Mechanism for micro finance

Smarter

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
527
110
Salaam Wakuu,
Nafurahi kupata pahala kama hapa, ambamo tunapata Maarifa.

Niko kwenye initial stages za kufungua Microfinance, Nina mtaji wa wastani. Nataka ni -deal zaidi na wakopaji wadogo wadogo wanao hitaji (20,000 to 50,000) Naamini wapo wahitaji wa kuanzia kiwango hiki.

Nafikiri kutoa mikopo hio kwenye groups mfano watu 10 @ 20,000Tshs.

TafaDHALINI, mwenye experience naomba nisaidiwe Mechanism ya kuendesha shughuli hi.

Nawasilisha,
 
hii ni kazi ya consultancy mkuu, tangaza tenda tukuletee ma proposal, mimi ni mtaalam ila kama unahitaji huduma yang ulipie. kama upo tayari weka mawasiliano yako tufanye kazi.
 
Hii ni kazi ngumu kidogo,lakini naamini wewe utaiweza cha msingi ni kuzingatia baadhi ya vitu muhumu!!Tatizo kubwa katika mradi huu ni suala zima la dhamana(collateral security).Lakini kwa suala lako naona wewe unatarajia kutumia makundi,hii inaweza kukusaidia kutatua tatizo hili.Cha msingi kabla ya kuanza biashara hii ni kuzingatia kama wateja wako wanakopesheka,katika hili ni vema kuzingatia mambo yafuatayo:
-Biashara inayotarajiwa kufanya ni biashara halali na itamwezesha kurejesha fedha alizokopeshwa?
-Je mkopaji anauzoefu na biashara anayotaka kuikopea fedha?
-Je kuna mafunzo yoyote atakayohitaji kabla ya kukopeshwa?
-Je ana historia gani ya kukopa na kurejesha fedha?
-Je ana dhamana yoyote itakayochukuliwa endapo atashindwa kurejesha?
-Je hakuna uwezekano wa mkopoji kutumia fedha atakazokopeshwa kufanyia vitu vingine tofauti na malengo yaliyokusudiwa?

Nafikiri ukizingatia mambo haya unaweza kufikia malengo yako!lakini mimi nimezingatia zaidi matatizo waliyonayo wateja,na ninaamini kwa upande wako wewe hauna tatizo lolote.Lakini ni vizuri na wewe kujipima vizuri na kutatua matatizo yako kabla ya kuanza mradi huu.Nakutakia kila la kheri!cha msingi ni kuamini hakuna kitu kisichowezekana hapa duniani!!
 
TUKUTU,
Asante sana Mkuu, Analysis yako imekuwa somuch helpful kwangu,
Nitazingatia haya. Will get back after sometimes, tuone mchakato huu unaendaje and umefikia wapi.

Asante sana
 
Mechanism for micro finance inaeleweka zaidi naam tunahitaji wachangiaji zaidi ili tuweze kuelewa kwa wale wanaohitaji msaada wa elimu hii ,tafadhalini sana....
 
Hili ni wazo zuri sana hata Mimi nategemea kufanya ishu hiyo 2015 cha msingi Fanya utafiti kama location unayotaka kufungua ina mzunguko wa biaahara kwa kiasi Fulani,kuhusu dhamana kwenye mkopo kama huo Mara nyingi angalia asset ndogo kama vile pikipiki,vitu vya ndani,kiwanja nk,
 
Back
Top Bottom