Mdhamini anahitajika: Nina wazo la kutafsiri vitabu maarafu kutoka kingereza kwenda kiswahili..

Habarii
Sijui wazo langu ni lakijinga?? But nalileta kwenu kama mtaona linafaa..

First mm napenda sana sana kusoma vitabu vya aina yoyote bahati mbaya kila kitu ninachokisoma kipya hua natamani niwagawie wenzangu yale niliyoyapata kwenye kusoma... ndio maaana nikipata kitu kipya hua nashea nanyi humu.

SASA IPO HIVI.

Ninawazo kwamba niwe natafsiri vitabu vinavyouzika sana kimataifa kwenda lugha ya kiswahili. Imagine unasoma kitabu cha The Davinci Code kwa kiswahili au Rich Dad poor dad kwa kiswahili na vinginevyo kwa lugha yetu adhimu ya kibantu. Itapendeza na inavutia kisi chake

Hivyo nilitaka apatikane mtu atakaye fund hili wazo langu kama ataona lina faa kwakua napenda kusoma na kuandika suala hili la kuandika nitalifanya mwenyewe.. kushinda kutwa nzima hadi usiku nikiwa naandika ni kazi ndogo kwangu.
Faida yake hii ni nini??
1. Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitabu hasa vya kingereza hivyo vitabu vikiwa kwenye lugha yetu itakua rahisi kidogo.
2. Tutaongeza idadi ya watanzania wenye kujisomea vitabu kuliko kutazama tamthilia za Sultan
3. Tutaongeza maalifa kwa vijana wanaopenda kujisomea ikumbukwe elimu na utajili wote umefichwa kwenye vitabu..

• Lakini pia watz ni wavivu kusoma hivyo kwa wale wavivu tungewatengenezea mfumo ambao kitabu anakipata chote kizima kwa mfumo wa Audio katika lugha ya Kiswahili hata mtu akiwa safari anavaa earphones anasikiliza kitabu hadi anfika kwao vijijini huko kutembea.

Swala la Copyright na Marketing ya hivyo vitabu sijalifikiria sana coz bado sijajua kama litafanikiwa but kama mtu atavutiwa na wazo langu atanifuata pm tupange kisha nimpe mikakati ya soko la hivyo vitabu.
Samahini kwa wote nilio wakwaza kwa wazo langu hili la kijinga
Ahsanteni
~Da'Vinci...

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
Mkuu wazo nmelikubari maana ni mpenzi mzuri na msomaji wa vitabu nicheck whatssap +27784696692

Sent using Jamii Forums mobile app
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom