Mdeni wangu kanilipa asilimia 78 ya deni langu, mda bado ila kaanza kusua sua kumalizia deni je naweza kurudi tena mahakamani

Oct 16, 2016
34
10
Ninamdeni wangu nilikuwa namdai nikamua mpeleka mahakamani ili anilipe deni langu tukakubaliana kimandishi mbele ya hakimu kuwa atanilipa deni langu ndani ya mwaka mmoja

Kweli kipindi cha marejesho mdeni wangu amekuwa akilipa deni lakini tangu awali analipa mwezi wa kwanza alilipa kiwango chini ya ambacho tulikubaliana mahakamani, hilo halikunipa wasi wasi kalipa hivyo hivyo ndani ya miiezi kumi na moja huu sasa ni mwezi wa mwisho ambao inatakiwa amalize deni lake, lakini mpaka sasa kanilipa asilimia 78 ya deni lote

Nikimuuliza vipi anasema tarehe ya mwisho wa deni hili atamalizia hizo asilimia 22 zote sasa nimekuwa na wasi pengine asimalizie maana tarehe ya kulipa mwezi uliopita akunipa nauliza naweza kurudi tena mahakamani kutoa taarifa kuwa mdaiwa wangu kashindwa nilipa deni langu nishike Mali yake

Naomba msaada nisije kwenda mahakamani nikaharibu mambo maana mdaiwa lengo la kulipa naona analo ila hana pesa sema miye naitaji hiyo pesa kwa haraka sasa je naweza shika Mali yake na ili anilipe maana Mali za kushika zipo nikishika anaweza nilipa

Sasa na wasi wasi mahakama kama unaweza kataa kushika Mali zake maana kanilipa asilimia 78 na tarehe ya mwisho bado kufika ebu nisaidieni hapo
 
We kiazi 78% plus hiyo 32%.. ina maana una mdai 110%???
Muhimu mkuu amekulipa above 50%

Sent using Jamii Forums mobile app
Makosa ya kiuandishi kiongozi niwie radhi nimerekebisha,

Hapo umesema muhimu kalipa asilimia 50 je mahakama inaweza nigomea kushika Mali yake kisa kavuka asilimia 50 naomba msaada wako, maana nohofia kurudi mahakamani mdaiwa akasema kabanwa na majukumu apunguziwe kiwango cha marejesho ikala kwangu ndio maana nipo hapa jamvini kupata ushauri wa kitaalamu kuwa niendelee naye bana hivi hivi uku ananilipa kidogo kidogo au nirudi mahakamani
 
Back
Top Bottom