Media inafaidika nini kudanganya Umma? Waliokufa ajali ya Matumbi ni zaidi wengi ajabu.

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,637
458
Nadhani hili suala limewekwa kisiasa ili kutoua Trending Topics za nchi, na pia kutostua ujio wa ugeni wa Rais na wasindikazji wake kutoka sijui nchi gani ile.

Waliokufa (kwa mujibu wa walioshuhudia, mimi nikiwa mmoja wapo) ni zaidi ya 40, almost basi zima na wengine wamefia Hospitali.

Lakini vyombo vya habari vinatangaza tofauti, na watu wana-rely Media kupata habari bila kwenda kujionea Mochwari zilivyoshona mpaka mahospitali yanapeana Transfer.
 
Kiukweli mkuu hata mimi mwenyewe nilijua lazima kuna mambo ya kisiasa yamehusishwa katika taarifa. Yaani daladala ibondwe vile alafu mwisho wa siku mnasema watu wawili pekee ndo wamepoteza maisha?
 
Kiukweli mkuu hata mimi mwenyewe nilijua lazima kuna mambo ya kisiasa yamehusishwa katika taarifa. Yaani daladala libondwe vile alafu mwisho wa siku mnasema watu wawili pekeee ndo wamepiteza maisha?

wanasema eti walizimia.... walizinduka wote kasoro wa4 tu ndio marehemu......... hata kwa bunduki sikubali...
 
Kama kuna mtu aliangalia taarifa ya habari jana ITV unaweza kuonganisha dot ukajua hapa siasa imeingia, jana wakati wa taarifa ya habari yule mtangazaji alikwepa kabisa kutaja idadi ya watu akamuachia mkuu wa police ndo ataje ila ukiona body language ya mtangaza habari unajua kabisa hapa kuna siasa. Sijui huwa wanaficha nini? na hii ndo inapelekea kutochukuliwa hatua madhubuti ya kukomesha/kupunguza ajali za barabarani kwa sababu halionekani kama ni tatizo kubwa kwa sababu ukweli unafichwa sana.
 
mwenye idadi kamili ya majeruhi, na waliopoteza maisha atupe. vinginevyo media zitabaki kuwa sahihi
 
sasa kama wewe umeshuhudia ajali lakini umeshindwa kutoa idadi kamili unategemea nini..? kinyume cha uongo ni ukweli na kinyume chake kwa hiyo we toa taarifa uliyokuwa nayo ili kuweka mambo sawa. yaani siasa hizi zimewaharibu sana watu mwaka huu kila kitu wao wanaona siasa tu inawezekana hata mkeo akienda kwa mchepuko wake utasingizia mkeo anafanya siasa na mchepuko.
 
Mleta uzi acha papara wewe! Msipende kupata umaarufu kupitia maiti za watu. Mnataka kurudia tena ya kanda ya ziwa?? HAPANA, haikubaliki. Taarifa zilizotolewa mpaka jana jioni zilikuwa sahihi.
 
Back
Top Bottom