Edokay
Member
- Mar 8, 2017
- 25
- 32
Habari za jmosi wana jf, mwaka 2015 nikiwa kwenye harakati za kutafuta ajira hapa na pale nilienda kutoa kopi stationary moja Dar es slaam maeneo ya Tegeta jina kapuni. Nilitoa vyeti form 4 mpk chuo kikuu, ghafla nikapigiwa simu nikatoka nje kuongea kwa sababu ndani hakukua na usikivu wa kutosha. Mara narudi ndani namkutua mhudumu huyo akiscan baadhi ya vyeti vyangu!!!! Kwa kweli nilihamaki na kumhoji kulikoni akasema natest tu coz photocopy machine inagoma! Sasa najiulza hapa isije kuwa aliscan na akatumia kwenye ajira na mm nije kutafutwa kwenye UTATA.