Mdogo wake na Rostam Aziz amepelekwa mahakamani kwa dawa za kulevya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdogo wake na Rostam Aziz amepelekwa mahakamani kwa dawa za kulevya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KING COBRA, Nov 12, 2011.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Nimesituka baada ya kusikia kwamba Mdogo wake na Rostam Aziz aitwaye ASSAD ABDULSUL AZIZI amepelekwa mahakamani jana kwa kosa la kukutwa na 92.2kg. Hapa naogopa kumupongeza Rais Kikwete lakini namumpongeza Kamanda Nzowa.

  Taarifa nilizo sikia ni kwamba Assad alikamatwa mapema baada ya Rais Kikwete kutuhumu Wachungaji na Maskofu kushiriki katika biashara haramu za dawa za kulevya!!!

  Pia muda mufupi alikamatwa Askofu wa pale biafra akiwa na kilo nyingi na akatngazwa kwa nguvu kubwa mpaka BUNGENI WAMEONYESHA PICHA YAKE Mpaka Salva RWEYEMAMU AKAANDAA kashfa ya kuyafilisi makanisa .

  Sasa swali langu ni kwa nini ASSAD alikamatwa siku nyingi lakini mkanda wake haukuonyeshwa Bungeni??
  Kwa nini ASSAD alikamatwa siku nyingi na wamechelewesha kumupeleka Mahakamani???

  ZIPO tetesi kuwa Rostam AZIZ amekataa kuwa huyo si mdogo wake , je hapa kuna mahusiano ya suala la kijivua gamba??? ASSAD na Fred Lowasa wanaonekana kundi moja baada ya mtandao wa Nzowa kunasa $1bils kweny account zao je, hii ni hatua ya vusasi??

  Wauza madawa ya kulevya ndani ya CCM na serikali walikuwa hawakamatwi , kwa sababu walikuwa pamoja , je serikali inafanya kazi kwa visasi??

  Tunajua hata nyaraka za kagoda zilifichwa sana lakini baada ya kuanza kugombania mali nyaraka zimesambazwa!!!   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  chanzo mkuu
   
 3. Fullfigadiva J

  Fullfigadiva J Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi habari in tetesi au zina ukweli. Mbona wauza powder wako wengi. Itaakuwa imekaa vizuri sana. Hasa kwa wakati huu vijana wetu wanaharibika na mapoda. Wajaribu watembelee magomeni maana watu 10 kati yao nane wanauza dawa za kulevya.
   
 4. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mdogo wake na rostam amekamatwa kabla ya ccm kujivua gamba lakini kapelekwa jana mahakamani mkoani Tanga.

  sorce :TANZANIA DAIMA LEO

   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu KING COBRA, nchi hii ina viongozi wa ajabu kweli!! Na nchi pekee yenye viongozi wengi wezi ambao wananchi ndo wanawaweka kutokana na kukosa elimu ya uraia, pamoja na vitisho vya hao wezi.
   
 6. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  willium lukuvi tunataka uonyeshe mkanda wa namna assad alivyo kamatwa maana alipo kamatwa askofu mulikimbilia kuliarifu bunge sasa amekamatwa kada wa ccm , je ccm inaongzwa kwa fedha za dawa za kulevya???

  Nani aliyemusaidia kuingiza karibu gunia zima la dawa za kulevya ??
  Nani alikuwa anamulinda??
  Mpaka muvuane magamba kwanza ndipo mkamatane??

  Ndio maana hata suala la ushoga mupo kimya !!!
   
 7. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana jf ni nani asiyejua kuhusu sakata la kukamatwa 50kg za drugs mkoani mbeya ambapo baada ya hapo polisi wakaiba 8kg, na wamefanya uchunguzi wao wenyewe wakagundua madawa hayo yameibiwa chini ya ulinzi mkali masijala ffu mkoani mby.

  Watuhumiwa wakuu ni rco malimbisa , rpc nyombi na wenzake. Cha kushangaza wamekubali kuyamaliza na wamepeleka mahakamani 42kg!!!!

  Mhusika wa madawa hayo anafahamika na ni kada wa ccm!   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli mdogo wake, hapo ndipo inatakiwa Serikali isifiwe kwa kufuata mkondo wa Sheria na si jina.
   
 9. j

  jigoku JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Nilishasema humu jukwaani ya kwamba Mungu haja lala,wataendelea kuumbuana na mpaka tutawajua wote,ila itakuwa vema kama Lukuvi atapeleka mkanda wake tena bungeni,na hii najua iko wazi kwa wengine wetu,kwamba CCM -magamba wanakula pesa za powder,hili halifichiki.
  makada wao wengi ndo kazi yao hiyo,na wanajificha huko ili waweze kufanya uharamia wa biashara zao
   
 10. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Bakwata, Kanisa Katoliki watajwa dawa za kulevya [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 20 August 2011 21:23 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  [​IMG]Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Amina Mohamed Mwidau akifuta machozi baada ya kushindwa kuzuia hisia zake alipokuwa akichangia kwenye semina ya wabunge kuhusu athari za dawa za kulevya nchini. Amina alisema watoto wawili wa dada yake walipoteza maisha kutokana na kutumia dawa hizo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  Habel Chidawali, Dodoma
  KANISA Katoliki nchini na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) ni miongoni mwa taasisi za dini ambazo zimetajwa kutumiwa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kufanya biashara ya dawa za kulevya.Mmoja wa watoa mada kutoka Kikosi Kazi za Kupambana na Dawa za kulevya aliwaambia wabunge jana mjini Dodoma kwamba, eneo lingine ambalo limekuwa likitumika katika biashara hiyo ni vyama vya michezo vinavyosafirisha wanamichezo wake kwenda nje ya nchi kushiriki michezo ya kimataifa.

  Mtoa mada huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, alisema Tanzania iliwahi kupeleka vijana katika moja ya mikutano iliyoitishwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Benedict XVI nchini Australia, na kwamba miongoni mwa vijana hao walibainika kujihusisha na dawa za kulevya na kwamba wengine hawakuwahi kurejea nchini.

  Japokuwa mtoa mada huyo hakuweka wazi kwamba vijana hao walisafiri chini ya mwavuli wa Kanisa Katoliki nchini, tukio lilitokea Siku ya Vijana Duniani iliyofanyika mwaka 2008 katika mji mkuu wa Australia, na kuhudhuriwa na Papa Benedict XVI.

  Siku ya vijana duniani ni tukio la kimataifa ambalo huratibiwa na Kanisa Katoliki likiwajumuisha maelfu ya vijana kutoka sehemu mbalimbali duniani Katika mkusanyiko huo vijana hujadili masuala mbalimbali yanayohusu rika lao na mustakabali wao.

  Kwa upande wa Bakwata, alisema baadhi ya watu hujichomeka katika msafara wa watu wanaokwenda kuhiji Makka, lakini wakiwa na nia ya kujihusisha na biashara hiyo ya dawa za kulevya na kwamba, wakipata fursa hutimiza malengo yao.Kuhusu michezo, mtoa mada huyo alisema njia hiyo hutumiwa sana na watu ambao hujitokeza kufadhili safari za wanamichezo husika ili kutimiza matakwa yao ya biashara hiyo haramu.

  "Wakati mmoja, mzee Nyambui (Suleiyman) timu yake ya ndondi ilikuwa ikitafuta wafadhili kwenda nje, wakajitokeza wafanyabiashara watatu kwa ajili ya kutoa ufadhili huo, lakini wakatoa masharti kwamba lazima nao wasafiri," alisema na kuongeza:

  "Walitoa fedha hizo, lakini walipofika nchini Australia wale jamaa walikamatwa na dawa za kulevya ".

  Katika semina hiyo Serikali pia ilitekeleza ahadi yake iliyoahidi juu ya mkanda wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambapo ilionyesha hadharani, huku wabunge wakitaka wahusika wanyongwe mara moja.Kwa muda mrefu kumekuwa na kelele za wabunge na wananchi wakitaka majina na mtandao huo uwekwe hadharani ili wananchi wajua juu kilichoko nyuma ya pazia.

  Kikosi Kazi cha Kupambana na dawa za kulevya chini ya Kamishina, Godfrey Nzowa, kilitaja orodha hiyo kwa wabunge huku sehemu kubwa ya waliokamatwa wakionekana kuwa ni raia wa kigeni.Hata hivyo, baadhi ya raia wa Tanzania waliotajwa ni sehemu ya mtandao huo ambao watoa mada walisema kuwa ni mawakala."Si hao tu, lakini wapo Watanzania ambao ni mawakala katika vita hiyo ambayo kwa kweli tunakiri kuwa ni ngumu na inahitaji msukumo wa aina yake,'' alisema mtoa mada.

  Aliwataja baadhi ya waliokamatwa kuwa ni pamoja na Mchungaji Ikechuku Okidi wa Kanisa la lililopo Biafla jijini Dar es Salaam.Wengine ni pamoja na Mzee mmoja wa Kanisa, Mkazi wa Mbezi na mwanamtandao mkubwa wa dawa za kulevya ambaye ni mwanamke.
  Hata hivyo, watoa mada hao walilalamikia kitendo cha mahakama kuwaachia kwa dhamana watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao ni raia wa Pakstani wawili ambao walikamatwa kwa kilo 180 za Heroin."Tumesikitika sana na kuvunjika moyo kwa kitendo kilichofanywa na mahakama kwa kuwaachia kwa dhamana watuhumiwa wale huku tukiamini kuwa haikuwa haki kufanya hivyo,'' alisema msemaji huyo.

  Katika picha mbalimbali zilizoonyeshwa katika mkanda wa video hiyo, ziliwafanya wabunge kupandwa na jazba na kuanza kupiga kelele wakitaka watuhumiwa wanyongwe pamoja na jaji na mahakimu waliohusika kuwaachiwa huru raia hao wakamatwe na kuwajibishwa.

  Mbunge amwaga machozi
  Mbunge wa Viti Maalumu Amina Mohamed Mwidau (CUF) jana alimwaga machozi mbele ya wabunge wenzake na kushindwa kuendelea na mchango wake baada ya kueleza kuwa watoto wa dada yake walikufa kwa pamoja baada ya kuathirika na dawa za kulevya.
  "Mimi nataka wafanyabiashara hawa wanyongwe mara moja kwani wanaumiza watoto wetu. Watoto wa dada yangu walikufa wote kwa wiki moja kutokana na dawa hizo,'' alisema na kuanza kulia huku akishangiliwa na wabunge wengine.

  Baadhi ya wabunge waliopendekeza kunyongwa kwa wafanyabiashara hao ni pamoja na Moses Machali, Mohamed Sanya, Mohamed Mnyaa na Mohamed Rashid.Kwa upande wake, David Kafulila, yeye alitaka wafanyabishara hao wanyongwe ili watu walioajiliwa kwa kitendo cha kunyonga wasilipwe mishahara ya bure.

  Mbunge kijana kuliko wabunge wote kwa majimbo, Ferix Mkosamali (Muhambwe-NCCR Mageuzi), aliwataka wabunge kuigomea bajeti ya Wizara ya Sheria kuwa isipitishwe hadi itakapotoa majibu ya hakimu aliyetoa dhamana kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

  Kombani azomewa
  Kufuatia malalamiko kuhusu kuachiwa kwa raia hao huku Watanzania waliokamatwa nao wakiendelea kusota ndani, ilimuwia vigumu Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani ambaye hotuba yake ilibezwa na wabunge kwa makelele hakuna, hakuna, haiwezekani.
  Kombani alisimama na kutaka kutoa ufafanuzi juu ya kuachiwa huru wageni hao ndipo wabunge walianza kupiga makelele wakimbeza na kumfanya akae chini na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema aliingilia kati.

  "Ndugu wabunge, huu ni wakati wa kusema kweli, biashara hii ina fedha nyingi, inahitaji wenye moyo wa simba kushinda vishawishi, kwa kweli lazima tuwe makini sana,'' alisema Jaji Werema.

  Alisema kuwa tatizo lililofanya wageni hao kuachiwa kwa dhamana ni kutokana na upungufu makubwa ya sheria iliyopo kuhusu dawa hizo.Hata hivyo, alisema ofisi yake inafanya uchunguzi juu ya hakimu aliyewaachiwa wafanyabiashara hao ambapo alisema mwisho wa siku sheria itachukua mkondo wake.

  Hata hivyo, Werema alisema kuwa suala la kutenga adhabu ya kifo kwa wajumbe hao si la lelemama na akathibitisha uzoefu wake kuwa aliwahi kutoa adhabu ya kifo, lakini mwisho wa siku alijikuta akimwaga machozi kwa kuwa si rahisi kumhukumu mtu kifo.

  Kikosi kazi cha dawa wanena
  Wakitoa majumuisho ya maswali kutoka kwa wabunge, watoa mada hao walisema kuwa wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu huku wakikosa hata ulinzi licha ya kuwa wako katika vishawishi vikubwa.

  Nzowa alisema wamekuwa wakipata taabu kubwa licha ya mazingira ya kufanyia kazi kuwa ni magumu, lakini hawana hata chembe ya ulinzi wowote."Mimi natumia Zaburi ya 21 na ya 120 kwamba namtegemea Mungu tu maana kazi ni ngumu kweli…,'' alisema Nzowa.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 11. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Kanisa Katoliki laijibu serikali tuhuma za dawa za kulevya![/h]
  KANISA Katoliki nchini limesema haliridhishwi na utaratibu wa unaotumiwa na serikali kulituhumu kanisa hilo kuwa linajihusisha na biashara ya dawa za kulevywa.

  Kanisa limetoa kauli hiyo siku siku chache baada ya semina ya wabunge kuhusu athari za dawa za kulevya nchini iliyofanyika hivi karibuni mjini Dodoma. Semina hiyo ili kuwa ni ahadi ya serikali kutekeleza ahadi iliyoahidi kuhusu kuonesha mkanda wa video wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuonesha hadharani. Kanisa Katoliki nchini na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) yalikuwa miongoni mwa taasisi za dini ambazo zilitajwa kutumiwa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kufanya biashara ya dawa za kulevya.

  Taarifa iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Padri Anthony Makunde na kusambazwa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kanisa hilo linaamini kwamba biashara hiyo itakomeshwa iwapo wahusika wote, pasipo kujali wadhifa wao katika jamii, watakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria na si kwa malumbano na kauli zenye utata ambazo malengo yake yanatia shaka.

  "Tumepokea habari hizo kwa mshtuko mkubwa kwa kuzingatia hadhi na ushawishi ambao kanisa inao mbele ya jamii pamoja na maadili yanayofudishwa na kusimamiwa na taasisi hiyo. "Habari hizi zimelisikitisha na kulifadhaisha sana Kanisa Katoliki kwa vile, kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari kauli hiyo imetolewa katika semina ambayo sisi kama Taasisi hatukualikwa au kuwepo hivyo kushidwa kutoa maelezo juu ya shauri hili. Alisema kuwa kanisa hilo limeshangazwa na taarifa hizo kwa sababu halijawahi kudokezwa ama kushirikishwa juu ya suala hilo ili kutoa ufafanuzi na pengine ushirikiano iwapo ungehitajika.

  Ni kwa mantiki hiyo, Kanisa Katoliki linasubiri maelezo na taarifa rasmi kutoka mamlaka husika ili liweze kutoa ufafanuzi na pengine ushirikiano iwapo utahitajika.

  "Tukio lililotajwa katika magazeti ni Kongamano la Vijana lililofanyika huko Australia 2008. Katika tukio hilo ni kweli kwamba Baraza la Maaskofu liliratibu safari ya vijana na walezi wao waliohudhuria Kongamano hilo. Kwa mujibu wa taarifa zetu, vijana na walezi waliopitia TEC walienda na kurudi wote. "Hatuna taarifa za vijana waliobaki Australia kutoka katika kundi la vijana ambao safari yao iliratibiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.

  "Hata hivyo inashangaza kuona kwamba safari iliyofanyika miaka mitatu iliyopita inanukuliwa katika siku hizi katika hali ambayo Kanisa Katoliki halijawahi kuulizwa, au kuamriwa na mamlaka husika kutoa taarifa zozote kuhusu kundi ambalo safari yao ya kwenda Australia iliratibiwa na Kanisa hili ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.Ilieleza kuwa hata hivyo mwaka huu kuanzia tarehe 16/8/2011 vijana wa Kitanzania wakiwa na walezi wao walikuwa Madrid- Hispania kwa Kongamano la aina hiyo. Kilele chake kimefanyika Agosti 21 mwaka huu kwa Ibada ya Misa iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Benedicto VI.

  "Ikumbukwe kuwa si mara ya kwanza Kanisa Katoliki kuratibu safari za Kiroho na Kichungaji kwa makundi mbali mbali ya waamini wake. Ziko safari za kwenda nchi Takatifu, Roma, Fatima, Lurdi na sehemu nyinginezo za Hija. "Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limekuwa ikiratibu safari hizo baada ya kujiridhisha kwamba wale wote wanaokwenda kushiriki katika Hija hizo wamefuata taratibu zilizowekwa kikanisa na kuridhika kwamba wanakwenda huko kwa lengo la kuhiji na si vinginevyo. "Kwa vile si sera ya Kanisa Katoliki kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, Kanisa Katoliki linaamini kwamba hata ikitokea kwamba mmoja wa mahujaji amebainika kujihusisha na biashara hiyo, atakuwa amefanya hivyo kama mtu binafsi na si kwa jina ama kwa niaba ya Kanisa.

  "Kanisa linaunga mkono harakati zote za serikali na watu wote wenye mapenzi mema za kupiga vita biashara hiyo haramu. Hata hivyo taarifa ilisema kanisa halitaunga mkono kauli za jumla jumla zinazotolewa na baadhi ya watu kuhusu dawa za kulevya ambazo pengine zinatia shaka iwapo lengo lake ni kweli kupiga vita dawa za kulevya ama kulichafua, kulidhalilisha na kulipotezea hadhi na mvuto lililonao mbele ya jamii.

  Chanzo: Majira
   
 12. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Mbona bado tuombeni uhai 2taona mengi
   
 13. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Rais Kikwete: Viongozi wa dini acheni biashara dawa za kulevya

  Written by mwidady // 14/10/2011 // Habari // 5 Comments

  Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Mhashamu John Ndimbo, askofu mpya wa Jimbo katoliki Mbinga wakati wa ibada ya kumsimika askofu huyo iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Kilian mjini Mbinga leo.

  Rais Jakaya Kikwete amepasua jipu mbele ya viongozi wa dini kwamba kuna baadhi yao wanashiriki biashara haramu ya dawa za kulevya.
  Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga jana katika ibada maalum ya kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo wa jimbo hilo, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Killian, Rais Kikwete aliwataka viongozi hao kuacha biashara hiyo na badala yake washirikiane na viongozi wa serikali katika kuidhibiti.

  Katika ibada hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Kikwete, alisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara hiyo kwa kuwafanyia mipango vijana ya kuwatafutia hati za kusafiria kwenda nchi za nje kwa shughuli hiyo.
  Rais Kikwete aliwataka viongozi hao kukemea biashara hiyo na kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya dola ili kuikomesha kwa kuwafichua wahusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.

  " Inasikitisha sana na kutisha; biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, Taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili, baadhi yenu tumewakamata," alisema Kikwete na kuongeza kuwa:

  " Kauli zenu kemeeni jambo hili kwa kuelimisha jamii hususani vijana waweze kuepukana na matumizi ya dawa za kulevya."
  Aliyaomba madhehebu ya dini katika mipango yao ya maendeleo yaweke kipaumbele kujenga vyuo vya ufundi stadi ili kuisaidia jamii katika ushindani wa soko la ajira.

  Alifafanua kuwa kutokana na wananchi wengi kukabiliwa na tatizo la ajira, ni vyema sasa serikali kwa kushirikiana na madhehebu ya dini kujikita zaidi katika kujenga vyuo hivyo ambavyo vitasaidia kupunguza kero hiyo.

  " Kufanikiwa kwa viongozi wa dini katika shughuli za kimaendeleo ni faraja kwa serikali iliyopo madarakani na Watanzania wote kwa ujumla, " alisema.

  Kwa upande wake, Rais wa Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki Tanzania, Askofu Yuda Thadei Rwaichi, aliiomba serikali kuwa makini wakati wa kuandaa bajeti ya nchi.

  Askofu Rwaichi, alisema bajeti hiyo ni vyema izingatie maendeleo ya Watanzania ambao wengi ni maskini.
  Pia aliitaka serikali kudumisha amani na utulivu, kwa kuhakikisha vitendo vya vurugu havipewi nafasi na kwamba kanisa Katoliki litaendelea kushirikiana na serikali na Watanzania wote bila ubaguzi wa rangi, dini au kabila.

  Pamoja na mambo mengine, Askofu mpya wa Jimbo la Mbinga, Ndimbo, baada ya kusimikwa alitoa shukurani zake kwa Rais Kikwete na waumini wa jimbo hilo kuwa katika uongozi wake atakuwa bega kwa bega kuhakikisha anashirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

  Hata hivyo, Askofu Ndimbo, alisema kazi yake kubwa ni ya kuwachunga kondoo wa Mungu (Waumini) na kuwahamasisha waumini wa jimbo hilo kujikita katika kilimo cha kisasa ambacho kitawasaidia kupunguza ukali wa maisha.

  CHANZO: NIPASHE
   
 14. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Pengo amtolea uvivu Kikwete[/h]
  Fredy Azzah na Ibrahim Yamola

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema Watanzania wanasherehekea miaka 50 ya uhuru huku kukiwa na makundi ya viongozi na vigogo nchini wanaojineemesha kupitia migongo ya wananchi bila kujali wanawasaliti, wanawaongezea umaskini na kuwaua.

  Kardinali Pendo alilaani akisema: "hayo yamekuwa yakitendeka kinyume na misingi iliyoainishwa na waasisi wa taifa wakati wakidai uhuru kutoka kwa wakoloni ambapo walitamani kujenga Tanzania yenye utukufu.

  Kardnali Pengo alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akiongoza ibada ya maadhimisho ya miaka 50 ya Tanzania, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme Parokia ya Tabata.

  "Waasisi wetu walipokuwa wanapigania uhuru wa taifa hili, lengo na maono yao yalikuwa kutengeneza taifa lenye utukufu, lenye kutawala mataifa mengine …," alisema Kardinali Pengo na kuongeza:

  "Katika miaka 50 tunayoikamilisha, kumekuwa na mafanikio na changamoto nyingi tu, inabidi tujipange ili watakao kuja kuadhimisha miaka 100, au hata miaka 25 ijayo wasije wakasema afadhali wakati wa mkoloni."

  Katika ibada hiyo ambayo pia ilitumika kuliombea taifa, Pengo alisema wakati wa kupigania uhuru lengo ilikuwa ni kulifanya sehemu salama na bora ya kuishi watu wake.

  Kardnali Pengo alitahadharisha akisema: "Lakini sasa Taifa lina makundi ya watu wasaliti, wenye ubinafsi na ambao wako tayari kujitafutia utukufu hata ikibidi kuwakandamiza na kuwaua wenzao".

  Kwa sababu hiyo akawataka Watanzania kutafakari katika kipindi hiki cha kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, wajiulize wamekuwa wakijitafutia utukufu binafsi au ule ulioasisiwa na taifa wa wananchi wote kufaidi matunda yake.

  Kwamba, tumepata utukufu wa aina gani?" Alisema Kardinali Pengo na kuonya; "Baadhi ya watu wanapata utukufu bila hata kujali kama watu wengine wanakufa, jambo ambalo ni hatari kwa taifa."

  Kardinali Pengo aliwaonya waliopewa dhamana ya uongozi na kutumia nafasi hiyo kujitajirisha, kuwa ni usaliti kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla.

  Tuhuma za dawa za kulevya
  Katika hatua nyingine, Kadinali Pengo, alilaumu mtindo wa viongozi wa Serikali na dola kutotaja hadharani majina ya watu wanaowatuhumu kuhusika na biashara ya dawa za kulevya huku wakiendelea kulalamika kuwa wapo na wamewakamata.
  Alisema hali hiyo haionyeshi nia yao ya dhati katika kupambana na biashara hiyo haramu.

  Akikumbushia kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete wakati wa Sikukuu ya kumwekwa wakfu na kumsimika Mhashamu Askofu John Ndimbo kuwa Askofu wa Jimbo la Mbinga kuwa baadhi ya viongozi wa dini huuza dawa za kulevya, alisema alitakiwa kuwataja.

  Kardinali Pengo alisema kitendo cha Rais Kikwete pamoja na baadhi ya viongozi waliojitokeza kuzungumzia suala hilo huku wakisema hawawezi kuwataja kwa majina, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa.

  "Haiwezekani mtu mkubwa tu, wala siyo mdogo kuja katika eneo la Kanisa la Katoliki, kukiwa kumejaa Maaskofu kutoka karibu nchi nzima, unasema maneno haya halafu unasema, siyo nyie ni viongozi wa makanisa madogomadogo," alilalamika Kardinali Pengo.

  Aliongeza kwamba: "Kama ndivyo hivyo kwa nini sasa uje kuyasema maneno hayo katika eneo la Kanisa Katoliki."

  Akasisitiza: "Mapadri, watawa; naomba tujiangalie kama sisi tunaguswa na hii kauli, kama haitugusi tumshukuru Mungu, lakini ni vyema hawa watu wakatajwa.

  Hata kama ni mimi njoo uniambie, ukisema hunitaji kwa sababu ni kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa."

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, William Lukuvi, aliwahi kuliambia Bunge hivi karibuni kuwa Serikali ina safari ndefu katika kufanikisha mkakati wa kukomesha biashara hiyo haramu.

  Alisema Serikali inaamini kuwa vita ya kuwakamata wanaojihusisha na dawa za kulevya ni ngumu lakini akasisitiza kuwa anaamini mwishowe watashinda uhalifu huo.

  Lukuvi alisema mbali na kuwataja hadharani baadhi ya viongozi wa dini, imebainika kuwa wana mtandao mkubwa.

  "Hapa sio kuwataja tu maana kama ni kuwataja tayari Serikali ilikwisha wataja na watu wanajua kuwa kiongozi wao ni yule Askofu wa Nigeria, lakini hapa suala ni namna ya kupambana na kuwajua wengine,'' alisema Lukuvi.

  Hata hivyo, mara baada ya Rais Kikwete kutoa kauli hiyo, Jumuia ya Kikristo Tanzania (CCT), ilikuja juu na kumpa saa 48 za kuwataja hadharani viongozi wa madhehebu ya dini wanaohusika na biashara hiyo haramu.

  "Rais ataje majina ni kina nani wanahusika na ndani ya saa 48 awe ameyataja la sivyo itakuwa ni aibu zaidi kwake na Serikali," alisema Makamu Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Valentino Mokiwa.

  Rais Kikwete alijibu wito huo kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwamba, viongozi wa dini siyo malaika kwa hivyo wasijivune kuwa hakuna miongoni mwao ambao ni wahalifu.

  Source: Gazeti la Mwananchi
   
 15. J

  Jonathan Kiula JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  thanx for telling the source
   
 16. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  illegal money ndo mana wanafikia hatua ya kutia kiburi mbele ya serikali mana wanakula wote.
   
 17. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #17
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  blood money
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Nov 12, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Au ndo kujibu mapigo ya sherehe zinazoendelea Mwanza leo! This is the moment which we must seize!
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Akili ni nywele kila mtu na zake.
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  You are very correct na sina la zaidi
   
Loading...