Mdude hana sifa za uongozi, hafai kuwa mwenyekiti wa Bavicha, abaki kuwa mwanaharakati tu

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
Mimi namuona Mdude akiwa jela na kwa kuwa tabia ni kama ngozi simuoni mdude kubadilika kutoka katika hulka na haiba zake zile

Naiona Bavicha Kufanya uchaguzi wa marudio kama Mdude atakuwa Mwenyekiti wao maana kama Hata kuwa Jela sijui

Kumpatia Mdude Uenyekiti ni Risk kubwa kwa baraza la hawa vijana, nampima Kher James wapo katika utetezi wa hoja na mdude naona matusi kwa mdude... namuona kher anacheka tu maana. Haoni mjenga hoja anaona kapu la matusi

Nimeona vijana wa CHADEMA wanachukua form na kurudisha za Kugombea nafasi ya Uenyekiti wa baraza la vijana Chadema taifa (Bavicha)

Nimewaona wengi lakini nitawatolea maoni vijana wawili tu kati ya hao wengi

1. Mdude Nyagali maarufu kama Mdude Chadema (mwanaharaki na mwanachadema

2. Mwalimu John Pambalu (Diwani na mwanachadema na makamu mwenyekiti wa Bavicha Taifa)

Leo nitatoa maoni kwa huyu Mdude Nyagali na nitakuwa muwazi sana

Binafsi naona mambo makubwa mawili kwa Mdude kama atakuwa Mwenyekiti wa Bavicha lazima chama chake Kiwe kimejindaa kumuwekea mawakili wa kutosha maana ninamuona Mdude akiwa Jela ama korido za kisutu ama namuona Keko ama Butimba au gereza la Geita ama gereza kuu la Dodoma ama Mbeya au Iringa

Na kuna ujinga mwingi kwa vijana kujifaraji kipumbavu Eti kamanda ipo siku atatoka au huyu ndiye mwanaume

Kama vijana hatutawekeza kwenye hoja na haswa mdude wa twita akihamia pale Taifani basi naona fujo na sioni mipango kuhusu Vijana

Mdude ataishia jela na chama chake kitalaumiwa kwa kumsaidia kushirikiana na serikali kumuweka jela maana Chadema ili wamnusuru lazima asiwe Mwenyekiti

Mdude ni kijana jasiri sana katika eneo lisilo sahihi Mdude ni mpiganaji lakini anakosa maarifa ndiyo hayo mambo ya uropokaji na ujuaji usio maana mbaya zaidi wanaomshabikia wanamwambia wewe ndiye mwanaume na kwa hulka zake anadhani wanamwambia jambo la maana sana

Kama atakuwa Mwenyekiti wa Bavicha maana yake atakuwa amepewa jukwaa na chama chake la kusemea na kuonekana wazi

1. Zile tweet za kwamba Tumechagua Msukule ikulu yaani pale ikulu tuna msukule ( Rais) watanzania tulimpigia kura msukule atazirudia kuzisema ( tayari namuona jela wazi wazi

2. Tweet za kudharau Viongozi kwa lugha ya kuudhi mfano anasema Nyoka wa kibisa ananunua ndege anajenga madaraja anafanya siasa miaka minne mfululizo peke yako halafu anaogopa uchaguzi.Mzee nitakudharau mpaka naingia kaburini..

Najua atarudia haya kumuita mtu mwenye Serikali kuwa ni Nyoka wa kibisa yaani sisi tulichagua Nyoka la kibisa hapa namuona jela

Wapo wakina Heche,Katambi na Sosopi wamekuwepo hapo lakini hawa walikuwa ni mabingwa wa kuichamba serikali Lakini walichagua lugha maana wanajua leo wangekuwa jela

Kwa hulka na tabia za mdude Bavicha sioni kama inamuhitaji sana maana Bavicha inataka Vijana wa kusaidia baraza liwe lenye mikakati na siasa zenye tija na sio baraza lenye kushinda polisi na mahakamani kumtetea Mdude

Kwa hulka na tabia za serikali ya JPM siioni kama itavumilia kabisa Rais aje aitwe msukule sioni

Kwa tabia hulka na mienendo ya Mdude,lugha kukosa ustaarabu na kwa kuwa anaamini pale ikulu hakuna mtu anaweza kuwaambia vijana twendeni ikulu kwa maanadamano tukaidai ikulu.

Hapo ndipo kutakuwa na matokea makubwa Mawili damu kumwagika au roho kumwagika au vyote viwili kwa pamoja maana huo utakuwa uhaini

Sasa mdude abaki kuwa mwanaharakati hana uwezo wala sifa za kuongoza watu haswa vijana wasomi wenye akili na kuhoji bila mafanikio

Lakini kwa kuwa hata wajinga wanapiga kura basi tena maana wajinga wengi huwa wanaungana kumchagua mjinga mwenzao na kwa wingi wao hushinda kwa kishindo

Acha Demokrasia ifanye kazi lakini namuona Mdude Jela labda abadilike

Alloyce Nyanda
Mtozi
 
Vichaa wengi ni majasiri sana ila hawana akili na maarifa, the same to Mdude and the likes
 
Back
Top Bottom