Yamakagashi
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 8,615
- 17,607
Wakuu,
Niliwahi kujiuliza maswali mengi kuhusu Medard Kalemani-Mbunge wa jimbo la Chato na Naibu, Waziri nishati na Madini. Dr. Medard Kalemani kabla ya nafasi aliyonayo hivi sasa, alikuwa mwanasheria mkuu katika hiyo hiyo ya Nishati na Madini. Hii ina maana kwamba wakati wizara hiyo ikiongozwa na mawaziri kadhaa waliopita ( William Njeleja, Sospeter Muhongo) na ambao wametajwa kwenye ripoti mbili za makinikia pamoja na ripoti za Almasi na ile ya Tanzanite, huyu bwana alikuwa mshauri mkuu wa wizara katika masuala ya sheria. Kwa mantiki hiyo ameshiriki na kushauri mikataba yote ya madini ambayo imegundulika kuwa mibovu na haina maslahi ya taifa.
Sasa kinachoshangaza ni huyu baba kujifanya watu wanaomfahamu hawajui aliyoyafanya wakati akiwa mtumishi wa umma. Busara ndogo tu ingemshauri ajiuzulu kabla mambo hayajamfikia. Nadhani anafikiria Mkulu atamteua au kumpandisha cheo kuwa waziri kamili. Jambo analosahau ni kwamba mkulu anaona huyu baba atakuwa chanzo cha kusakamwa na balaa kila siku.
Kujiondoa serikalini kutamuongezea heshima zaidi kuliko kusubiri mpaka mambo yamfikie. Ajipime na aangalie kama bado anastahili kuwa kiongozi ndani ya serikali ya Magufuli.
Leo tumeona mpaka raisi anwaambia wakae kando watu waliotajwa kwenye ripoti ya almasi na Tanzanite.
Hivi hawa mawaziri hawajioni wenyewe kuwa wamepoteza sifa zo uongozi?
Watanzania tujifunze ustaarabu wa kujipima wenyewe.
Umesema anavizia cheo cha kuwa waziri kamili na kwamba akae pembeni kisa Magufuli kasema wakae kando walio tajwa kwenye ripoti
Sasa Magufuli kamteua kuwa waziri kamili ndio ujue anachokisema Magufuli na anacho kifanya ni vitu viwili tofauti
Juzi wafanyakazi watapandishiwa mishahara kesho yake sipandishi mishahara
Huyo ndiye Magufuli
Kalemani ni wa Chato hivyo kapewa shavu na ndugu yake
Wale wamalize awamu yao
Waje wengine kuendelea kula mpaka tutakapo kuwa na akili na maamuzi magumu