Mdhamini anaweza kufungwa mtuhumiwa akitoroka?

JMF

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
1,735
2,686
Hello wana JF,

Naombeni ufafanuzi wa kisheria juu ya swala hili: Endapo mtu amemdhamini mtu polisi ambae anashikiliwa kwa kesi ya utapeli au wizi wa kuaminika halafu akatoweka na asipatikane kwa zaidi ya miezi 6, 1) Mdhamini anaweza kuhukumiwa kwa kosa lake?
2) Je, naye anaweza kupewa dhamana awe huru aendelee kumtafuta mtuhumiwa aliyemdhamini?
3) Kuna ukomo wa muda wa kumtafuta mtuhumiwa?

Natanguliza shukrani zangu za dhati nikisubiria mchango wenu kutokana na uzoefu, mazoea na sheria inavyosema.

Ahsanteni.
 
Kufungwa au kulipa faini au gharama za uharibifu uliofanywa iko wazi endapo mtuhumiwa uliyemdhamini atachoropoka.
 
Mkuu pole sana, kama ni kesi utapeli we ndio utamlipa aliyemshtaki uliyemdhamini.

kuhusu kushtakiwa na kufungwa sijui.

maana umesema umemdhamini polisi na sio mahakamani. Jukumu lako mi kuhakikisha anapatokana ili sheria ichukue mkondo wake
 
Hello wana JF,

Naombeni ufafanuzi wa kisheria juu ya swala hili: Endapo mtu amemdhamini mtu polisi ambae anashikiliwa kwa kesi ya utapeli au wizi wa kuaminika halafu akatoweka na asipatikane kwa zaidi ya miezi 6, 1) Mdhamini anaweza kuhukumiwa kwa kosa lake?
2) Je? Nae anawezakupewa dhamana awe huru aendelee kumtafuta mtuhumiwa aliyemdhamini?
3) Kuna ukomo wa muda wa kumtafuta mtuhumiwa?

Natanguliza shukrani zangu za dhati nikisubiria mchango wenu kutokana na uzoefu, mazoea na sheria inavyosema.

Ahsanteni.
Mkuu hapo ni kwamba utapaswa kubeba jukumu la kulipa gharama zinazohitajika.

Kwa maana moja ya sharti la dhamani wakati wa kumdhamini mtuhumiwa ni kumdamini kwa dhamana ya kitu au pesa inayozidi kiwango kilichotajwa kwenye kesi husika.

Hivyo bhasi kwa vile wew ndio muweka dhamana bhas utapaswa kutoa ushirikiano ili kumaliza kesi hiyo kwa kulipa gharama zote zinazohitajika.

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom