mdokozi...

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
...nilipokuwa 'kijijini' nilihadithiwa visa vingi vya kusikitisha, kimojawapo ni hiki;

...utaishije ishije au kumvumilia mke/mume 'kibaka'?... yaani, ukishtuka yeye tayari keshapunguza salio kwenye account zako kwakuwa tu anaijua pin number na wapi unaweka ATM cards zako,...

au,

...kufumba na kufumbua vidani, hereni na pete za mke zilizokuwa kwenye dressing table 'zinapotezwa' katika mazingira ya kutatanisha. Ukimuuliza mtu kama huyo anakuwa mkaaali, eti unamdhania yeye mwizi akuibie ili iweje!

Kama si yeye nani mwingine sasa?

...Kwa mtizamo wenu, hatua gani makhsusi zinazofaa kuchukuliwa na wenye matatizo ya ndoa aina hii, ukizingatia vitu hivyo 'vinapotezwa' ilhali wenye access ya vitu hivyo ni wenza tu?
 
Mbona hadithi yako haiendani na mazingira ya kijijini? Maana umedai ulihadithiwa hadithi hiyo ulipokuwa kijijini, lakini vijijini hakuna ATMs na sidhani kama wanawake wa vijijini wana uwezo wakuwa na dressing tables!
 
amesema "kijijini" na sio kijijini, labda atatueleza zaidi maana yake akirudi..
 
akiiba kwenye ATM change pasword bila kumfahamisha nk

shida inakuwaga pale ambapo spouse ni mwizi aka jambazi, mkewe anaona vitu vya gharama kuliko uwezo wao vinaletwa ndani, mumewe ananunua viwanja na kujenga nyumba zinazoisha chap chap kama magician vile..akimuuliza anasema ati amepata bonge la "dili" halafu baada ya hapo hakuna maelezo zaidi...kuna dada mmoja aliyekuwa kwenye hiyo situation aliniuliza swali kama amripoti mumewe aka baba watoto wake polisi au auchune tu
 
Mbona hadithi yako haiendani na mazingira ya kijijini? Maana umedai ulihadithiwa hadithi hiyo ulipokuwa kijijini, lakini vijijini hakuna ATMs na sidhani kama wanawake wa vijijini wana uwezo wakuwa na dressing tables!

Serendipity...Uko sahihi kabisa..Its so pity na ni jambo la ajabu sana huyu Mbu anaongelea mambo ya vidani na ATM CARDS vijijini!..Nam'refer asome thread yangu isemayo " Umeishi Kijijini?";, aone uhalisia wa maisha na kinachojiri vijijini...This is too much a FICTION...!hUYU bWANA KUNA WAKATI ALIKUWA NA SIGNATURE ILIYOPATA KUNIFURAHISHA SANA nikiwa ndo naingia jeiefu..Ilikuwa inasema ..."Wanatumia neti kuvua samaki, hawawezi kulala kwenye neti, huku wana njaa" .....Hakika yalikuwa ni maneno yaliyokuwa yananipa hamasa sana na kunikumbusha maisha ya kweli ya vijijini!..Anyway, namsubiri aje atetee hoja hapa!..Mungu ibariki TANZANIA.
 
.....hahahahahahaha!:D:D
lakini amesema ''hadithi''
 
hili hataweza kujitetea mkuu!AMECHEMKA!
halafu ni modereta huyu!lol:D
 
akiiba kwenye ATM change pasword bila kumfahamisha nk

shida inakuwaga pale ambapo spouse ni mwizi aka jambazi, mkewe anaona vitu vya gharama kuliko uwezo wao vinaletwa ndani, mumewe ananunua viwanja na kujenga nyumba zinazoisha chap chap kama magician vile..akimuuliza anasema ati amepata bonge la "dili" halafu baada ya hapo hakuna maelezo zaidi...kuna dada mmoja aliyekuwa kwenye hiyo situation aliniuliza swali kama amripoti mumewe aka baba watoto wake polisi au auchune tu
...ukamshauri nini??
 
Naachana na Mbu kwakuwa hajaeleweka bado na hajajikosoa pia.Ni vyema nichangie kuhusu huyu dada kwa kuwa naona ni nzuri kuchangia.situation kama hiyo ni ngumu na inahitaji maamuzi magumu katika wakati sahihi.Kuna mambo mawili hapa ya kuzingatia.
  1. Maisha yanavyotakiwa kuwa na
  2. Maisha jinsi yalivyo
kwa ushauri wangu mi naonelea huyu dada atambae na namba mbili hapo,kwa maisha jinsi yalivyo achune apange mipango yake mingine ya kujiweka sawa halafu atambae ikibidi,hana budi kufanya hivyo maana panapodharula lisilobudi hutendwa.kumtosa polisi wakati bado yupo katika ndoa si vyema kutamsusuwika katika maisha yake,atoke kwanza then amtose polisi
 
Kama anaiba ina maana haikuija ghafla, ulijua tangu mwanzo ukakaa kimya. Huyo anahitaji maombi ya kiukweli, kuna tabia nyingine ni embarassment huwezi vumilia. Huwezi mpeleka mwenza wako police afungwe, ufanyeje, shirikisha mapastor wenu ili wamuombee atapona tu.
 
Mi naona kama vile mwenzetu hajajielewa,
au nahisi labda kachanganya mafaili
Labda ndio MABWEKA ya kufungia mwaka.
 
...daaah, mbona wakali hivyo? kwani kijijini kuna sifa gani mbaya mbaya kiasi kwamba dressing table na ATM zikosekane?

Kama mmezoea kijijini kutokuwa na umeme, maji, barabara za lami nk kuna tofauti gani na mimi niliyekuwa Dar es salaam kwenye shida hizo? Kwani kuishi kijijini kuna ugumu gani kwenda masafa kadhaa, au hata kupanda daladala kwenda kwenye ATM, au nyie wenzangu ukifungua dirisha tu unaionaATM ileeee?

...Dar es salaam eneo kubwa ni "vijiji" tu, mtake msitake.
Nimeleweka au tufungue thread uwanja wa Siasa? :D
 
Naachana na Mbu kwakuwa hajaeleweka bado na hajajikosoa pia.Ni vyema nichangie kuhusu huyu dada kwa kuwa naona ni nzuri kuchangia.situation kama hiyo ni ngumu na inahitaji maamuzi magumu katika wakati sahihi.Kuna mambo mawili hapa ya kuzingatia.
  1. Maisha yanavyotakiwa kuwa na
  2. Maisha jinsi yalivyo
kwa ushauri wangu mi naonelea huyu dada atambae na namba mbili hapo,kwa maisha jinsi yalivyo achune apange mipango yake mingine ya kujiweka sawa halafu atambae ikibidi,hana budi kufanya hivyo maana panapodharula lisilobudi hutendwa.kumtosa polisi wakati bado yupo katika ndoa si vyema kutamsusuwika katika maisha yake,atoke kwanza then amtose polisi

Kama anaiba ina maana haikuija ghafla, ulijua tangu mwanzo ukakaa kimya. Huyo anahitaji maombi ya kiukweli, kuna tabia nyingine ni embarassment huwezi vumilia. Huwezi mpeleka mwenza wako police afungwe, ufanyeje, shirikisha mapastor wenu ili wamuombee atapona tu.

...hivi ni halali kweli kuishi maisha ya ndoa halafu mkeo.mumeo asijue PIN ya account zako benki kweli? incase unapatwa na dharura itakuwaje? anyway...

Hiyo case ya mwanadada kuchukuliwa vito vyake vya dhahabu bado halijapatiwa ufumbuzi...yataka moyo kusubiria majibu toka kwa Mw'Mungu, ilhali unaishi na 'kibaka' ndani...

Kwenye ndoa kuna mengi, si ajabu katika baadhi ya nyumba matendo haya yapo sana, lakini kama alivyosema nanihii, it's very embarrasing kuyaelezea hadharani, unless wakikorofishana ndio siri zinaanikwa hadharani...
 
...ukamshauri nini??

kwanza samahanini niliiacha hii topic tangu siku ilee...unajua tena masuala ya krismas..

anyway..

asante Mbu kwa kutuhabarisha maana ya "kijiji"..

nikirudi kwenye swali lako Laligeni, kuhusu yule dada mwenye mume jambazi nilimshauri amuone lawyer kimya kimya kwanza (asiyetetea majambazi) ili apate ushauri wa kisheria, aliniambia atanipa feedback ya kinachoendelea.. ila kusema kweli naogopa hata kutaka kujua zaidi nini kinachoendelea maana jamaa yaelekea ni jambazi hasa...
 
...nilipokuwa 'kijijini' nilihadithiwa visa vingi vya kusikitisha, kimojawapo ni hiki;

\\huu ubishi wa kijijini hata sioni mantiki yake kwa sababu Mbu kasema kijijini in quotes, ina maana hilo neno lina maana zaidi ya its literal meaning...so inabidi ufikiria zaidi ya hapo, ndo uandishi wa Mbu na wengine wetu hapa. Sio lazima awaambie alikuwa likizo Mwanza au Tanga au Dar au Mbeya au Ntwara (inategemea ntu na ntu)

Nikirudi kwenye hoja ya msingi ni kwamba mi naona ni kitu cha ajabu sana kuwa na mpenzi mdokozi huyu atakuwa anajiibia hata yeye mwenyewe! Kama akianza ivo ujue kuna wakati itafika atakuliza kiukweli ukweli!
 
...!ndugu,upo?:D:D
 
...hivi ni halali kweli kuishi maisha ya ndoa halafu mkeo.mumeo asijue PIN ya account zako benki kweli? incase unapatwa na dharura itakuwaje? anyway...

Hiyo case ya mwanadada kuchukuliwa vito vyake vya dhahabu bado halijapatiwa ufumbuzi...yataka moyo kusubiria majibu toka kwa Mw'Mungu, ilhali unaishi na 'kibaka' ndani...

Kwenye ndoa kuna mengi, si ajabu katika baadhi ya nyumba matendo haya yapo sana, lakini kama alivyosema nanihii, it's very embarrasing kuyaelezea hadharani, unless wakikorofishana ndio siri zinaanikwa hadharani...

mi nizungumzie hapo tu kuw ainategemeana mnaaminiana kiasi gani, unajua kuna wengine wameolewa basi tena ndo hawana haki ya kujua kipato cha mume/mke nk, so hata kujua ivo vitu sio rahisi
 
kuna mifano ''halisi'' kabisa ninayo jamaa anaishi na mkewe kama ASKARI NA MHALIFU!....hatari tupu
 
Inapofika hatua ya mwenza kuiba/kupunguza salio katika ATM anakuwa na tatizo la uteja. Iwapo mwenza anaiba vidani anaweza kuwa ni teja na amekosa njia nyingine ya kuweza kupata kipato ili kupata madawa yake.

Hali kadhalika iwapo mwenza anadokoa pesa katika ATM, inawezekana kuna upungufu mkubwa wa matumizi ya mambo ya ndani. Hivyo pasipo kusubiri kupewa fedha ili akanunue kitoweo huamua mwenyewe kuingia kwenye ATM. Hii usababishwa na udhaifu mkubwa wa mawasiliano baina yao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom