Mdogo wangu Metacha 'Poti' Mnata, Meneja wako Jemedari Said atakuponza na Yanga SC 'watakuua' sasa!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,518
108,793
Japo ni 'Poti' wangu kabisa kutoka Mkoani Mara (Musoma) ila kwa hili na haya yanayokutokea sasa hapo Yanga SC Kipa Metacha Mnata wala sikuonei 'Huruma' kabisa kwani umeyataka Mwenyewe na tunaokupenda na Wanaokupenda tumekushauri vya kutosha na unatuona Mangumbaru (Wajinga) na Mapopoma (Wapumbavu) sasa Kazi Kwako.

Umeshauriwa na Kutahadhirishwa vya Kutosha kuwa hama Yanga SC kwakuwa hawakutaki na una Damu ya Kunguni kuanzia kwa Uongozi, Wachezaji wenzako hadi Mashabiki ila hutaki Kusikia.

Unamsikiliza na Kumuamini Meneja wako Jemedari Said ( Mchambuzi wa Michezo EFM ) ambaye ni mwana Yanga SC 'lia lia' kuwa usihame Yanga SC na uwe 'mvumilivu' wakati Wao (Yanga SC) wenyewe si tu hawakutaki bali hawakupendi pia.

Kipa Metacha Mnata 'Poti' hii ni mara ya Nne (4) sasa unakumbana na Matatizo lakini bado huoni tu kuwa 'Hatari' inakufuata na nadhani kwa Kuamua Kwako kubakia Yanga SC kwa Kumsikiliza Meneja wako Jemedari Said ambaye 'anatajirika' kupitia Jasho lako umeamua Kujitoa 'Mhanga' kuwa hata 'ukipigwa' au 'Kuumizwa' ni sawa.

Mwezi Mmoja au Miezi Miwili iliyopita Azam FC walikufuata kwa ahadi ya Tsh 50 Milioni na Mshahara wa Milioni 5 kwa Mwezi ukawakatalia kama kawaida yako kwa Kumsikiliza Meneja wako Jemedari Said ambaye hadi huwa anaenda kwa Waganga 'Kukurogea' ili upate namba hapo Yanga SC.

Simba SC nao walikufuata kwa ahadi ya Tsh 75 Milioni na Mshahara wa Milioni 7 na ukakubali kabisa ghafla ukiwa njiani kwenda kuonana na Watu wa Simba SC Meneja wako Jemedari Said akakupigia Simu na kukuzuia Kumalizana na Simba SC na kukutaka ubakie Yanga SC.

Metacha Mnata 'Poti' umeamua Kujitoa'Mhanga' kubakia Yanga SC ila GENTAMYCINE najua huna Mahusiano mazuri na Kocha wako wa Makipa Raia wa Kenya Razak Siwa na mmekuwa hata mkigombana mara kwa mara kwakuwa hakupendi na anataka Mkenya mwenzake Kipa Farouq Shikalo ndiyo awe anadaka ila unapangwa Wewe kwa Amri ya Mwenyekiti wa Yanga SC Dkt. Mshindo Msolla ila akina Injinia Hersi Said na GSM yake wala hawakutaki kwakuwa wanakuhusisha kuwa na 'Vinasaba' na Simba SC.

Kwakuwa Kitendo cha Kishamba na Kipumbavu ulichokifanya Jana 'Kimekugharimu' na umesimamishwa nakushauri usikubali Kudaka Mechi ya "Derby' kama ikitokea mkamaliza na Yanga SC kwa 'Upuuzi' ulioufanya jana kwani najua Yanga SC inaenda Kufungwa mengi na Simba SC siku hiyo hivyo 'Ukidaka' Wewe na hivi wasivyokupenda 'Watakuua' na kuanza kutupa Kazi 'Poti' zako akina GENTAMYCINE wa Kukusafirisha ukiwa 'Maiti' kwenda Mazikoni Mkoani Mara (Musoma).

Na usichokijua sasa 'Poti'wangu Kipa Metacha Mnata anayekumaliza hapo kwa 'Ndumba' hadi 'Nuksi' tu zinakuandama Kutwa wala siyo Kipa Farouq Shikalo bali ni hako ' Kamwanangu ' kutoka Kawe Kipa Ramadhan Kabwili ambaye Kutwa anazungushwa kwenda kwa Waganga na Rafiki yake 'Kipa Mwenzake' Mtani wangu kutoka Kigoma Juma Kaseja ili 'uharibikiwe' na aaminiwe rasmi Yeye.

Achana na Jemedari Said anakuponza.
 
Hivi lile dole la kati alilowaonesha mashabiki wa deportivo la UTO si ndio kwa kizungu wanasemaga FAKENI ati 🤔🤔🤔
 
Kwa Metacha pale hamna kipa. Iwapo Simba na Azam kweli waliweka mzigo kama mleta mada alivyosema ili wamchukue basi nina mashaka sana na uwezo wa kamati zao za usajili.Ukimpeleka kipa mpya Simba lazima awe zaidi ya Manula na kwa Azam lazima awe zaidi ya Kigonya vinginevyo itakuwa ni upotezaji wa pesa tu.

Metacha kwa sasa aachane kabisa na Yanga kwani ni muda mrefu sasa wameshaonesha kutokuwa na imani naye kiasi hata ikitokea yale makosa ya kibinadamu anayoweza fanya kipa yoyote kwake inaonekana amechomesha timu makusudi. Na ni vizuri kwake akaenda hizi timu za katikati ya ligi kuanza moja kwani umri bado unamruhusu na hata ikiwezekana atafute timu nje ya nchi hata kama ni madaraja ya chini itamsaidia zaidi.
 
Mleta mada unaamini sana ushirikina wakati hakuna kitu kama hicho katika mpira ni njia tu ya wajanja kupiga pesa.

Mathalani, timu zote mbili zikichangia mganga moja halafu awatendee haki sawa, matokeo yatakuwaje.

Tuache mambo ya kijinga, mpira ni mazoezi, mbinu na ufundi. Wachezaji wanapaswa kuwa very disciplined with the dictates of the game and nothing else.
 
Japo ni 'Poti' wangu kabisa kutoka Mkoani Mara (Musoma) ila kwa hili na haya yanayokutokea sasa hapo Yanga SC Kipa Metacha Mnata wala sikuonei 'Huruma' kabisa kwani umeyataka Mwenyewe na tunaokupenda na Wanaokupenda tumekushauri vya kutosha na unatuona Mangumbaru (Wajinga) na Mapopoma (Wapumbavu) sasa Kazi Kwako.

Umeshauriwa na Kutahadhirishwa vya Kutosha kuwa hama Yanga SC kwakuwa hawakutaki na una Damu ya Kunguni kuanzia kwa Uongozi, Wachezaji wenzako hadi Mashabiki ila hutaki Kusikia.

Unamsikiliza na Kumuamini Meneja wako Jemedari Said ( Mchambuzi wa Michezo EFM ) ambaye ni mwana Yanga SC 'lia lia' kuwa usihame Yanga SC na uwe 'mvumilivu' wakati Wao (Yanga SC) wenyewe si tu hawakutaki bali hawakupendi pia.

Kipa Metacha Mnata 'Poti' hii ni mara ya Nne (4) sasa unakumbana na Matatizo lakini bado huoni tu kuwa 'Hatari' inakufuata na nadhani kwa Kuamua Kwako kubakia Yanga SC kwa Kumsikiliza Meneja wako Jemedari Said ambaye 'anatajirika' kupitia Jasho lako umeamua Kujitoa 'Mhanga' kuwa hata 'ukipigwa' au 'Kuumizwa' ni sawa.

Mwezi Mmoja au Miezi Miwili iliyopita Azam FC walikufuata kwa ahadi ya Tsh 50 Milioni na Mshahara wa Milioni 5 kwa Mwezi ukawakatalia kama kawaida yako kwa Kumsikiliza Meneja wako Jemedari Said ambaye hadi huwa anaenda kwa Waganga 'Kukurogea' ili upate namba hapo Yanga SC.

Simba SC nao walikufuata kwa ahadi ya Tsh 75 Milioni na Mshahara wa Milioni 7 na ukakubali kabisa ghafla ukiwa njiani kwenda kuonana na Watu wa Simba SC Meneja wako Jemedari Said akakupigia Simu na kukuzuia Kumalizana na Simba SC na kukutaka ubakie Yanga SC.

Metacha Mnata 'Poti' umeamua Kujitoa'Mhanga' kubakia Yanga SC ila GENTAMYCINE najua huna Mahusiano mazuri na Kocha wako wa Makipa Raia wa Kenya Razak Siwa na mmekuwa hata mkigombana mara kwa mara kwakuwa hakupendi na anataka Mkenya mwenzake Kipa Farouq Shikalo ndiyo awe anadaka ila unapangwa Wewe kwa Amri ya Mwenyekiti wa Yanga SC Dkt. Mshindo Msolla ila akina Injinia Hersi Said na GSM yake wala hawakutaki kwakuwa wanakuhusisha kuwa na 'Vinasaba' na Simba SC.

Kwakuwa Kitendo cha Kishamba na Kipumbavu ulichokifanya Jana 'Kimekugharimu' na umesimamishwa nakushauri usikubali Kudaka Mechi ya "Derby' kama ikitokea mkamaliza na Yanga SC kwa 'Upuuzi' ulioufanya jana kwani najua Yanga SC inaenda Kufungwa mengi na Simba SC siku hiyo hivyo 'Ukidaka' Wewe na hivi wasivyokupenda 'Watakuua' na kuanza kutupa Kazi 'Poti' zako akina GENTAMYCINE wa Kukusafirisha ukiwa 'Maiti' kwenda Mazikoni Mkoani Mara (Musoma).

Na usichokijua sasa 'Poti'wangu Kipa Metacha Mnata anayekumaliza hapo kwa 'Ndumba' hadi 'Nuksi' tu zinakuandama Kutwa wala siyo Kipa Farouq Shikalo bali ni hako ' Kamwanangu ' kutoka Kawe Kipa Ramadhan Kabwili ambaye Kutwa anazungushwa kwenda kwa Waganga na Rafiki yake 'Kipa Mwenzake' Mtani wangu kutoka Kigoma Juma Kaseja ili 'uharibikiwe' na aaminiwe rasmi Yeye.

Achana na Jemedari Said anakuponza.
ukitulia huwa unaandika kwa mpangilio kumbe,

Kumbe dogo Hana akili uyo, Simba na Azam walionyesha kumuitaji akaringa, kwaiyo ameridhika kubakia hasipopendwa
 
'Hasipopendwa' ndiyo Kiswahili cha wapi hiki? Kumbe na Wewe huwa huandiki Kimpangilio kama hivi?
 
Mleta mada unaamini sana ushirikina wakati hakuna kitu kama hicho katika mpira ni njia tu ya wajanja kupiga pesa.

Mathalani, timu zote mbili zikichangia mganga moja halafu awatendee haki sawa, matokeo yatakuwaje.

Tuache mambo ya kijinga, mpira ni mazoezi, mbinu na ufundi. Wachezaji wanapaswa kuwa very disciplined with the dictates of the game and nothing else.
Wee ndumba ipo shehe, unaweza shangaa timu mnapoteana mpira hauonekani hata man city anaweza kukaa kwa simba
 
Back
Top Bottom