Mdhamini: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA,Tundu Lissu amepona ila anaogopa kurudi nchini kwa kuhofia maisha yake

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,902
141,842
Mahakama ya Kisutu imesisitiza kuwa inamtaka Mahakamani aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi.

Hata hivyo, Lissu ameieleza Mahakama kupitia Mdhamini wake Ibrahim Ahmed kuwa anahitaji kurejea ila bado anahofia usalama wake, kesi imeahirishwa hadi Januari 20,2020.

Novemba 21, 2019 Mahakama hiyo iliwataka wadhamini wa mwanasheria mkuu huyo wa Chadema kuhakikisha wanampeleka mahakamani ili kesi ya msingi iendelee.

Katika maelezo yake mahakamani, Ahmed amedai alifanya utaratibu kama alivyoelezwa na Mahakama, alipomfikishia mteja wake agizo hilo alijibiwa kuwa anatamani kurejea nchini lakini ana hofu na usalama wake.

Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto amedai upande wa mashtaka umeshindwa kuleta mashahidi kutokana na mshtakiwa wa nne kutokuwepo.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba alimsisitiza mdhamini huyo kuhakikisha Lissu anafika mahakamani kwa kuwa taratibu za dhamana zinaeleweka.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 20, 2020.
 
Wakili wa mh Tundu Lisu katika kesi inayomkabili katika mahakama ya kisutu amemueleza hakimu anayesikiliza shauri hilo kuwa mteja wake ameshapona ila anaogopa kurudi nchini kwa kuhofia usalama wake.

Source ITV habari!

Aseme ukweli tu anaogopa kupoteza haki yake ya ukimbizi hivyo atapoteza mafao yake kule Belgium. hata alipokuja oops aliposafiri kwenda Kenya alifahamu fika kwamba angekanyaga Tanzania na ukimbizi wake ungekuwa historia.
 
Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba alimsisitiza mdhamini huyo kuhakikisha Lissu anafika mahakamani kwa kuwa taratibu za dhamana zinaeleweka.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 20, 2020.

Naamini Hakimu Simba anatakiwa ajue kuwa kwa issue kama hii, busara inatakiwa itumike na sio kusisitiza taratibu. Lissu hakuondoka hapa nchini kwa njia za kawaida, si tu alikuwa mahututi bali usalama wake ulikuwa na mashaka makubwa (hata kama wabaya wake wanakataa kuliona hilo).

Sioni mdhamini atahakikishaje uwepo wa Lissu mahakamani kama usalama wa Lissu bado ni issue unless wakamteke huko aliko.

Bila busara kutumika hakimu anaweza kumfanyia mdhamini kitu mbaya kwa kitu ambacho kiko nje ya uwezo wa mdhamini, vinginevyo mahakama imhakikishie Lissu usalama wake.
 
Kwa sasa asiwe na wasiwasi tena. - MWENYEKITI tumeshamchagua.
Tishio halipo tena,
Arudi tu, USALAMA UPO!
 
Aseme ukweli tu anaogopa kupoteza haki yake ya ukimbizi hivyo atapoteza mafao yake kule Belgium. hata alipokuja oops aliposafiri kwenda Kenya alifahamu fika kwamba angekanyaga Tanzania na ukimbizi wake ungekuwa historia.
Muogopeni Mungu!!! Nani hajui kuwa Tundu Lissu akirejea tu anaweza akauliwa!!!!! Mungu yupo lakini na ni wa watu wote!!!
 
Muogopeni Mungu!!! Nani hajui kuwa Tundu Lissu akirejea tu anaweza akauliwa!!!!! Mungu yupo lakini na ni wa watu wote!!!
ataenda kukaa segerea chini ya ulinzi mkali hadi kesi yake itakapoisha, baada ya hapo anaweza amua kurudi ulaya akiona hali bado tete
 
Aseme ukweli tu anaogopa kupoteza haki yake ya ukimbizi hivyo atapoteza mafao yake kule Belgium. hata alipokuja oops aliposafiri kwenda Kenya alifahamu fika kwamba angekanyaga Tanzania na ukimbizi wake ungekuwa historia.
Siku nyingi sana nilikuwa nakataa sana kuwa kuna uchwai mpaka leo sijawai kuona uchawi unafanyika vipi kumbea matendo fulanifulani na maneno fulani ndio uchawi wenyewe aah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muogopeni Mungu!!! Nani hajui kuwa Tundu Lissu akirejea tu anaweza akauliwa!!!!! Mungu yupo lakini na ni wa watu wote!!!

Yaani wamuue yeye kwa kisa gani? Ndio umbeya wenyewe huo!
 
Back
Top Bottom