Mdororo wa mawazo unaligharimu taifa(makala gazeti la dira) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdororo wa mawazo unaligharimu taifa(makala gazeti la dira)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMBOTA, May 8, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Na Nova Kambota

  Inaelezwa kuwa moja ya vitu ambavyo baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivipigania mpaka mauti yanamfika ni kujenga taifa la watu wenye uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo kwa hoja ndio maana wakati wa utawala wake alikuwa akienda chuo kikuu cha Dar es salaam kuchambua mambo na wasomi, Nyerere alikuwa ni mtu huru hata baada ya kuacha uongozi hakusita kukosoa pale alipoamini kuwa mambo hayakwenda sawa, hakupenda kuacha kufikiria.
  Lakini siku hizi kuna tatizo linaendelea kukua kwa kasi kila uchao hili si lingine bali ni mdororo wa mawazo kama ulivyo mdororo wa uchumi ambapo sekta za uchumi zinaboronga na uzalishaji kuanguka hivyohivyo mdororo wa mawazo unasababisha taifa kushindwa kuibua mawazo mapya.
  Taifa letu la Tanzania linaangamia siku baada ya siku kutokana na mdororo wa mawazo , viongozi hawana ubunifu, wanaishi kwa mazoea kuliko kusoma alama za nyakati hili ni tatizo kubwa wamefikia sehemu naona hawafikirii kabisa bila kupindisha maneno kazi ya kufikiri kwaajili yetu sasa inafanywa na Marekani na Ulaya.
  Huwa najiuliza iwapo kweli hawa viongozi wanafikiria kwanini tunadidimia siku baada Ya siku, kwanini tupo palepale? Kwa wanasaikolojia wengi ukweli ni kuwa mtu anayewaza mambo yaleyale kwa staili ileile tena kwa kiwango kilekile kisha anafanya vilevile basi hawezi kuendelea hata kidogo badala yake anabaki vilevile bilashaka sasa ndio tulipofikia kama taifa hatuna jipya hata tukiita jipya ujue ni boya au bomu linangoja kulipuka.
  Shule za kata ni ushahidi wa wazi kuwa jamii yetu imedorora kimawazo, hivi kuna haja gani ya kuwa na majengo bila madawati, walimu, vitabu na maabara? Kama jamii yetu inafikiria kuna haja gani ya kuwa na shule zinazozalisha sifuri? Huwa najihoji mara nyingi nashindwa kuamini kama kweli tunafikiria.
  Haiingii akilini nchi yenye madini ya kumwaga ina watu masikini wa kushindwa kumudu milo mitatu kwa siku halafu kweli nchi hii ina viongozi? Wanafikiria kwa usahihi kweli au bora liende? Madini kibao nenda hiyo mikoa yenye madini kama Shinyanga uone wananchi wanavyoteswa na umasikini wa kupindukia!
  Ajabu sana kuwa nchi hii ina mito , mabwawa, maziwa na maanguko kibao ya maji kama ya mto Rufiji lakini ipo gizani umeme hakuna, mikataba ya ubabaishaji kama Dowans na Richmond ndiyo tunaweza sio kumaliza tatizo la umeme, tutawezaje ilihali hatuwezi kufikiria? Tuna mdororo wa mawazo!
  Kuonyeha mdororo wa mawazo lilivyo janga la kitaifa kama UKIMWI sasa naona viongozi wa serikali wanapoteza muda mwingi kupambana CHADEMA kuliko kupambana na umasikini wa watanzania mpaka mama Maria Nyerere amewashangaa nasikia kawakumbusha waache malumbano yasiyo na tija badala yake watumikie wananchi.
  Kuibuka kwa Babu wa Loliondo na dawa yake ya kikombe , wagonjwa wanakimbia mahospitalini tena wengine kwa kungÂ’oa drip wanaenda Loliondo kupata kikombe serikali haishtushwi na hili mpaka Babu Mwasapile anasema kuwa pale kwake sio hospitali ya Rufaa, hii ina maana gani? Kuwa hospitali za serikali hovyo kabisa, sio za kawaida wala za rufaa mpaka wagonjwa wanadhani babu ni hospitali bora ya rufaa kuliko za wizara ya afya, hii ajabu sana!
  Mimi nilitegemea mpaka sasa hivi waziri wa afya awe kishajiuzulu au amesitisha kupokea mshahara lakini wapi bwana! Loliondo bora kushinda Muhimbili lakini kwake yeye ni sawa tu, siyo yeye orodha ni ndefu tu angalia watoto wa kidato cha nne walivyopata sifuri kibao lakini waziri wa elimu hatuoni kama atawajibika hata kidogo bilashaka atasoma bajeti ya wizara yake bungeni bila aibu huku watoto wakiendelea kusota kwenye shule za kata, hapa tusemaje basi? Huu kama sio mdororo wa mawazo wa jamii yetu ni nini?
  Hata huko Ulaya na Marekani maendeleo hayajaja kwa kubweteka tu na kusubiri watu wengine wawasaidie kufikiri bali wenyewe walipambana na changamoto na viongozi wao wakajitoa kwa hali na mali kuwatumikia wananchi sisi tumeamua kugawa maliasili zetu kwa kigezo cha ubinafsishaji wananchi wanaporwa ardhi halafu nasikia mke wa mkubwa fulani alikuwa huko Lindi na Mtwara kwenye ziara zake akawaasa wananchi wasiuze ardhi kiholela huu sasa kama sio undumilakuwili nini? Nasema hivi acha wao waongeze hao wapora ardhi wanaowaita wawekezaji ila niwape angalizo kuwa ardhi haiongezeki.Tafakari!

  Nova Kambota ni mwandishi kijana wa Makala , ni mchambuzi na mtafiti wa maswala ya kisiasa pia ni mwanaharakati wa vijana anapatikana kwa anwani ya barua pepe; novakambota@gmail.com au tembelea blog yake ; Nova Tzdream
  Au mpigie kwa namba 0717-709618 au 0766-730256.

   
Loading...