Mechi ya Mwisho ya ligi kuu Tanzania ingekuwa Yanga Vs Simba

MashaJF

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
246
119
Natamani mechi ya mwisho ya ligi mwaka huu ingekuwa ya Yanga Vs Simba . Nadhani TFF nao wanamezea mate kupita maelezo ila ndio ishatoka hivyo.

Kwa wapenzi wa Simba iwapo Yanga itashinda bao 1-0 dhidi ya Toto Africa, Simba atatakiwa kushinda bao 4-0 dhidi ya Majimaji ili atwae ubingwa, na kama Yanga atashinda 2-0 Simba atatakiwa kushinda 5-0, na kama Yanga atashinda 3-0 basi Simba 6-0, mahesabu mengine endeleza mwenyewe mimi nimeisha rahisisha.
 
Mkuu una wazo zuri, ila mechi za watani wa jadi hata ktk ligi kuu za Ulaya hazichezwi kuwa za mwisho (kimazoea sio kikanuni)
Ila kwenye mechi za mtoano haijalishi
 
Na hata wangecheza (kwa wakati huu) nadhani Yanga inanafasi kubwa ya kuikandamiza Simba kwa sababu zifuatazo
Kwanza inaonyesha wachezaji wa Simba bado akili zao zinawazia walivyotolewa na TP Mazembe, na kama hilo ni kweli basi nawashangaa sana maana wanasumbuliwa na mawazo ya kutolewa na timu ambayo iliwazidi kila kitu ndani ya uwanja, na pengine wanajihisi kudhalilika baada ya kutolewa kana kwamba wametolewa na Lipuli ya Iringa.

Pili rekodi yao dhidi ya Yanga ktk ligi mwaka huu sio nzuri, hilo litawapa psychological boost wachezaji wa Yanga
Tatu mechi zao 3 za mwisho, kuanzia dhidi ya Kagera, TP Mazembe mpaka JKT zinaashiria wanashuka kiwango kwa kasi (japo si uthibitisho)
Nne, kwenye mechi watataka kuionyesha Yanga kwamba, kwa vile wamecheza mechi na Mabingwa wa Afrika mara mbili, na Mabingwa namba 2 wa Klabu Duniani, basi kiwango chao kimekuwa sana. Na hilo ndio litakuwa kosa kubwa zaidi kwenye soka endapo kweli watafanya hivyo
 
Back
Top Bottom