Serikali: Kampeni ya kupambana na Ushoga ya RC Makonda sio msimamo wa nchi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Wizara ya Mambo ya Nje imesema kampeni iliyoanzishwa na RC Paul Makonda kukabiliana na ushoga ni mawazo yake binafsi na si msimamo wa Serikali

2EB6A534-4FFF-492E-B8EF-F488A6D1420F.jpeg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inapenda kuwajulisha wananchi na jumuiya ya kimataifa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kuhusu masuala ya ushoga yaliyoongelewa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni.

Katika mkutano wake na vyombo vya habari, Mhe. Mkuu wa Mkoa alitangaza kampeni ya kukabiliana na vitendo vya ushoga katika jiji la Dar es Salaam.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa kufafanua kwamba, hayo ni mawazo yake na sio msimamo wa Serikali.

Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa kutumia nafasi hii kukumbusha na kusisitiza kwamba, itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa inayohusu haki za binadamu ambayo imesaini na kuridhia.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na itaendelea kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
04 Novemba, 2018
 
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki umefafanua kuwa kampeni iliyotangazwa na RC wa Dar ya kupambana na vitendo vya ushoga ni mawazo yake sio msimamo wa Serikali

IMG_20181104_174549-1.jpeg
IMG_20181104_174555-1.jpeg
 
Msiba huu!

Wazungu walishatupiga pini kitambo sana.. Mikataba hii inabidi iwe reviewed kama kweli tuko serious na tunahitaji kujiamulia mambo yetu wenyewe..

Haiwezekani sheria zetu zikataze sodomy na homosexuality, halafu tuifuate mikataba ya kimataifa inayosema tofauti.. Hata issue ya uzazi wa mpango ipo kwenye mikataba lakini Rais alitoa ya moyoni kwamba hakubaliani nayo.

We need to review some agreements with the international community!
 
Wizara ya Mambo ya Nje imesema kampeni iliyoanzishwa na RC Paul Makonda kukabiliana na ushoga ni mawazo yake binafsi na si msimamo wa Serikali
Ndo wameanza kuona impact yake kimataifa, wazee wakukurupuka serikali iendeshwi kimhemko......hilo swala la ushoga nikumbwa zaidi ya poor Makonda next time mwemnajifuza, mna tuaibisha nje ya nchi.
 
1541343252642.png

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inapenda kuwajulisha wananchi na jumuiya ya kimataifa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kuhusu masuala ya ushoga yaliyoongelewa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni.
Katika mkutano wake na vyombo vya habari, Mhe. Mkuu wa Mkoa alitangaza kampeni ya kukabiliana na vitendo vya ushoga katika jiji la Dar es Salaam.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa kufafanua kwamba, hayo ni mawazo yake na sio msimamo wa Serikali.
Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa kutumia nafasi hii kukumbusha na kusisitiza kwamba, itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa inayohusu haki za binadamu ambayo imesaini na kuridhia.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na itaendelea kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
04 Novemba, 2018

Chanzo cha taarifa: Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation
 
Nahisi ndiyo maana kosa la James ni kusambaza maudhui ya ngono na siyo kuwa homosexual.

Anyway, hatimaye njaa haimpendezi mtu. Shangazi kashinda kwa kuwa wa kwanza kuonyesha msimamo ( though in a wrong way).

Na Makonda anaendeleza rekodi ya kutofanikisha kampeni yake yeyote.
 
Wizara ya Mambo ya Nje imesema kampeni iliyoanzishwa na RC Paul Makonda kukabiliana na ushoga ni mawazo yake binafsi na si msimamo wa Serikali

Hawa Wanasiasa na Watawala wetu ifikie mahali waache KUTAWALA KIUJANJA UJANJA....Waziri Mahiga aache usanii,,,maana la Balozi wa EU kaongea kinafiki na hili la Ushoga anataka kutuingiza chaka. Kama kweli ati HAYO NI MAWAZO BINAFSI YA MAKONDA....NINI BASI MSIMAMO WA SERIKALI YA MAGUFULI??

Kinachoonekana hapa ni MAKONDA KUTUMIWA NA UTAWALA(RAIS) KWA MAELEKEZO TOKA JUU. Haiwezekani mtu ajitungie SERA(Policy) au SHERIA(Law) kutoka kichwani mwake zinazopingana na SHERIA MAMA(Katiba)halafu Serikali inyamaze tu lakini watu wakihoji Kiongozi mmoja bazazi anajitokeza na kusema huo sio msimamo wa Serikali....!!Kumbe msimamo wa Serikali ni nini...!!!

Magufuli na Makonda ndio wanaohangaisha watu katika nchi hii na kuyumbisha mahusiano ya Kidiplomasia na Mataifa mengine. Ifike mahali waache kutawala nchi hi kama familia za nyumbani mwao!!
 
Back
Top Bottom