Mdudu kwenye mifupa anyanyasa maisha yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdudu kwenye mifupa anyanyasa maisha yangu

Discussion in 'JF Doctor' started by Vumilia matola, Aug 19, 2009.

 1. V

  Vumilia matola Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninatatizo la mifupa toka nikiwa mdogo hadi leo hii bado nateseka nimejaribu dawa nyingi bila mafanikio huwa unatokea uvimbe mikononi na mguuni baada ya kupasuka uvimbe huwa vinatoka vipande vya mifupa watalamu wanasema kuna mdudu ndani ya mifupa ndo anakula mifupa, naombeni ushauri nifanyeje?
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Ndugu Vumilia matola jaribu kuifuatilia hii dawa yangu ya kienyeji ikiwa hao Ma doctor wameshindwa kukutibu kuhusu hayo matatizo yako jaribu upate na kutwanga karafuu gramu 50 upate unga wake hiyo karafuu,Utwange Tangawizi kavu gramu 50 upate unga wake Utwange Pilipili Mtama gramu 50 upate unga wake hivyo vitu vyote uchanganye na chupa moja ya Siki ya Zabibu au kwa jina lingine Vinegar uwe unajipaka ile Sehemu yako inayovimba ndio yupo hapo huyo mdudu itaondoka ule uvimbe na kufa huyo mdudu lakini wakati unapokwisha kupakaaile dawa kwa kutumia mkono wako kisha kauoshe haraka huo mkono wako kwa sababu hiyo dawa inakuwa sumu usiile na inakuwa kwanza baridi kwa ile sehemu uliyopakaa kisha inakuwa na joto kali sana kiasi cha kuweza kumuuwa huyo mdudu ndani ya huo mfupa wako jaribu kutumia kwa muda wa siku kama kumi kisha utaniambia kama bado hayo matatizo yako unayo asante sana
   
 3. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Vumilia please call me through this number just now 0712234095
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180

  ...Afadhali msaidieni huyu mtu... naona tatizo lake kweli ni serious.

  Sijapata kukutana na hali ya hiyvyo.

  Pole sana Vumilia.
   
 5. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mtafute haraka tuwasiliane atapata ufumbuzi wa kudumu.
   
 6. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,384
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  pole sana kwa mateso unayoyapata vumilia,jaribu kufuata maelekezo ya mzizi mkavu,huenda yakasaidia,nakuomba usipuuzie.Tunakupenda sana mwana jf mwenzetu na Mungu atakuponya!!
   
 7. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mnaweza kuuelezea vizuri huu ugonjwa ukoje, dalili zake, n.k? Hii itasaidia pia kuweza kupata msaada ulio sahihi kwa tatizo hilo.
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Pole sana Vumi! ...very touched with your problem!
   
 9. V

  Vumilia matola Member

  #9
  Aug 20, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwakifupi: Nikwamba ugonjwa ulianza mwaka 1991 nikiwa darasa la kwanza, Mguu ulianza kuniuma wenyewe baada ya hapo nikapelekwa hospilalini nikalazwa ukawa umevimba mguu wote vikatoka vidonda viwili vilikuwa vinatoa usaa na vipande vya mifupa. Mwaka 1993 ukaanza mkono ukatokea uvimbe baada ya muda ukapasuka na usaa na mifupa mingi ikatoka hadi mkono umelemaa nashindwa kuunyosha saiz tatizo limerudi tena mguuni unaniuma sana nimetumia dawa nyingi sipati nafuu napata maumivu makali sana dawa za kutuliza maumivu saiz hazifanyi kazi
   
 10. D

  Discoverer Member

  #10
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vumilia!!! Pole sana kwa yanayokusibu kwa muda wote huo. Huo ugonjwa unaitwa osteomyelitis unatibika hospitali. Kama unaishi Dar nakushauri uende taasisi ya mifupa MOI utafanyiwa operation na utapona vizuri tuu.
   
 11. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa kwa kuwa umekusumbua kwa muda mrefu huo ugonjwa utakuwa chronic osteomyelitis.
  Wahi MOI faster.
   
 12. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa!!!! kwa kuwa umekusumbua kwa muda mrefu huo ugonjwa utakuwa chronic osteomyelitis.
  Wahi MOI faster.
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Pole sana Vumilia. Kwani madaktari wanasema dawa hakuna kwa ugonjwa huo?? Kama hakuna basi jaribu za kienyeji kama ambavyo wenzangu wataendela kukupa ushauri. Mdalasini na Asali ni dawa pia ya magonjwa mengi. Pia umejaribu kufanyiwa maombi kwa imani unayo amini??? Naamini sana watumishi wa Mungu wale ambao si matapeli, wale wenye upako wanaombea na maajabu yanatokea. Hebu jaribu tena huko kulingana na imani yako inavyokutuma na uchaguzi wa mtumishi ambaye unaona anafaa.

  Naamini pia Vumilia siyo jina lako halisi!!! Kama si halisi basi usipende kulitumia!!!! Majina mengine yana reflect hali halisi ya maisha ya baadaye, Imagine kumpa jina mtoto, Matatizo, Shida, Tabu, Vumilia, Maneno, Makelele, Mangumi, Makusaro, Tatizo, Vita, n.k!!! Majina mema yamebeba mema kwa watoto wako mf. Furaha, Sia, Zawadi, Rikiki, Baraka, Amani, Imani, Tumaini, Upendo, Pendo, Busara, etc. Hata kama umepitia mabonde na milima katika maisha yako, usimpe mtoto jina linaloambatana na mateso au ambalo lina maana isiyo njema katika jamii. Ni mawazo yangu tu wakuu.
   
 14. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Yanayomsibu mwenzetu yanasikitisha. Ila tumejifunza kwamba tiba ipo.
  Pole sana Vumi.
  Je, daktari anayekutibu ameshauri ufanye nini?
   
 15. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Maelezo zaidi ya huo ugonjwa unaweza kusoma hapa,
  Osteomyelitis


   
 16. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  I am very touched by this story, hope he/she finds treatment soon.

  SteveD.
   
 17. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Pole sana ndugu yetu. Jaribu kufuatilia ushauri uliopewa humu ndani, usisahau kumpigia Kimatire kwa namba aliyokupa.
   
 18. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  I have to confess, jukwaa la JF Doctor lilipoanzishwa mi niliona kama masihara. Sikuwa na picha kuona jukwaa hili litakuwa la msaada kama ilivyo sasa.

  Wakati tunapigania haki za waalimu, madaktari.... tuendelee kutumia jukwaa hili kusaidia wengine kwa yale tunayofahamu. Unaweza ukatoa information ndogo tu lakini ikampa mgonjwa matumaini yasiyo kifani. Nichukue fursa hii kuwashukuru wachangiaji wanaofungua hili jukwaa mara kwa mara.

  Shukrani ziwaendee pia JF owners na moderators.
   
 19. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Vumilia pole sana, nimeguswa na tatizo lako mpaka mwili umesisimka mana inaelekea huyo mdudu anakusumbua kweli kwa ulivyoelezea. Kama ulivyoshauriwa,nenda MOI haraka hata leo au kesho lazima watatibu watakusaidia.
  Zingatia kuwahi MOI na ugua pole ndugu!
   
 20. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Discoverer, many thanks kwa mwanga huo...lakini nifahamuvyo hizi hospital zetu kama sio mwenyeji sana au si mzoefu huwa kuna usumbufu sana. Vipi unaweza ukawa na uzoefu na pale au member yeyote akasaidia kutoa maelekezo ya ''logistics'' za MOI....ili huyu dada asiende akapigwa zengwe au kuzungushwa sana?

  Vumi kama sio mwenyeji au mzoefu wa MOI please let people know ili usaidiwe vizuri.....are you financially well equiped?
   
Loading...