Mdhamini anahitajika: Nina wazo la kutafsiri vitabu maarafu kutoka kingereza kwenda kiswahili..

Haki miliki ndo jambo la kwanza, kisha huyo mtu mwenye haki za kitabu akubali urudufu kazi yake,

Wala hata wadhamini hutawahitaji mana utalipwa na wenye haki miliki kisha wao watauza kwetu....
Other wise uwalipe mabilioni ya pesa ili wakupe haki zote kwa lugha yako unayoitaka kitabu chake kiwe...
Kikubwa utakubaliwa na wenyewe endapo wanauhakika hautovuruga maana ya kitabu chao
Noted

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapatikana wapi Mkuu?
Habarii
Sijui wazo langu ni lakijinga?? But nalileta kwenu kama mtaona linafaa..

First mm napenda sana sana kusoma vitabu vya aina yoyote bahati mbaya kila kitu ninachokisoma kipya hua natamani niwagawie wenzangu yale niliyoyapata kwenye kusoma... ndio maaana nikipata kitu kipya hua nashea nanyi humu.

SASA IPO HIVI.

Ninawazo kwamba niwe natafsiri vitabu vinavyouzika sana kimataifa kwenda lugha ya kiswahili. Imagine unasoma kitabu cha The Davinci Code kwa kiswahili au Rich Dad poor dad kwa kiswahili na vinginevyo kwa lugha yetu adhimu ya kibantu. Itapendeza na inavutia kisi chake

Hivyo nilitaka apatikane mtu atakaye fund hili wazo langu kama ataona lina faa kwakua napenda kusoma na kuandika suala hili la kuandika nitalifanya mwenyewe.. kushinda kutwa nzima hadi usiku nikiwa naandika ni kazi ndogo kwangu.
Faida yake hii ni nini??
1. Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitabu hasa vya kingereza hivyo vitabu vikiwa kwenye lugha yetu itakua rahisi kidogo.
2. Tutaongeza idadi ya watanzania wenye kujisomea vitabu kuliko kutazama tamthilia za Sultan
3. Tutaongeza maalifa kwa vijana wanaopenda kujisomea ikumbukwe elimu na utajili wote umefichwa kwenye vitabu..

• Lakini pia watz ni wavivu kusoma hivyo kwa wale wavivu tungewatengenezea mfumo ambao kitabu anakipata chote kizima kwa mfumo wa Audio katika lugha ya Kiswahili hata mtu akiwa safari anavaa earphones anasikiliza kitabu hadi anfika kwao vijijini huko kutembea.

Swala la Copyright na Marketing ya hivyo vitabu sijalifikiria sana coz bado sijajua kama litafanikiwa but kama mtu atavutiwa na wazo langu atanifuata pm tupange kisha nimpe mikakati ya soko la hivyo vitabu.
Samahini kwa wote nilio wakwaza kwa wazo langu hili la kijinga
Ahsanteni
~Da'Vinci...

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana nahitaji mdhamini au shareholder ambae atafund wazo langu coz vitendea kazi siwez kupata... Mfano mada zangu humu hua nakaa na wazo karibia miezi 6 kuandika inanichukua wiki kadhaa ili kuandika kilicho thabiti.. hiyo yote kutokana na uhaba wa vitendea kazi

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
Kwa hesabu yako linaweza kugharimu kiasi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifupi ni kuwa
Wewe kutafuta mdhamini ambae hana haki na kitabu mnachotaka kurudufu ni kujisumbua (japo ni wazo zuri).

Itahitajika pesa nyingi sana ili kununua haki za kitabu husika na hapo suala linakuja Kwenye marketing ya lugha husika,...
Mfano: Umenunua haki nusu kwa billion moja (pesa ndogo zaidi kwa makadirio)
Je hapa kwetu kwa lugha yetu utauza kopi ngapi na kwa sh ngapi ili urudishe pesa yote na faida?

Kwa wenzetu vitabu ni biashara nzuri sana na huwez kuta kitabu cha chini ya dola mia(labda vya hapa Africa)

Cha kukusaidia sana labda urudufu kiswahili kwenda kingereza au kifaransa, mana ni rahisi kununua haki ya kitabu cha kiswahili kuliko ulichofikiria,na ni rahisi kupata faida kubwa kwa kurudufu kutoka kiswahili kwenda kingereza...

Ni maoni yangu ngoja tuone wengine
Nadhani mpaka hapa atakuwa ameelewa. Umeeleza kwa kinaga ubaga mkuu. Umeeleweka sana. Nafikiri hata wazo lenyewe la kudurufia linaishia hapa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado sijapiga hesabu ila nikipata mtu tutakaa tupige hesabu

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
Mkuu Da'Vinci ni vizuri sana kwa kuanzia fuata ushauri wa *Kudo* na *Sir Khan*. Mimi no mpenzi mkubwa wa vitabu hasa vya kipelelezi na ujasusi,na biashara pia,ningekuwa tayari tuishie kazini,ila Vinginevyo unaweza kupoteza hela zako na kushitakiwa,ukitaka kudurufu labda kwa kificho. Mawazo yao nimeyaelewa sana,ni vizuri na wewe uyasome kwa makini muda mwingine unaweza usihitaji mdhamini,wadhamini wanaweza kuwa wao wenye kitabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom