Mdogo wangu aliwahi kuniambia, asilimia kubwa ya wahitimu wa elimu ya juu wanaohudhuria "Graduation Ceremony" ni wale wenye GPA za chini. Is he right?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za muda huu watanzania wa humu JamiiForums.

Mdogo wangu aliwahi kuniambia, asilimia kubwa ya wahitimu wa elimu ya juu wanaohudhuria "Graduation Ceremony" ni wale wenye GPA za chini. Was he right?

images (4).jpg


Mwaka wa 2017 nilipata fursa ya kuhudhuria mahafali ya wahitimu wa elimu ya juu pale chuo cha ******** kipo huku Dar. Mimi kama mgeni mualikwa nilienda kuwavisha taji watoto wa mama yangu mdogo na mkubwa (mmoja wa kike na mwingine wa kiume).

Hawa madogo mmoja alisomea Accountancy na mwingine kama sijakosea alisomea masuala ya Ualimu hivi. Sasa siku ile ya maafali nilikuwa niende kwenye mishe zangu Kigamboni ila nikasema ngoja nikawavishe mataji hawa majamaa isije baade wakasema kaka hajui kushirikiana vema na ndugu zake.

Basi muda ulipofika mimi huuyoooo nduki mpaka chuoni kwao nikakuta watu weeengi wakiwa ndugu, jamaa na marafiki wamekuja kwa ajili ya kufurahi na ndugu zao. Ngoja nifupishe story isiwe ndefu saaaaana.

Nilifanikiwa kumvisha taji ndugu yangu mmoja huyu wa kike na kufurahi naye. Tulifurahi sana kunywa na kula ila yule mwingine baada ya kumuuliza kwanini hakuja katika sherehe hizi kuna jibu alinipa.

images (5).jpg


Jibu alilonipa ni kwamba, "hawezi kuhudhuria "Graduation Ceremony" kwa maana GPA yake ni kubwa mno na kamwe picha za kwenye graduation haziwezi kuambatanishwa katika barua ya maombi ya kazi. Wahitimu wengi wanaopapatikia sherehe za mahafali ni wale wenye GPA za chini".

Je, huyu dogo yupo sahihi au yeye ndio wale watu wanaoitwa "anti-social" (wasiopenda kuchangamana na wenzao)?

Maoni ya wadau
=====
Waliofaulu kimagumashi huwa na mbwembwe sana

1. Tafrija nzito lazima iandaliwe

2.Usafiri wa hali ya juu

3.Wengi wana ka uwezo au ndugu zao wanauwezo

4. Watakuwa na ndugu ukoo mzima na watoto

5.Atashinda na Joho wiki nzima na kutembea nalo kila mahala huku akipiga picha kila sehemu
=====
Kweli kabisa, mm huwa naona ni kupotezeana muda, niliyohudhuria ni ya form4 tu... form 6 niliamua kutoka mapema kwenda kulala, first degree na MSc sikuibuka kabisa licha ya kwamba zote GPA top 3 ya class yangu haikukosekana... na hata jamaa zangu kama 3 hivi tuliokuwa vizuri class hawakuibuka.. wengi wanatumia ile nafasi kupiga picha, kupost mitandaoni na ukifuatilia asilimia kubwa hupenda kujionyesha kwamba na wao wamefanikiwa kuziba lile ombwe la uwezo mdogo darasani...
=====
Ni kweli,nilipata gpa ya 4.4 kwenye recognized University lakin sikuhudhuria mahafali.Wale wenye gentleman degree Sasa walijaa Kama wote
=====
Inawezekana lakin maana wao wakiwa chuo wanafanya na mishe zingine za hela labda afu sisi wa konko tunajua life ni gpa tu
=====
Dogo yupo sahihi 98%. Mara nyingi wenye GPA kubwa ni wale wanaasomea kijiji, hawa huwa hawana time na chochote duniani zaidi ya kukariri tu madesa. Hawana hobi na mara nyingi anti social. We unategemea kidukulilo au warumi apate first class
=====
Yupo sahihi 100% mimi sikuwahi kwenda toka degree, masta na professional body. bahati mbaya tu nilohudhuria ya Advance kwa sababu nilikuwa boarding
=====
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Sidhani, japo kweli mi sikwendaga na nilikua na gpa kubwa ila sababu nilikua sina hata mia, ningeenda. Kwa hiyo inamaana wenye gpa ndogo walikua na hela kuliko mi nilokua na gpa kubwa? Inawezekana lakin maana wao wakiwa chuo wanafanya na mishe zingine za hela labda afu sisi wa konko tunajua life ni gpa tu
 
Wao wana afadhali kuliko wewe usiyejua hata kuandika. chuo cha kikuu cha.....ndiyo nini?

Sio tuu hujui kuandika ipasavyo, bali pia hujui nomino gani inatakiwa iwe na herufi kubwa na ipi haijui.

Kilaza Mkubwa wewe!
Sa jamaa amekukosea nini mzee๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
"hawezi kuhudhuria "Graduation Ceremony" kwa maana GPA yake kubwa inamtosha. Kamwe picha za kwenye graduation haziwezi kuambatanishwa katika barua ya maombi ya kazi. Wengi wanaopapatikia sherehe za mahafali ni wale wenye GPA ndogo na za kuungaunga".
Nafikiri swali halikupaswa kuuuliza 'Je yupo sahihi'

Swali ni โ€˜Je ana akili timamuโ€™

kwa thinking yangu tu Huyo ana tatizo kwenye akili.
 
Back
Top Bottom