Mdomo wa juu kuvimba inaweza kuwa ugonjwa gani, chanzo na tiba yake ni nini?

Okwaaa

JF-Expert Member
Dec 3, 2020
1,316
2,917
Habari za asubuhi wakuu?

Nianze hivi,

Jana nilitoka Mbeya kuja huku Sumbawanga hadi Nkasi, kiukweli safari ilikuwa na changamoto ya nauli nilivutana sana na makonda hadi kudiliki kunitoa nje ya gari si mchezo, kwahiyo nilichelewa kidogo kufika huku Rukwa wilaya ya Nkasi, nikifika kwenye saa nne kasoro usiku.

Baada ya kufika nikaamua nijifukize kwanza ndipo nikaoge nilale maana huwezi jua usalama ulikuwaje wakati nasafiri, kwa hiyo nikafanya kwa tahadhari tu. Na nilijifukiza kwa maji tu bila mchanganyiko wowote.

Sasa leo asubuhi naamka nimekuta mdomo lips ya juu umevimba sanaaaa, utadhani nimepigwa na ngumi ya adabu na hauumi, yani ata nje naogopa kutoka, watu wanaweza kuhisi nilipigana sehemu nikapigwa konde zito au nyuki kaning'ata.

Na hii hali iliwahi nitokea miaka mitatu iliyopita tena lips ya juu ya mdomo ndiyo huwa inavimba.

Sasa wakuu hii inaweza kuwa nini? Na inaashiria nini?

Wajuzi nisaidieni maana nawaza sanaaa.
 
Picha kakaa.
tatizo uligomban na makonda huko sumbawanga sio mchezo
Picha tena. Si mtabaki mnacheka tu ulivyovimba! Alafu sijui kuambatanisha picha kwenye bandiko lolote humu jf nikijaribu huwa nashindwa labda kwa sababy natumia jf ya free basic kwa sababu sina hela ya bundle
 
Hiyo ni Allergies wengine huvimba macho ila yanakua hayaumi kama unavosema.
Asante mkuu nimekuelewa hapa. Sasa cjui itakuwa ni allergy ya kitu gani ili niepukane nacho siku nyingine nisije kuvimba. Na sikumbuki historia ya nyuma mara ya kwanza nilipovimba kama nilifanya vitu gan kabla ya kuvimba ili nifanananishe na nilichokifanya jana yote kabla cjavimba.

Asante mkuu umenipa mwanga wa pakuanzia🙏
 
Asante mkuu nimekuelewa hapa. Sasa cjui itakuwa ni allergy ya kitu gani ili niepukane nacho siku nyingine nisije kuvimba. Na sikumbuki historia ya nyuma mara ya kwanza nilipovimba kama nilifanya vitu gan kabla ya kuvimba ili nifanananishe na nilichokifanya jana yote kabla cjavimba.

Asante mkuu umenipa mwanga wa pakuanzia
Hapo ndio inabidi uchunguze movement zako za hiyo jana. Kuna wengine mfano mahindi yanavochanua zile Pollen zinawaletea allerg wengine aina ya vyakula, matunda wengine baadhi ya miti inapochipua huwaletea allerg sasa siwezi kujua wewe kilikupata nini exactly.
 
Asante mkuu acha nitafti nini kinaweza kuwa shida🙏
 
Mkuu Mungu anakuona, ujue sijaongea na mtu yeyote tangia nimeamka, sasa ulivosema niseme pipos ndo nimejaribu nikituko mluzi wenyewe umegoma kutoka, unazibwa pakutokea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom