Mdhambi anapotakiwa kutubu pasipo toba

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,771
7,138
Wana JF,

Uenda hii ni wiki ya ya mkorogano baada ya mkuu wa nchi kuwapa marungu ya kuponda vichwa maji wasiojielewa na wasioelewa kwa nini wamejikuta hawana ajira. Mtu asiye na ajira uonekana ni mdhambi na mwovu kwani uonekana kwa watu kuwa ajishighulishi na lolote, nchi hii imebana sana kiasi kwamba ukianzisha chochote kama fursa , kinavamiwa na kinaonekana hakina maana tena. Pool table ni mchezo wa akili uliobuniwa na wabunifu kwa ajiri ya ajira, lakini kwa tanzania ni kichaka cha wahuni, hili ni sahihi kabisa kwani kwa sasa sio mchezo tena wa kutegemea kutoa watu wa vipaji kwa ajili ya mashindano bali umegeuzwa mchezo wa kamali ambayo kwa upande mwingine inafilisi watu.

Pamoja na hayo serikali isikimbilie tu kuona hawa vijana ni wadhambi , Rais kasema wenye ajira ni takribani laki tano. Kwa nini amerudia mchezo ule ule wa kuteua wazee waliokwisha staafu au kuwa na umri wa kustaafu. Kama yeye alivyomuona Makonda aliyepewa ukuu wa wilaya kwa majaribio na akafaulu kwa kiasi kikubwa na kuwa kipenzi cha watu, kwa nini asitafute wengine wenye mafanikio kama haya ambao wana vision, tumeona makonda anavyojitahidi kuwa mbunifu wa vitu mbali mbali ambavyo wengi wameshindwa, Je, kuwarudisha hawa wazee walioshindwa ubunge, waliochokwa mikoani haoni kwamba nafasi za vijana zinazidi kuwa finyu. Wale wote waliokwisha kustaafu ubunge, Majeshi ndio wanatakiwa kwenda vijijini kuanzisha vikundi vya maendeleo kwa kutumia fedha zao walizopewa baada ya kustaafu.

Mstaafu mmoja ambaye nimemsifu ni Kamanda Alfred Tibaigana ambaye aliamua kustaafu na kuondoka mjini kuanzisha kilimo cha migomba aina ya fia, kwa sasa ametengeneza ajira nyingi , na anazalisha mbegu bora za migomba hiyo, hadi amekuwa tegemeo kwa wale ambao wanataka kilimo hicho. Mfano kuna wabunge wengi ambao wakiwa bungeni wanalia na kilimo kwanza kinavo feli, kwanini wanaendelea kupewa vyeo badala ya kwenda kukifanyia kazi kilimo vijijini.

Mkuu wa nchi benki zetu ndio mufilisi kabisa, vijana tunaogopa kukopa kwa sababu hatujalengwa, uwezi kutuambia tuwe na viwanja wakati serikali inaanza kupima viwanja inaviuza kwa mamilioni, na ikimaliza kupima tu , kunatokea wajanja wanachukua viwanja vyote sisi tunabaki kuliwa na fedha za form, form inacost Tshs mia Tano kuchapishwa lakini tunaliwa tshs.30,000/= kumbe viwanja vina wenyewe.

Sitetei ujinga wa kukaa vijiweni ila serikali ipitie upya mipango ya kuendeleza vijana. Mfano mzuri, vijana walipojiajiri kwa bodaboda waharifu wakajipenyeza biashara hii ikaonekana hovu, lakini taarifa za kipolisi waarifu wote wanajulikana ila hawafanyiwi kazi. Hapo zamani kulikuwepo mkakati wa kumaliza tatizo la wizi, watu walikuwa wanafanya mikutano wanapiga kura za siri kwenye kapu wanaweka orodha ya waharifu baadaye wanafanyiwa uchunguzi kujiridhisha kuondoa uonevu, leo hii jirani wa chumba chako haumjui jina, kwa barozi anakujua siku akitaka kuweka fedha benki. Inabidi kurudisha utaratibuwa zamani wa Mwl Nyerere wa nyumba kumi kumi kutambuana hata tatizo la watu kukaa bure vijiweni litaisha.
 
Back
Top Bottom