Mdogo wangu Ibrahim Ajib ' Mido ' kama hii taarifa ni ya kweli basi japo ni mwana Simba SC mwenzio ila ' umeniangusha ' sana na mno

Unakuja Simba SC mdogo wangu hapo utapata Namba ya nani? Kwanini hupendi kusikia Mawazo ya Kaka zako ambao tunakupenda Ibra? Hivi kweli kwa Mfumo wa Kocha Aussems Wewe utapata Namba kweli ndani ya Kikosi cha Simba hii ya sasa Ibra? Ni kwanini Maisha ya hapa Dar es Salaama yanakulevya na yanakuridhisha hivi Mdogo wangu Ibra? Najua kuwa umeshawishiwa na Rafiki zako wakubwa akina Mkude, Ndemla na Tshabalala ila nawe pia ulipaswa ujitathmini Kwanza kabla ya Kuamua ulichoamua Ibra.

Mimi GENTAMYCINE ni Kaka yako, Rafiki yako mzuri tu tena tokea ukiwa Boom FC na wakati ukicheza pia pale Uwanja wa Shule ya Msimbazi achilia mbali Uwanja wa Barafu, ule wa Tanganyika Packers Kawe na hata pale Biafra ukiwa na ' Washikaji ' zako akina Mkude na Sure Boy wa Azam na unajua fika kuwa Mimi ni mwana Simba SC lia lia ila nilikushauri kuwa usije Simba SC na kukupa Sababu zangu nyingi ila kuna Mtu wako wa karibu yupo TRA Makao Makuu ' amenitonya ' kuwa jana ulikuwa na Viongozi wa Simba na huenda ndani ya Saa 48 au 72 kutoka sasa ukasaini rasmi Simba SC.

Nilikushauri vizuri sana Mdogo wangu Ibra kuwa kwa Mafanikio yako makubwa ya Kimpira ni vyema ukaondoka kabisa Tanzania hii ili ' ukatengenezwe ' zaidi na Makocha wakubwa wa Timu zingine na nakumbuka ulipopata ' Offer ' ya TP Mazembe nilifurahi mno na kujua kuwa usingeiacha hiyo bahati na kwa masikitiko makubwa sana nikaja kuambiwa kuwa ' umewachomolea ' kwakuwa tu Simba SC wanakuhitaji na Wewe umekubali kabisa kuingia ' Mtegoni ' na unaelekea Kusaini nao.

Ibra Mdogo wako kutoka Ilala Bungoni najua kuwa umeangalia Pesa na Maisha mazuri ya hapa Jijin Dar es Salaam hasa ukizingatia kuwa unapenda sana Starehe ila ipo Siku utakuja Kunikumbuka Mimi Kaka yako GENTAMYCINE na naamini hata Rafiki yako mkubwa SaluRaka ambaye sasa yupo nchini Ujerumani ( baada ya Kujilipua / Kuchukua Uraia wa huko kama Mkimbizi ) nae akisikia kuwa umekataa kwenda TP Mazembe atakushangaa achilia mbali Kaka yake Hemed wa TRA ambaye ndiyo Mshauri wako Mkuu najua nae pia atakuwa amesikitika mno tu.

Hivi Ibra ungevumilia tu uende zako TP Mazembe ukapikwe na ukatengenezwe hata kwa miaka yako miwili na ukomae vyema unataka kuniambia na Wewe Vilabu vikubwa vya Ulaya visingekuona na Kukusajili? Ibra ni mara ngapi Mwenzako Mbwana Samatta amekuwa akikuambia Wewe na Rafiki yako Mkude kuwa mnachelewa hapa Tanzania na kwamba nyie ni wa Ulaya tu? Hivi hamuoni Mafanikio yake huko KRC Genk?

Najua mida ya baadae tunaweza Kukutana maeneo ya Morocco Hotel katika Duka za Mke wa Mchezaji mwenzako wa Yanga Beki Gadiel Michael ambako huwa unapenda kuwa hapo ukiwa na Wachezaji wenzako bila Kumsahau Beki Mtukutu na Kaka yako Kelvin Yondan ila nimelazimika Kuja na hii ' Kitu ' hapa ili kuwa ' Funzo ' kwa Wachezaji wengine kuwa achaneni na mawazo ' Finyu ' kuwa Maendeleo ya Mchezaji basi ni lazima tu achezee Klabu za Simba na Yanga wakati kumbe ukweli siyo huo.

Nina uhakika kuwa kwa hili Bandiko langu kuna wana Simba SC Wenzangu watanikasirikia kama siyo kuninunia kwakuwa sijapendelea Ibra kuja Simba SC yetu ila ' Kiufundi ' kabisa na ninavyomjua Ibrahim Ajibu alivyo na Kocha wetu wa Simba SC hatoweza kupata Nafasi ya Kudumu Kikosini na atasubiri mno kwa akina Chama, Niyonzima, Muzamiri na hata Ndemla ila kwa Maendeleo yake ya Kimpira angeenda Azam FC angepata Namba tena ya Kudumu ila angeenda huko TP Mazembe au hata Ulaya angefanya vyema zaidi.

Nimefurahi tu Kusikia kwamba Simba SC inamrudisha Beki wetu wa Vijana William Lucien ' Gallas ' ili aje acheze Namba yake ya Kiasili Beki Namba Mbili kwani si uwongo sikufurahishwa na Usajili wa Beki wa ' hovyo hovyo ' ambaye Kiwango chake Kimeshuka kama si Kupotea ghafla Zana Coulibaly na nasikia kuwa anaachwa rasmi ili Nafasi hiyo ya Beki Namba Mbili ibaki tu kwa Nicolas Gyan, William Lucien na Majeruhi Shomary Kapombe.

Mdogo wangu Ibrahim Ajib umeniangusha sana Kaka yako Mimi GENTAMYCINE ila nayaheshimu pia Maamuzi yako.

Nawasilisha.
Mawakala wake sio sahihi. Wanataka pesa nyingi kuliko kuangalia maendeleo ya ibra
 
kidevu alisema anataka su ya uhakika kwahiyo si tatizo akija ka sub ya maana japo kimpira najua atapotea ila angeenda Congo angekuwa mtu mwingine na angejenga cv kubwa maishani ambayo ni muhimu kwa timu yetu ya taifa
 
Mtamlaumu Ajibu bure ila kumbukeni huyo kijana yuko kwenye mfungo wa Ramadhan kwa vyovyote vile atakua anaendeshwa na akir ya swaum
Over
 
kidevu alisema anataka su ya uhakika kwahiyo si tatizo akija ka sub ya maana japo kimpira najua atapotea ila angeenda Congo angekuwa mtu mwingine na angejenga cv kubwa maishani ambayo ni muhimu kwa timu yetu ya taifa

Umeandika vizuri sana Mkuu. Heko Kwako na huo ndiyo ukweli halisi ila nashangaa kwanini huyu ' Dogo ' Ibra haya Maisha ya Dar es Salaam, Tanzania anayapenda mno wakati kwa Kiwango na Kipaji chake ana uwezo mkubwa sana kuliko hata Mbwana Ally Samatta. Ajib kama akienda Vilabu Vikubwa vya TP Mazembe au Mamelodi Sundowns au Al Ahly kisha akakutana na Makocha wakubwa huko wakampika na kumjenga vyema nina uhakika atakuwa ' Mtamu ' zaidi ya alivyo sasa na Vilabu vingi huko Ulaya vitamgombania sana labda Changamoto Kubwa Kwake inaweza kuwa ni Umri kwani kwa ninavyomjua Umri anaoutaja sasa ni wa ' Pasipoti ' tu lakini siyo ule Umri wake halisia.
 
Umri wake ni miaka 22 hii ndio bongo ila kumbuka kacheza simba miaka zaid ya mitatu pili kacheza yanga miaka miwili hapo kwa hesabu ya haraka haraka itakua alianza kucheza soka la kulipwa akiwa na umri chini ya miaka 16 ambapo pia kisheria nikosa
 
yawezekana mshauri wake kashapata kiasi flani ili kumshawishi abaki TZ, ila kiuhalisia angeenda TP ingekuwa kajipanulia wigo zaidi, yote kwa yote tumuombee mafanikio katika maisha ya mpira kingine sidhani ka tunacho cha kufanya dhidi yake
 
Ukiniambia Ajib ana miaka 28 au 30 nitakubaliana nawe tena kwa 100% Mkuu ila huo Umri anaoutaja sasa sijui wa 22 akawadanganye wengine. Sasa bora ya Ajibu kwenye suala la Umri huwezi amini hadi leo Kipa Juma Kaseja Umri wake anadai ni miaka 30 wakati nakumbuka amesoma na Wachezaji wenzake tena wakiwa pale Makongo kama Boniface Pawasa, Ephraim Makoye na Wilfred Kidau huyu wa TFF sasa bila kumsahau Rafiki yangu mkubwa Kocha Suleiman Abdallah Matola a.k.a Mzambia a.k.a Veron ambao wote hawa sasa miaka yao ni 40's ila Yeye ( Kaseja ) bado anasema yupo katika huo Umri wa 30's na bado kuna Watu wamemuamini kabisa. Huwa nacheka mno Mkuu.
 
Ni kweli na tumuachie tu Yeye mwenyewe. Nasikia kaamua Kuchukua hizo Milioni 80 na Gari jingine Jipya la Kifahari. Ila kwa Mimi ninavyojua kama angeenda zake TP Mazembe angelipwa Mshahara mkubwa kuliko ambao atapewa Simba SC kama hizi Tetesi za Yeye Kusajili Simba SC zikiwa Kweli ila nina uhakika kwa Kipaji chake na Uwezo wake wa Kucheza Mpira kama angeenda Ulaya basi hizo Tsh Milioni 80 atakazopewa Simba SC kwa Mkataba wa Miaka Miwili huko angekuwa anapewa hiyo Pesa kwa Wiki na huko angekula ' Bata ' za Kufa Mtu hadi angezichoka. Ilala na Dar es Salaam inamuharibu ' Dogo ' huyu.
 
Ukiniambia Ajib ana miaka 28 au 30 nitakubaliana nawe tena kwa 100% Mkuu ila huo Umri anaoutaja sasa sijui wa 22 akawadanganye wengine. Sasa bora ya Ajibu kwenye suala la Umri huwezi amini hadi leo Kipa Juma Kaseja Umri wake anadai ni miaka 30 wakati nakumbuka amesoma na Wachezaji wenzake tena wakiwa pale Makongo kama Boniface Pawasa, Ephraim Makoye na Wilfred Kidau huyu wa TFF sasa bila kumsahau Rafiki yangu mkubwa Kocha Suleiman Abdallah Matola a.k.a Mzambia a.k.a Veron ambao wote hawa sasa miaka yao ni 40's ila Yeye ( Kaseja ) bado anasema yupo katika huo Umri wa 30's na bado kuna Watu wamemuamini kabisa. Huwa nacheka mno Mkuu.

Pia naweza nikaamin umri ukawa sababu ya Ibrahim Ajibu kukwepa kwenda Tp Mazembe hyo ni sababu ya kwanza ila sabubu ya pili na elimu ya masuala ya soka nayo pia hana hata haoni mfano kwa wenzaki kama kina Mao Mkami, Kichuya, Msuva, Yahya Zaid bila kumsahau Samatta

Elimu Elimu Elimu=E.Lowasa
 
Sahihi kabisa Mkuu.
 
Unakuja Simba SC mdogo wangu hapo utapata Namba ya nani? Kwanini hupendi kusikia Mawazo ya Kaka zako ambao tunakupenda Ibra? Hivi kweli kwa Mfumo wa Kocha Aussems Wewe utapata Namba kweli ndani ya Kikosi cha Simba hii ya sasa Ibra? Ni kwanini Maisha ya hapa Dar es Salaama yanakulevya na yanakuridhisha hivi Mdogo wangu Ibra? Najua kuwa umeshawishiwa na Rafiki zako wakubwa akina Mkude, Ndemla na Tshabalala ila nawe pia ulipaswa ujitathmini Kwanza kabla ya Kuamua ulichoamua Ibra.

Mimi GENTAMYCINE ni Kaka yako, Rafiki yako mzuri tu tena tokea ukiwa Boom FC na wakati ukicheza pia pale Uwanja wa Shule ya Msimbazi achilia mbali Uwanja wa Barafu, ule wa Tanganyika Packers Kawe na hata pale Biafra ukiwa na ' Washikaji ' zako akina Mkude na Sure Boy wa Azam na unajua fika kuwa Mimi ni mwana Simba SC lia lia ila nilikushauri kuwa usije Simba SC na kukupa Sababu zangu nyingi ila kuna Mtu wako wa karibu yupo TRA Makao Makuu ' amenitonya ' kuwa jana ulikuwa na Viongozi wa Simba na huenda ndani ya Saa 48 au 72 kutoka sasa ukasaini rasmi Simba SC.

Nilikushauri vizuri sana Mdogo wangu Ibra kuwa kwa Mafanikio yako makubwa ya Kimpira ni vyema ukaondoka kabisa Tanzania hii ili ' ukatengenezwe ' zaidi na Makocha wakubwa wa Timu zingine na nakumbuka ulipopata ' Offer ' ya TP Mazembe nilifurahi mno na kujua kuwa usingeiacha hiyo bahati na kwa masikitiko makubwa sana nikaja kuambiwa kuwa ' umewachomolea ' kwakuwa tu Simba SC wanakuhitaji na Wewe umekubali kabisa kuingia ' Mtegoni ' na unaelekea Kusaini nao.

Ibra Mdogo wako kutoka Ilala Bungoni najua kuwa umeangalia Pesa na Maisha mazuri ya hapa Jijin Dar es Salaam hasa ukizingatia kuwa unapenda sana Starehe ila ipo Siku utakuja Kunikumbuka Mimi Kaka yako GENTAMYCINE na naamini hata Rafiki yako mkubwa SaluRaka ambaye sasa yupo nchini Ujerumani ( baada ya Kujilipua / Kuchukua Uraia wa huko kama Mkimbizi ) nae akisikia kuwa umekataa kwenda TP Mazembe atakushangaa achilia mbali Kaka yake Hemed wa TRA ambaye ndiyo Mshauri wako Mkuu najua nae pia atakuwa amesikitika mno tu.

Hivi Ibra ungevumilia tu uende zako TP Mazembe ukapikwe na ukatengenezwe hata kwa miaka yako miwili na ukomae vyema unataka kuniambia na Wewe Vilabu vikubwa vya Ulaya visingekuona na Kukusajili? Ibra ni mara ngapi Mwenzako Mbwana Samatta amekuwa akikuambia Wewe na Rafiki yako Mkude kuwa mnachelewa hapa Tanzania na kwamba nyie ni wa Ulaya tu? Hivi hamuoni Mafanikio yake huko KRC Genk?

Najua mida ya baadae tunaweza Kukutana maeneo ya Morocco Hotel katika Duka za Mke wa Mchezaji mwenzako wa Yanga Beki Gadiel Michael ambako huwa unapenda kuwa hapo ukiwa na Wachezaji wenzako bila Kumsahau Beki Mtukutu na Kaka yako Kelvin Yondan ila nimelazimika Kuja na hii ' Kitu ' hapa ili kuwa ' Funzo ' kwa Wachezaji wengine kuwa achaneni na mawazo ' Finyu ' kuwa Maendeleo ya Mchezaji basi ni lazima tu achezee Klabu za Simba na Yanga wakati kumbe ukweli siyo huo.

Nina uhakika kuwa kwa hili Bandiko langu kuna wana Simba SC Wenzangu watanikasirikia kama siyo kuninunia kwakuwa sijapendelea Ibra kuja Simba SC yetu ila ' Kiufundi ' kabisa na ninavyomjua Ibrahim Ajibu alivyo na Kocha wetu wa Simba SC hatoweza kupata Nafasi ya Kudumu Kikosini na atasubiri mno kwa akina Chama, Niyonzima, Muzamiri na hata Ndemla ila kwa Maendeleo yake ya Kimpira angeenda Azam FC angepata Namba tena ya Kudumu ila angeenda huko TP Mazembe au hata Ulaya angefanya vyema zaidi.

Nimefurahi tu Kusikia kwamba Simba SC inamrudisha Beki wetu wa Vijana William Lucien ' Gallas ' ili aje acheze Namba yake ya Kiasili Beki Namba Mbili kwani si uwongo sikufurahishwa na Usajili wa Beki wa ' hovyo hovyo ' ambaye Kiwango chake Kimeshuka kama si Kupotea ghafla Zana Coulibaly na nasikia kuwa anaachwa rasmi ili Nafasi hiyo ya Beki Namba Mbili ibaki tu kwa Nicolas Gyan, William Lucien na Majeruhi Shomary Kapombe.

Mdogo wangu Ibrahim Ajib umeniangusha sana Kaka yako Mimi GENTAMYCINE ila nayaheshimu pia Maamuzi yako.

Nawasilisha.
Wakat mwingine zinarudi.
 
Back
Top Bottom