Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Sifa kubwa ya sisi watanzani(sio wote) ni kutumia muda mwingi na nguvu nyingi katika kulalamika huku tukitumia muda mchache na nguvu kidogo katika kupambana na chanzo /vyanzo vya malalamiko yetu.
Kwa mfano,leo hii kilio kikubwa cha watanzania wengi kuanzia wasomi, wanasiasa,wanaharakati,viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla,ni kupatikana kwa katiba mpya itakayokidhi mahitaji ya wakati tulionao leo.
Hata hivyo,ni bahati mbaya sana kuona tunatumia muda mwingi na nguvu nyingi kulalamikia matatizo yanayotokana na katiba hii ya sasa huku tukitumia muda kidogo,juhudi kidogo na nguvu kidogo kudai upatikana wa katiba mpya.
Kwa kasumba na tabia yetu ile ile,hivi sasa tunatumia muda mwingi na nguvu nyingi kuchambua ripoti ya CAG na kulalamikia madudu yaliyoibuliwa katika hiyo ripoti huku tukitumia muda mchache na nguvu kidogo kuhakikisha huyu CAG anapewa meno ya kisheria ya kuweza kuchukuta hatua pale inapobidi na tunasahau ripoti hizi kila mwaka huwa zinasheheni madudu chungu nzima.
Labda tujiulize,hivi sisi watanzania tunawaza sawa sawa?
Je,tunajipanga vipi kuhakikisha madudu haya hayajirudii?
Hivi mwakani ripoti ikitoka na ikawa mbaya kuliko hii ya sasa,tukiendelea kulalamika tutakuwa ni watu tunaowaza sawa sawa?
Mfano.Tumesikia wakati fulani(taarifa zisizo rasimi) kuwa bajeti ya CAG ilikuwa imeminywa na kuwa kikwazo katika utendaji wake.
Binafsi najiuliza,kama kweli Bajeti yake iliminywa,tunachukua hatua gani ili kuondoa tatizo hili?
Je,tunasubiri iminywe tena ili tuendelee kulalamika na kulaumu?
Binafsi kwa kutambua kazi nzuri ya CAG na ili kumuwesha afanye kazi zake kwa ufanisi zaidi na bila kutegemea fedha kutoka serikalini, nilishauri kupitia hapa JamiiForums kuwa sheria inayounda ofisi ya CAG ifanyiwe marekebisho na kumuwezesha CAG awe anapata fedha za kuendeshea ofisi yake moja kwa moja kwa kupitia tozo maalumu itakayotozwa kutoka kwenye baadhi ya biashara au huduma zitakazooneka zinafaa kama ilivyo kwa Ewura, REA,n.k. na si kusubiri mafungu kutoka serikali na hii ni kutokona na umuhimu wa chombo hiki kwa umma.
Vile vile namshauri CAG nae atoe mapendekezo ya aina hii kwa serikali na hata kwa kamati husika za Bunge na kwa kufanya hivyo atakuwa ametimiza wajibu wake na kunawa mikono.
Niwaambie tu bila kumpa meno ya kisheria CAG,mwaka huu tutajadili ripotI yake kwa mihemuko na mwakani yatajirudia haya haya na tena yanaweza hata kuzidi.
Albert Einsteni aliwahi sema: "insanity is doing the same thing over and over again and expecting different results."
Tujiuluze kama hii definition by Albert Einstein haituhusu.