Mdomo umeenda pembeni, anayejua dawa anisaidie

Utapata Vascular cerebral accident,lazima kuna shida kwenye mishipa ya brain inayoncontrol mdomo.Sasa ubongo ukizidi kukosa oxygen utajikuta unapata Hemiplegia.Nenda hospital haraka.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yaani ni week ya pili sasa mdomo umeenda pembeni. Nimetumia dawa bado kwa sijapona. Anaejua dawa pls anijuze.

Sent using Jamii Forums mobile app
kama miguu na mikono haijapat athari basi hiyo sio stroke....ni ugonjwa unaosababishwa na infections kwenye nerves...ni kwamba unatibika kwa dawa za hospitali...ni hiyo hali ya kupinda kwa mdomo itarudi pole pole ndani ya mwezi mmoja hadi mitatu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, ugonjwa wako unatibika lakini uwahi hospitali sio kwa waganga wa kienyeji.

Unaweza kutibika kati ya mwezi mmoja hadi mwaka, kama huna matatizo mengine. Hujasema ulianza lini kuugua.

Una ugonjwa unaoitwa Bell's Palsy. Utapewa dawa (corticosteroids) na lazima wakukande uso (physiotherapy).

Ukichelewa matibabu, mishipa ya uso (cranial nerve VII) itachelewa kurudi katika hali yake ya kawaida au kutorudi kwa muda mrefu zaidi.
 
hakuna cha pressure wala stroke wewe umepigwa jujumeni na wanga na dawa yake ni ndogo

tafuta nyanya pori zitwange kanda mdomo wiki moj unarudi mahala pake
 
Kuna dalili gani zilimtokea kabla ya kupinda mdomo
Je ,kichwa kinauma
hama anasikia ganzi
Macho yanauma
Mdomo kucheza cheza
Kutopata usingizi

au kuna tukio lolote umelifanya hapo uswazi kwenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Mkuu. Nenda hospital labda wanaweza kukusaidia, pia jaribu kutumia mafuta ya nazi mara mbili au hata tatu kwa siku kuumassage mdomo ili kujaribu kuurudisha upande ule unaostahili.

Yaani ni week ya pili sasa mdomo umeenda pembeni. Nimetumia dawa bado kwa sijapona. Anaejua dawa pls anijuze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu nami nilikuwa na tatizo Kam
a hill, niliangaika sana na atimaye nilipata ufumbuzi, Kwa faida yako nifuate "INBOX" Nitakusaidia bure bila shaka Mungu atakuponya, Vinginevyo utatumia gharama kubwa bila ya mafanikio.
acha roho mbaya weka ujuzi huo bayana kila mtu aijue tiba,asa inbox ili iweje?
dawa yake ni avae kandambili mkononi harafu asukume shavu la upande ulioenda upande,baada ya siku mbili aje atupe mrejesho,i`ve seen people turn into normal ingawa huwa nilishindwa kujua mechanism how does that works,but amini nikwambiacho mkuu!
pole sana muathirika kwa tatizo though!
 
Back
Top Bottom