Mechi Kali: Vodacom vs Tigo, mpaka sasa ubao unasoma 0 - 2

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,311
Hili pambano wa kuamua ni baba lao TTCL tu. Huyo ndio refa pekee atakayeamua hii mechi kali yenye mitifuano na rafu za hatari.

Ni muda mrefu wateja wa hii mitandao miwili pendwa tumewalalamikia sana kuhusu vifurushi vyao hasa vya internet (data). Ulimwengu wa sasa umebadilika, watu hawatumii maongezi sana kwa mawasiliano bali wanatumia data kwa ajili ya kuwasiliana kwa njia ya social networks. Lakini hii mitandao haikusikiliza kabisa.

Raia tukaona isiwe kesi, tukahamia kwa akina TTCL na Halotel. Kule wanajali wateja wao sana, vifurushi viko affordable na vinaisha kwa uhalali tofauti na hawa Vodacom na Tigo ambao data zinaisha kwa speed ya 8G.

Sasa January mwishoni Tigo wakaboresha vifurushi vyao, wakaanza kutoa dakika za mitandao yote pamoja na kuongeza wingi wa data kwa gharama za chini kidogo. Wengi tuliwakimbilia nikiwemo mimi, niliwahama Voda baada ya miaka kama 10 ya kuwa wateja wao.

Juzi Voda nao wakaja na maboresho ya vifurushi vyao hasa vya data ambapo wakaongeza viwango vya data ambavyo viko juu kuliko vya Tigo kwa gharama ileile. Mfano Tigo kwa mwezi walikuwa wanatoa GB 13 kwa shilingi 20,000/=. Voda wao wakaja na GB 20 kwa kiwango kilekile cha 20,000/=.

Sasa Tigo walipoona wamepigwa chenga ya mwili wakasema isiwe shida, kwani kupiga counter attack shilingi ngapi?. Leo asubuhi wakaamua kuja na mabadiliko mazuri zaidi kwa sisi clients wao. Mfano mwanzo walipoboresha walikuwa wanatoa GB 5 kwa 10,000/= kwa mwezi, sasa wameongeza mpaka GB 10 kwa 10,000/= ileile. Kwa 20,000/= sasa unapata GB 22 badala ya GB 13 za mwanzo.

Hii sasa ni vita rasmi kwani lengo hapa sio kuongeza vifurushi tu bali kuvutia wateja zaidi. Tunaomba huu mpambano uendelee maana inaleta ahueni kwetu sisi watumiaji baada ya kuteseka kwa muda mrefu.

Tunaomba Voda mfanye mabadiliko tena na tena maana hamna mlichokifanya. Vifurushi vya wiki na mwezi vya data mmetoa option moja moja tuu, wakati wenzenu Tigo wana a lot of options. Voda kifurushi chenu cha wiki kinaaanzia na 15,000/= wakati Tigo wanaanzia na 3,000/=. Voda kifirushi chenu cha mwezi kinaanzia na 20,000/= tena ndio hichohicho kimoja tu wakati wenzenu Tigo wanaanzia na 5,000/=. Mpaka hapo mmeshapigwa KO. Hata mimi siwarudii ng'oo.

Mbaya zaidi mlichojichanganya nasikia mumepunguza speed ya internet yenu, 4G yenu imekuwa kama 2G.

PS: Tunasubiri mabadiliko mapya ya TTCL baba lao ili tujue tunabaki na nyie ama tunahamisha makazi Tigo moja kwa moja. Kwa mabadiliko ya Voda na Tigo ni wazi TTCL mmepigwa gap kubwa sana kwenye unafuu wa vifurushi kwa sasa. Tunategemea mje na mabadiliko mara 3 yao. Yani TTCL tunategemea mje na GB 10 kwa shilingi 5,000/= au GB 5 kwa shilingi 2,000/=.
 
Vodacom wameniudhi sana. Wamepungiza bei ya vifurushi halafu wamepunguza kasi ya internet yao.

Nilijiuliza sana baada ya kuona hivi vifurushi vipya, nikajua tu hapa lazima kuna kitu kimekua compromised, sasa wamecompromise speed sababu ya price.

Wengine tuko vodacom kwa sababu ya kasi na ubora wa huduma zao, sasa vodacom wanafanya mambo ya hovyo. Hawana tofauti na tigo, airtel na halotel.

Hovyo kabisa.
 
Wamepindua meza
Screenshot_2020-02-15-07-43-14.jpeg




tapatalk_1581749822119.jpeg
tapatalk_1581749729015.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waendelee kupambana hukohuko mjini ila kwa Sisi tuliopo Katavi huku Wilaya ya Nsimbo maeneo ya Itenka na imilamate wakija huku wajue kuna raia anaitwa HALOTEL yeye bundle ni affordable na internet speed yake ni reliable,yaan ni speed utadhani nipo karibu na White House pale magogoni, wakija huku watapigwa za uso sana na hawatoamini.

tar 18 naenda mnadan itenka na kwa hisan ya Halotel huwa naweza kupiga WhatsApp video call jamaa zangu hujionea kinachoendelea mnadan!

Voda na tigo wenu hawana kitu kwass watu wa pori,Nilikuwa borisa/Kondoa yaan ni kama 10km kutoka kondoa mjini ila internet slow mnooooo,nilipoweka halotel ilikuwa burudani!
 
Mbaya zaidi mlichojichanganya nasikia mumepunguza speed ya internet yenu, 4G yenu imekuwa kama 2G.
NAdhani hi ni kweli kabisa, niliachana na voda miezi Zaidi ya 6 though line bado naitumia, nilikua natumia Zaidi ya sh 50k kwa mwezi for both airtime na vifurushi vya internet, nikahamia airtel but speed yao inaniboa sana, juzi na jana niliweka kiasi kidogo sana cha pesa ili nipate internet kwa voda but nilishangaa sana cause speed niliokutana nayo ilikua very slow tofauti na mwanzoni, jana hiyo hiyo usiku nimemrudia mpenzi wangu airtel. Halotel sijawahi kuijaribu wala hata kumiliki line yao
 
TTCL hawana cha kurekebisha upande wa bando, wenye laini za chuo watanielewa, wale jamaa ni cheap 70% sema tu internet yao haiko strong mbali na mjini baas.
 
Back
Top Bottom