Mdude Chadema ni uthibitisho kuwa kuwaweka ndani wapinzani, ni kuwakomaza na zaidi ni kuwaongezea "ari" ya mapambano

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Asubuhi ya leo, nilileta uzi hapa nikionya kuwa ukimfunga Mbowe, utafanya wapinzani waone hawana tena cha kupoteza kwa kufungwa au kuwekwa mahabusu.

Nilionya kuwa hatua ya kuwaweka ndani inawafanya kuwa majasiri zaidi.

Kabla jua halijazama, Mdude Chadema, aliekaa ndani kwa muda mrefu, jioni hii kaja na tweet yenye maneno tatanishi kumuhusu Mama chanzo kikiwa ni mahojiano aliyoyafanya jana.

Mdude ni kama hajaonja mahabusu na ni wazi hahofii kurudi mahabusu. Hivyo, kuwaweka ndani wapinzani, ni kuwajengea uwezo wa kupambana na si kuwafanya wawe waoga(warudi nyuma).

Nasisitiza, kadri mnavyoendelea kuwaweka ndani, ndvyo mnavyozidi kuwaimarisha, na mkuchukua hatua iliyobaki(siitaji), basi mtajimaliza wenyewe na sijui mtawashughulikia wangapi maana na wao ni wengi kama siafu.

Hii vita CCM mmeshashindwa, kilichobaki ni ku-surrender tu.

Mdude Chadema mmemtengeneza wenyewe, na mnawaongeza wengine kila kukicha.

Lingine msilolijua ni kuwa, wakati mnatumia muda mwingi na nguvu nyingi kupambana na CHADEMA,wenzenu wanawatoa kwenye reli(wako smart kuwazid) na 2025 watawananga majukwaani.

Mnaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Nope! Kinaonesha kwamba Magufuli hakuwa tatizo kama baadhi wanavyotaka kuiaminisha umma; ila wao wenyewe ndio chanzo na hakibi (cause & effect) cha masaibu yao.
 
Mdude ni wakumuonea hurum kichwa yake ina matatizo mtafutie madaktari mabingwa wa magonjwa ya akili wamsaidie.
 
nadhani hata kwa wakati huu mali za Mbowe zote zinapaswa zizuiliwe pomja na acount zake.
lazima sheria ya Ugaidi ifuatwe kikamilifu.

Nilishangaa sana alipo fikishwa nakaona Mbowe anaruhusiwa kukumbatiana na jamaa zake!
mahakamani lazima gaidi alindwe, nilishangaa pale kisutu inakuwaje Gaidi anapewa nafasi ya kukubatiana na watu mahakamani?!! hili halipaswi kujitokeza. ni muhimu vyombo vyetu vyote vikajifunza kutoka mataifa mengine namna ya kudili na watuhumiwa wa Ugaidi.

kamwe vyombo vyetu vya ulinzi na usalama visikubali kuhadaiwa au kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na mawakili au viongozi wa chadema, lazima sheria ifuatwe kikamilifu kama ilivyo kuwa inafuatwa kwa washitakiwa wengine.

nilishangaa kuwaona watuhumiwa wenzake wa Ugaidi wamefungwa pingu huku Mbowe akiwa hajafungwa pingu, sijafahamu kwa nn,!! kama hakuna ulazima basi wote wasifungwe pingu, sio baadhi wanafungwa wengine hawafungwi!!!
 
Mdude ana jiamini sana
Ukichunguza, utagundua wote sasa wanaanza kuwa tayari kwa lolote na inakuwa sawa na ile dhanya ya kifo cha wengi ni harusi.

Kadri unavyowaweka ndani wengi, walioko uraiani wanaona ni bora tu kwenda kuungana na wenzao kuliko kuwasiliti au kurudi nyuma.
 
Wewe mbona hujajitoa ili tupumue hapa JF
 
Asubuhi ya leo, nilileta uzi hapa nikionya kuwa ukimfunga Mbowe, utafanya wapinzani waone hawana tena cha kupoteza kwa kufungwa au kuwekwa mahabusu.

Nilionya kuwa hatua ya kuwaweka ndani inawafanya kuwa majasiri zaidi...
Mbowe Yuko wapi kwa sasa?
 
Tuendelee kupeana moyo huku wenye akili timamu wakifahamu kuwa viongozi wetu wa chama kitaifa, na wale wanaojifanya majasiri humu mitandaoni wanaogopa kuandamana kwa ajili ya kumpigania mwenyekiti.
 
Mdude ni wakumuonea hurum kichwa yake ina matatizo mtafutie madaktari mabingwa wa magonjwa ya akili wamsaidie.
Mwenyekiti alimpa unga auze, yey akawa anabwia mwenyew. Sasa madhara yake ndo kama tunavyoyaona!!!
 
Ukichunguza, utagundua wote sasa wanaanza kuwa tayari kwa lolote na inakuwa sawa na ile dhanya ya kifo cha wengi ni harusi.

Kadri unavyowaweka ndani wengi, walioko uraiani wanaona ni bora tu kwenda kuungana na wenzao kuliko kuwasiliti au kurudi nyuma.
Naona umeamua kujifariji😁
 
Asubuhi ya leo, nilileta uzi hapa nikionya kuwa ukimfunga Mbowe, utafanya wapinzani waone hawana tena cha kupoteza kwa kufungwa au kuwekwa mahabusu.

Nilionya kuwa hatua ya kuwaweka ndani inawafanya kuwa majasiri zaidi...
Hiyo twiti iko wapi au kelele tu?
 
Asubuhi ya leo, nilileta uzi hapa nikionya kuwa ukimfunga Mbowe, utafanya wapinzani waone hawana tena cha kupoteza kwa kufungwa au kuwekwa mahabusu.

Nilionya kuwa hatua ya kuwaweka ndani inawafanya kuwa majasiri zaidi...
Chadema mtaingia uchaguzini bila katiba mpya?

Maana siku hizi hatuli wala hatunywi maji kisa katiba mpya.

Zamani niliwaponda Kitila Mkumbo na Zitto kwa kuwaita wajivuni pale walivomwita "mwenyekiti" wao enzi hizo hana elimu ya kutosha kuongoza chadema. Leo nadhani nawaelewa.

Kinachoiangamiza Chadema ni kukosa maarifa. Basi.
 
Back
Top Bottom