Mechanism inayotumika kucontrol izi taa za kuongozea magari (traffic light)

Kuna diwani wa CUF hapa dar alijiuzulu cheo chake akahamia CCM,akasema moja kati ya vitu watu wa kata yake wanamkumbuka ni yeye kuweka UMEME/LUKU kwny taa za barabarani huko katani kwao kwa gharama zake na tangu amejiuzulu udiwani taa haziwaki tena sababu hakuna wa kuweka LUKU.

So point ya msingi hapa,baadhi yanatumia umeme wa LUKU.
 
Wabongo bhana, badala ya kutoa majibu na ufafanuzi, wadau mnakimbilia kusema nenda DIT mara hayo yanafundishwa DIT! Kwani ameulizwa hivyo vitu vinafundishwa wapi?
Kama mmeyasoma huko DIT na mkaelewa basi mfafanulieni la sivyo inadhihirisha mlisoma huko mkatoka kappa!
Ndio mainjijia wetu kaka,

Tuwavumiliee tuu
 
Mkuu unaonekana umekariri tu,

Hujamsaudia mleta mada
NAONA TULIOPITIA DIT TUNAVYO SASAMBULIWA HUMU........NAJARBU KUFUNYUA MAFAILI NIJE NA MUELEWESHO WA MAANA
1.CONTROL ENGINEERING
2.DIGITAL ELECTRONICS
3.ELEMENTS OF ELECTRONIC CIRCUIT..
 
Zamani kabla ya matumizi ya solar kuongezeka hizi taa zilikia zinatumia umeme wa tanesco sijajua kwa kipindi hiko kama kulikua na control room au laa, ila nyingi zinazofungwa kwa sasa hutumia solar energy na hakuna control room yoyote isipokua kuna small cabinet mita chache katika upande mmojawapo wa barabara hizo ambapo ndani yake kuna connection ya taa zote mfano junction ina pande 4 au 3 za barabara basi nyaya zote zinakua connected hapo na hizo nyaya hupitishwa chini kabisa ya barabara. Vilevile kuna kua na time interval ya kuruhusu magari kupita na hii inasetiwa kwenye hiyo cabinet. Kwa barabara inayokua na magari mengi yanayopita huwa inapewa sekunde nyingi kidogo kuliko yenzake. Wajenzi wa taa hizi kwa sasa hapa nchini ni TEMESA na hufanya hii kazi kwa barabara eidha za TANROADS au TARURA na ni nadra kwa sasa taa hizi kutumia umeme wa tanesco
 
NAONA TULIOPITIA DIT TUNAVYO SASAMBULIWA HUMU........NAJARBU KUFUNYUA MAFAILI NIJE NA MUELEWESHO WA MAANA
1.CONTROL ENGINEERING
2.DIGITAL ELECTRONICS
3.ELEMENTS OF ELECTRONIC CIRCUIT..

Unataka kutuchanganya tuu wewe.. ingia google lete tafsiri yake humu tukuelewe hayo mafaili yako baki nayo.
Lakini mkuu hivi si tumeambiwa eti mnacheza navyo sana kuanzia mwaka wa kwanza hapo DIT, mafaili utayapata kweli?
 
na vp kuhusu taa za pale bwawa la mtera darajani zile haiwezekani kuwa zinesetiwa kwa dakika nadhan lina sensor
Kama msemaji aliyepita hapo juu alivyosea mataa yana Intergrated Circuit (IC). Yanakuwa programmed while yanakuwa Installed. DIT kwa bongo wanatisha sana, ila kwa mataa ya barabarani ni Tanroads wakishirikiana na TEMESA........


Matarajio yako hayo mtoa mada kwa huku kwetu bado changamoto nadhani ni miundombinu mfumo huo unawezekana ni ku overcome short comings tu, na inawezekana. Ni technology ambayo inakwenda na wakati. Traffic Light Systems, fika idara ya mawasiliano angani pale DIT kwa uelewa zaidi.
 
1.Trafic Light karibia zote zilizopo Dar kwa sasa zinazalishwa na DIT 100% at Chip level.
2..Trafic light zina computerized system inazoziongoza
3.Zinatumia umeme wa Tanesco,solar na pia nyingi uwa na Backup system pale umeme unapokatika
4.Upo uwezakano wa kuzilink taa zote za barabarani za mji mzima kwenye control system moja.
5.Upo uwezekano kwa mfano taa zikawaka kijani toka mnazi mmoja mpaka airport kipawa kuruhusu msafara wa kiongozi n.k kama itafungwa centerized unit ya kuongoza hizi taa ,Ila kwa sasa akuna kitu kama hicho hapa Tanzania
Nafikiri nimesaidia kiasi
 
Dakika inawezekana, hata ya mjini ni dakika, ni calculation za zero and one, Logic and Gates.
 
Nachojua hizi taa hua zina control box yake hapo hapo karibu. Nakumbuka miaka ya 90s pale magomeni mapipa ilikua traffic akitaka kuongoza yeye magari badala ya taa basi anaenda kwenye hicho ki control box anasimama hapo na kuanza kubonyeza bonyeza.

Kilikua kiko upande/kona ya pale kanisani kutoka morroco kukunja kwenda kariakoo. Nadhan ule ulikua taratibu mzuri zaidi kuliko huu wa kusimama kati na kutumia mikono.
 
Unataka kutuchanganya tuu wewe.. ingia google lete tafsiri yake humu tukuelewe hayo mafaili yako baki nayo.
Lakini mkuu hivi si tumeambiwa eti mnacheza navyo sana kuanzia mwaka wa kwanza hapo DIT, mafaili utayapata kweli?
NTAYAPATA TU MKUU MBONA KABATI LANGU LINA PROJECT KM ZOTE NA KWENYE NINAYO NTAANZA KUYASHUSHA SOON
 
Mwanza wameadvance na kuwasaidia madereva kujua muda wa taa kuzima. Hii kitu ilipigiwa kelele sana na madereva wanaondesha nchi za wenzetu.
DSC_6745 (2).jpg
DSC_6745 (2).jpg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom