Mechi za Usiku Uwanja wa Mkapa mwanga ni mdogo

chamakh

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,024
1,261
Uwanja wa Benjamin Mkapa ndio uwanja Mkuu wa mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa ya Mchezo wa Soka kwa timu za Vilabu na Timu Ya Taifa Hapa Tanzania.

Kutokana na sababu mbalimbali, baadhi ya me hi zimekuwa zikichezwa nyakati za usiku. Hata hivyo ukiangalia hali ilivyo ya mwanga unaotolewa na taa zilizopo Uwanja wa Mkapa unaona kabisa zile taa zilzopo aidha ni chache au zimepungukiwa na uwezo wa kutoa mwanga wa kutosha ( luminosity).

Vile vile maeneo mengi ya Uwanja kama majukwaani hakuna mwanga wa kutosha na kufanya majukwaani kuwe na giza. Ukienda maeneo ya nyuma ya majukwaanna kwenye ngazi za kushuka hali ni mbaya zaidi. Kote huko ni giza tupu gali ambayo inaweza kuchochea vitendo vya Kihalifu ama hata ajali zisizo na msingi.

Ni vyema Wahusika wa Wizara ya Utamaduni na Michezo, Wahusija wa Menejimenti ya Uwanja pamoja na TFF kuangalia suala hili
 
Back
Top Bottom