Mdudu ndani ya kichwa cha mbuzi kazi yake ni nini?

kitoromondo

Member
Mar 26, 2017
64
75
Wana JF,

Naomba kujua kwa wenye ufahamu,

Kuna mdudu hupatikana ndani ya kichwa cha mbuzi, mdudu huyu ni kama jongoo mdogo, nini kazi yake ndani ya kichwa cha mbuzi, huingiaje pale, na itakuaje endapo atakufa kabla ya mbuzi, nini kitampata mbuzi, naamini humu kuna

Wanaofahamu hili kwa undani naomba kuelimika juu ya hili.
 
Aisee nmetoka kufikilia juu ya nyakat zile tulokua tunadanganywa kondoo anamdudu kichwan km funza, eti akimtembea basi kondoo atakupiga kichwa unakufa hapo haopo....eti uyo mdodo anafanya kondoo anapambana na Radi ...kwamba mvua ikinyesha ,wee mtoe Kondoo nje basi atailinda nyumba dhidi ya Radii
 
Ila suala la radi na Kondoo kuna uhusiano
Mkusanyiko wa mifugo akiwemo kondoo hawadhuriki na radi kuhusu mdudu sijui
 
Wana Jf naomba kujua kwa wenye ufahamu, Kuna mdudu hupatikana ndani ya kichwa cha mbuzi, mdudu huyu ni kama jongoo mdogo, nini kazi yake ndani ya kichwa cha mbuzi, huingiaje pale, na itakuaje endapo atakufa kabla ya mbuzi,nini kitampata mbuzi, naamini humu kuna wanaofahamu hili kwa undani naomba kuelimika juu ya hili
umetumia neno mdudu vibaya...mdudu ni kitimoto mzee...nikajua tangazo mwezi huu wap wanapika mdudu fresh nikapige.
 
Aisee nmetoka kufikilia juu ya nyakat zile tulokua tunadanganywa kondoo anamdudu kichwan km funza, eti akimtembea basi kondoo atakupiga kichwa unakufa hapo haopo....eti uyo mdodo anafanya kondoo anapambana na Radi ...kwamba mvua ikinyesha ,wee mtoe Kondoo nje basi atailinda nyumba dhidi ya Radii
hahah kondoo mafia sana,kuna dogo mmoja wa kimasai alikua anachunga kondoo ,akakaa chini .alivyoanza kusinzia kwa kudonoa donoa,kondoo akajua uyu anataka kipigo ,alirudi nyuma alimkwida dogo kwa nguvu ,dogo alilazwa hospital mwenzi mzima
 
Ni kondoo siyo mbuzi, hii ni kweli ila mi mwenyewe sijui anakuwa sehemu gani mwilini mwa kondoo, kwa wale waliofuga kondoo hasa wale kondoo waliokomaa akipiga chafya pendelea kwenda kuangalia pale ulipoangukia uchafu wake ndipo utashuhudia ukweli wa huyo mdudu na anakuwa hai, ni kama kiwavi.
 
Mkuu,nina uhakika kumuona mdudu ndani ya kichwa cha mbuzi niliemchinja mimi siku ya pasaka, tukiwa tunakiaandaa kichwa kiwe chakula cha mbwa ndipo tulipomtoa mdudu ndani ya kichwa,ni sehemu jirani na ubongo, ngoja waje wanataaluma watujuze, ikiwa labda sio kwa kila mbuzi
 
Huwa ana rangi nyeupe
 
Basi itakuwa kwa wote mbuzi na kondoo mi nimeshuhudia kwa kondoo kwanza kabla ya hapo nilikuwa na taarifa ya uwepo wa hao wadudu kwenye kichwa cha kondoo nikaja kuamini siku amepiga chafya tukiwa jirani ndipo tukaona huyo kiwavi akitembea kutoka kwenye yale makamasi. Anafanya nini ama anaingiaje wataalamu ndo watusaidie wasikwepe kutupa majibu kama hawana taarifa tumewapa kazi ya kuongezea ujuzi wa tafiti zao
 
Back
Top Bottom