mechi ya Azam fc na Mtibwa kurudiwa

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
mpambano uliomalizika dakika tano kabla ya dk 90 kumalizika umeamliwa kurudiwa. mamuzi hayo yamefikiwa na kamati ya usuruhishi inayoongozwa na Alfred Tibaigana..
 
TFF bana,wana mambo,mambo yenyewe tena ya ajabu!

lakini hili lilikuwa wazi ama mechi irudiwe au mtibwa ashushwe daraja maana kama unasema refa alimaliza pambano kivyume cha sheria sasa kwanini upe timu nyingine..
 
Ukishashidwa kusimamia sheria na kanuni zilizokubalika zitumike kuongoza jambo fulani, kwa vyovyote vile jambo hilo halitakuwa na tija. Leodegar Chilla Tenga TFF imeisha mshinda; haya ni matokeo ya kushidwa kwake.
 
Tenga ni mtu ambaye tulimwamini sana kuliendeleza soka letu lakini imekua kinyume! Yaani uongozi wake naona ndo umepoteza muelekeo wa soka kabisa na hata rank yetu inazidi kushuka.
 
Mechi itapigwa ijumaa kati ya Azam na Mtibwa. Cha kujiuliza je mechi ya Azam na Kagera Sugar itapigwa lini? Au ligi itasogezwa Jumapili? Je, ikisogezwa jumapili nani atalipa gharama za timu kukaa hotelini? Maisha yamepanda sana je kuongezwa siku moja ni kuzipa timu husika mzigo usiobebeka.

TFF na Magumashi ya soka la bongo.
 
sheria za fifa timu ina takiwa ipumzike kuanzia siku mbili kwa hiyo inarudiwa ili azam fc ichoke halafu kagera ikiifunga yanga inarudi juu what a trick lakini tutashinda na nafasi ya pili ni yetu..

hala azam fc
 
Kwanza poleni lakini ninawasiwasi kuwa mnanunua mechi hata hiyo kamati ya ligi kuna namna haiwezekani refa afungiwe halafu nyie mpewe ushindi.....
 
Tenga ni mtu ambaye tulimwamini sana kuliendeleza soka letu lakini imekua kinyume! Yaani uongozi wake naona ndo umepoteza muelekeo wa soka kabisa na hata rank yetu inazidi kushuka.
Ni watendaji naweza kusema baada ya yule katibu mkuu kuondoka ndiyo madudu yameongezeka amalize muda wake aondoke....
 
mpambano uliomalizika dakika tano kabla ya dk 90 kumalizika umeamliwa kurudiwa. mamuzi hayo yamefikiwa na kamati ya usuruhishi inayoongozwa na Alfred Tibaigana..

TFF kama NEC vile wizi mtupu
 
Yes wafungwe mechi zote mbili si kwasababu nawachukia AZAM lakini hii tabia waliyoanzisha ya kununua mechi ndio inakela haiwezekani kila mechi watu wanalaumu tu.
 
Awali yalikuwa maamuzi ya hovyo kabisa! Kwa maamuz ya jana ni sahihi kwa mantiki kabisa! Vilevile Tenga anachofanya mie sikioni.... Kama makosa yamefanyika ndan ya kamati tena aliyo ichagua yeye hapo ninashaka na uongozi wake kabisa!
 
sheria za fifa timu ina takiwa ipumzike kuanzia siku mbili kwa hiyo inarudiwa ili azam fc ichoke halafu kagera ikiifunga yanga inarudi juu what a trick lakini tutashinda na nafasi ya pili ni yetu..

hala azam fc
Mkuu acha woga, pamoja na kunyang'anywa pointi tatu za mezani bado hata mkipoteza mechi zote mbili tayari mna pointi 53 ambazo hata kama Yanga watufunge sisi magoli mengi kiasi gani wataishia kuwa na pointi 52 tu, kwa hiyo hizo nafasi mbili za juu zimejaa kilichobaki ni nani awe wa kwanza na nani awe wa pili, Yanga waondoe kabisa kushika nafasi ya pili, wao kama wana nia ya kushiriki ya kimataifa wamwombea tu mnyama aungurume hadi hatua ya makundi tayari tutakuwa tushawakatia tiketi ya kushiriki mashindano ya shirikisho.
 
Yes wafungwe mechi zote mbili si kwasababu nawachukia AZAM lakini hii tabia waliyoanzisha ya kununua mechi ndio inakela haiwezekani kila mechi watu wanalaumu tu.
Una udhibitisho upi kuwa Azam wananunua mechi au ukisikia tu udaku tu basi unathibitisha?Tatizo soka la bongo maneno ni mengi sana,mechi zikiwa live watu kimya wakijua kwamba hatukuona mechi live utasikia habari kama hizi-za kuonewa,kubebwa,magoli ya offside...
 
tenga pumbafu sana...kutwa kushinda namnan sinza huna lolote na liupara lako
 
Hii sasa kali Azam watacheza Ijumaa na Jumamosi haiwezekani kabisa huu ni uonevu mkubwa, naona wanairahisishia Simba kupata ubingwa hata ikifungwa na Yanga. Hii maneno italeta mvurugano sana kwa michezo kitaifa, lazima kesi zitafunguliwa kwa ajili ya hili swala.
Mabingwa wa Kagame wao wapo wanayasubiri mashindano yao makubwa ya Kagame kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki na Kati.
 
Back
Top Bottom