Mdomo huumba, ongea mazuri kuhusu mahusiano yako

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
52,470
70,590
Habari za muda huu wanabodi, leo ningependa tujadili mada hii...

Ni mambo ambayo yanatokea kila siku kwenye mahusiano..Karibuni

Ongea mambo mema kuhusu ndoa au mahusiano yako. Wahenga wanasema mdomo huumba, wakimaanisha kuwa kitu ukikisema mara nyingi basi hutokea kuwa kweli. Ndivyo maisha yalivyo yale unayoyaongea ndiyo unayoyahisi na ndiyo yanayotokea.

Ukiangalia watu wengi ambao kila siku hulalamika kuhusu mahusiano yao ndiyo walewale amabao kila siku utasikia wamepigwa, wamesalitiwa na mambo mengine mengi mabaya mabaya huwatokea wao tu. Hili halitokei kwa bahati mbaya, hutokea kwakuwa unapoongea mambo mabaya unatangeneza sumu katika mwili wako.

Huishii kuongea tu bali unajenga chuki na ile chuki inapokaa ndani sana hutokea na kujikuta unamchukia mwenza wako, ukimchukia akajua unamchukia basi nirahisi kukusaliti na wewe pia nirahisi kumsaliti na hapo ndipo kasheshe huanza.

Nikweli yanakutokea mabaya mengi lakini naamini pia kuna zuri hata moja katika mahusiano yenu, hembu unapokuwa na rafiki zako wakati wakiongea kuhusu furaha usiharibu na kuanza kuongelea machungu yako, anza kuongelea zuri hata kama ni moja tu.


Unapokuwa na mume au mke wako hembu acha kuwa mtu wa kulalamika na kulialia tu, shukuru kwa hata zuri moja alilokufanyia na sifia hilohilo moja zuri hapa sio tu kwamba utamuonyesha unashukurani na unajali lakini pia utamuonyesha kuwa umefurahi na kumsukuma kufanya zuri jingine.

Hawezi kukufanyia mazuri kama kila anapojitahidi wewe ni kulalamika, yaani unakuwa kama una kakaratasi ka mabaya ambako mkikorofishana kidogo tu wewe unakachukua na kunza kukasoma. kwakufanya hivyo mbali ya kumkatisha tamaa lakini pia utamfanya asione umuhimu wa kufanya mazuri tena.

Usione wanaosifia wenza wao kila siku ukadhani kuwa wanafanyiwa mazuri tu, yapo mabaya mengi na changamoto nyingi, lakini wanaamua kujikita katika mazuri kwani wanafahamu huwezi kuwa na furaha kwa kuwaza matatizo. Furaha inatokana na mambo mazuri tunayoyafanya na kuyawaza.


Credits: http://www.mahusianomagazine.com
 
Ni kweli Mutabari. Wengi huongea mabaya as if walilazimishwa kuingia kwenye hayo mahusiano. Wasisahau Kuwa unapoongelea vibaya hayo mahusiano you only prove how stupid you are on relationship.
 
Sio kuongea tu, bali pia kuwaza mazuri,
Unapokuwa na negative nyingi za mahusiano yako kwenye mawazo yako mwisho wa siku yanakuja kuwa kweli, utajishangaa unafanya maamuzi ya ajabu na sababu ni kuwa ulishakuwa na maswali na majibu kwenye mawazo yako
 
Sio kuongea tu, bali pia kuwaza mazuri,
Unapokuwa na negative nyingi za mahusiano yako kwenye mawazo yako mwisho wa siku yanakuja kuwa kweli, utajishangaa unafanya maamuzi ya ajabu na sababu ni kuwa ulishakuwa na maswali na majibu kwenye mawazo yako
kumbe ndivyo ilivyo ee
 
Mimi mambo ya ushilawadu sio yangu, hakuna hata rafiki yangu mmoja anaejua mambo yangu na mpenzi wangu. Kwasababu ni siri yetu kama jema au baya, nilijifunza miaka ya nyuma nilipokuwa nikiwaambia mambo yangu rafiki zangu.
KIKULACHO KINGUONI MWAKO.



Ndukiiiii
 
Ni kweli kabisa... Uliwazalo ndiyo hilo hilo litakalo kutokea.. Ukiawaza mabaya utavuna ubaya... Ukiwaza mazuri utavuna mema...

Ukisema naweza utafanikiwa kweli, ukisema siwezi utashindwa kweli..

mahondaw wangu mara zote namuwazia mazuri tu, namsemea mazuri mbele za watu, yale madhaifu yake yote tunarekebishana kimya kimya lakini hayawi gumzo...
 
Ni kweli kabisa... Uliwazalo ndiyo hilo hilo litakalo kutokea.. Ukiawaza mabaya utavuna ubaya... Ukiwaza mazuri utavuna mema...

Ukisema naweza utafanikiwa kweli, ukisema siwezi utashindwa kweli..

@mahondwa wangu mara zote namuwazia mazuri tu, namsemea mazuri mbele za watu, yale madhaifu yake yote tunarekebishana kimya kimya lakini hayawi gumzo...


Asante sana Smart911
Nami nakuwazia na kukuombea yaliyo mema Smart911 wangu
Mungu akubariki sana Smart911
 
Back
Top Bottom