Media Freedom: Uingereza yausifu uongozi wa Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Media Freedom: Uingereza yausifu uongozi wa Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Informer, Sep 16, 2012.

 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,223
  Likes Received: 2,434
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Namsembaeli Mduma | HabariLeo | Sept 16, 2012

  SERIKALI ya Uingereza imeusifu uongozi wa Rais Jakaya Kikwete kwa kukuza demokrasia nchini, kutokana na uhuru unaovipa vyombo vya habari kuujuza umma mambo mbalimbali yakiwemo matumizi ya fedha za umma yanayofanywa na serikali yake.


  Aidha, imesema uwepo wa mawasiliano yasiyo na vikwazo kati ya wanahabari na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini, umechangia kuufanya umma ufahamu kinachoendelea juu ya rasilimali zake na kuhoji wahusika pindi inapobaini matumizi mabaya ya rasilimali hizo.

  Balozi wa Uingereza nchini, Duane Corner alizungumza hayo juzi wakati wa kufungua semina ya siku moja ya jinsi ya kuripoti masuala ya rushwa, yanayojitokeza katika ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa wanahabari na Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs).

  Alisema uhuru na uwazi huo usingekuwepo kama Rais na Serikali yake wangewanyima wanahabari uhuru wa kupata taarifa.

  "Demokrasia ya Tanzania inakua siku hadi siku kutokana na imani ya Rais Jakaya Kikwete kwa vyombo vya habari inayowapa fursa ya kuufikishia umma taarifa kuhusu matumizi ya fedha za umma. Kama angezuia hata CAG asingeweza kueleza anayoyavumbua katika ukaguzi wake…".

  Kwa upande wake, CAG Ludovick Utouh alisema ofisi yake inatambua umuhimu wa vyombo vya habari nchini ndio maana inavipa taarifa zote muhimu ambazo umma unapaswa uzipate.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Na source HABARI LEO.................................:third::flypig: NO COMMENT
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Aidha amesema vikwazo vilivopo katika upatikanaji wa habari katika ofisi za mkaguzi wa fedha za serikali ni kikwazo kikubwa katika upashanaji habari kuhusu matumizi ya fedha ya umma.
   
 4. A

  ADK JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1,147
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ye kaona huko tu mwambieni na yanayojiri kwenye maandamano ya vyama vya upinzani
   
 5. A

  Abuu- Amin Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 5, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe inaobgelewa fact ambayo ndo chachu hata ya wewe kujua ishu huwa zinakwenda vipi. Unaleta mambo ya kukaririshana vyama pinzani na maandamano!
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Uingereza wangepeleka nakala ya huo ujumbe wao kwa mjane wa Daudi Mwangosi na Saed Kubenea!
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  David Cameron at work, hajui Mwanahalisi iko wapi saiz au ndo ukishapenda hata chongo utasema ni kengeza...

  There is no way waingereza chini ya David Cameron wakamkosoa JK, hata mauaji ya kisiasa hawayaoni.
   
 8. r

  raymg JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Source yenyewe "Habari leo"......looks like a delayed pablication, ilitakiwa kabla ya 3 yrs ago
   
 9. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Credit should be given where it deserves, she has opined correctly....with all his shams and drugery JK still allows freedom kwa vyombo vya habari,

  Mwanahalisi might have fact, but on presenting them fact you couldn't differentiate (sp) with Shigongo's cheap tabloid
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu hayo maneno yalisemwa juzi.
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Waandishi wa Mtanzania na Mwananchi wana kesi ya uchochezi kisutu kuhusiana na maoni yaliyochapishwa na gazeti kuhusu mapolisi

  gazeti la mwanahalisi limefungiwa kisa kukaribia ukweli wa mwanamboka.

  mchungaji mtikila ana kesi mbili kuhusu maoni yake aliyotoa kuhusu kuendeshwa kwa nchi.

  Waandishi wanauwawa na serikali wanauwawa wakitafuta ukweli wa mambo.

  Serikali imepuuzia kabisa wajibu wake wa kikatiba wa kuwapa wananchi habari km watanzania hatuna fursa ya kujua kuna nini ndani ya mikataba ya madini, gesi nk.

  Wana maana gani kusema kuna freedom of the press?????????
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Kumbe waingereza ni "WAJINGA" namna,
  hii!!!!

  CCM kwa vituko, wameona wakiitolea hii single hapa tanzania wasingeuza hata nakala moja, wameizindulia YUKEIIII, wamempa mzungu mistari aisome kwa ajili yao.

  Huku wanaleta MA-NIUUZ, nakala zote kuuzwa kwa wawekezaji.

  "Would you let the system make you kill your brother?" by Bob marley & the wailors
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  We should emancipate ourselves from mental slavery - Bob Marley
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  At least M4C can trigger mental emancipation for now!
   
 15. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wazungu ni wanafiki sana ni watu wa maslahi tu leo wanausifia utawala wa Tanzania sababu wana maslahi nayo, halafu kuna watanzania wengine wanajidanganya kuishtaki serikali ya Tanzania kwa wazungu, kuna uzi humu watanzania wanajidanganya wanaitaji sahihi sijui ngapi waishitaki serikali ya Tanzania huku ni kujidanganya na kupoteza muda, wazungu hawapo kwa ajili ya kusaidia wanyonge wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
   
 16. S

  SUPERXAVERY Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi ya magwanda, ubongo mchache ni kukataa kila kitu, hata kama ni ukweli. Tusiwashangae na maoni yao.
   
 17. f

  follow me Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vigeugeu tu! na hii ndo sura ya mtu nafiki, haijifichi, juzi kati walinnang'a rais,leo tena apewa shavu! i hate white people from usa and uk
   
Loading...