si usumbufu.Fikria ingekuwa wewe ndo unaumwa au unatafuta ajira ungejisikiaje unapodhihakiwa?
   
 17. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Utani hautanikiwa kwenye formal channels mfano, daktari hawezi kuwaatalifu jamaa kuwa mgonjwa wao kaaga dunia afu adai ni utani wa siku ya wajinga. utani ni kwa watu wa karibu sana tu. So media imekosea. Any way nadhani nao wameonyesha ujinga wao.
   
 18. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mwongo weweee...Mwongo...Huwezi mpiga mtu wewe....Mwongo..Ungekuwa selo sa hizi
   
 19. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Kuanzia mtoa hoja hadi mchangiaji wa mwisho wamedanganya,mfano mleta hoja anapolaumu Media kumislead watu bila kujua media inaongozwa na watu of whom haya mambo ya kijamii yanawagusa. SMU kaunga mkono pasi kujua km kadanganywa ama la! Haibreus terms na condition zizingatiwe...kwamba km aliyedanganya kakidhi vigezo vya kudanganya basi uwongo aliosema una ukweli/una baraka ...Manuu amedanganya kwa kua asingeweza kutahadharisha watu wote...Edson kadanganya kumpiga mfanyakazi mwenzie bila kuchukuliwa hatua na hakuweka wazi uhusiano wake na huyo mfanyakazi hadi ampigie simu usiku wa manane! Buswelu naye kadanganya kwa kukataa hoja ya Edson bila kufanya utafiti na finally nami nimedanganya kwa kua nimekiuka terms na conditions za kudanganya!
   
 20. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Ina maana HR na MD wako ni vilaza kiasi cha kukuunga mkono kwa kosa kumpgia huyo dada ofcn? Kwa mtazamo wangu hiyo ni fasihi simulizi tu. Haina ukweli wowote!!
   
Loading...