MDEE: Watake, wasitake Wataachia tu

Zapa RadioFm

Senior Member
Feb 12, 2016
112
171
HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe amesema, hekaheka zinazofanywa na Serikali, Jeshi la Polisi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi yao ni kutaka kutwaa Umeya wa Jiji la Dar es Salaam lakini wataachia, anaandika Faki Sosi.

“Watake wasitake wataachia, hapa ni Ukawa tu. Yote haya yana mwisho lakini wajue kuwa namba ‘zinatufeva’ na si vinginevyo,” amesema Mdee.

Mdee, Mwita Waitara ambaye ni Mbunge wa Ukonga na washitakiwa wengine watatu leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu na kisha kuachwa kwa dhamana.

Washitakiwa hao wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumjeruhi Terresia Mmbando ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika Jumamosi wiki iliyopita na baadaye kuhairishwa na kuibua malumbano ya kisiasa.

Washitakiwa wengine kwenye tuhuma hizo ni Shafii Juma, Alfonce Kinyafu, Manase John pamoja na Diwani wa Kimara Stop-Over ambapo kila mmoja amejidhamini mwenyewe kwa Sh. 2,000,000.

Mawakili wa wanasiasa hao ni Peter Kibatala, John Malya, Omari Msemo na Fredrick Kiwelo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mdee amesema, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imedai kuwa, hakukuwa na sababu ya kuwakamata isipokuwa ni amri kutoka kwa viongozi wao.

Mdee amesema, jeshi hilo linaendeshwa kinyume cha sheria na kwa matakwa ya wanasiasa na watawala.
“Rais John Magufuli atake asitake ni lazima ataongozwa na Ukawa kwenye Jiji la Dar es Salaam na uchaguzi huu ni lazima Ukawa itashinda kwasababu namba haziwezi kubadilika,” amesema.

Amesema, mahakama imeweka wazi zuio la uchaguzi wa uchaguzi walilopeleka CCM sio halali na kwamba, (CCM) walikua wanatafuta njia ya kuiba kura katika uchaguzi huo.

Waitala ambaye ni Mbunge wa Ukonga amesema hatishwi na kuwekwa rumande na kwamba, wao kuwekwa huko ni sawa na simu iliyoisha chaji na kuchajiwa upya.

“Msimamo umeongezeka, wasimamizi wajipange kwani ukweli upo wazi sasa hakuna figisu,” amesema.
Wafuasi wa Chadema waliofika mahakamani hapo walishangilia kupewa dhamana kwa viongozi wao huku wakiimba ‘Peoples Power.’

Salum Mwalimu, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema amewapongeza watuhumiwa hao na kusema kuwa, hiyo ni moja ya changamoto za ukombozi.

“Tayari tumesikia kuwa wanabuni mbinu mpya ya kuwakamata madiwani ili kuitisha uchaguzi kwa kushtukiza,” amesema.
Mwalimu amesema, chama hicho kimepoteza wanachama wengi kwa kuuawa na wengine wamesingiziwa kesi hatimaye kufungwa.

Kesi hiyo iliyo chini ya Hakimu Mfawithi Mwanaamina Kumbakono, imepangwa kusikilizwa tena tarehe 16 Machi mwaka huu.
 
Ina maana intelijensia ya polisi hawamuiangalia ile video iliyopigwa itv na media nyinginezo ili kuona uhusika wa mtuhumiwa kupigwa? Kama kweli alipigwa aliripoti polisi na hospitali kwa wakati au ni mazingira ya kutengeneza ili kutafuta ile cheapest popularity? Sikumtegemea huyo ras wa dar kufanya fyongo la kipuuzi hivi. Na wanaoongozwa nae watakuwa wanapata taabu kweli kwani upstair yake ni tabularasa completely. Ajiuzulu tu hiyo nafasi kwani hawa ukawa watamtumbua vibaya.
 
Ifikie mahala magufuli awambie ccm waache kuitia doa serikali yake,ni swala lisilo pingika kwamba meya wa jiji anapaswa kutokana na Ukawa.
Kama Kweli serikali hii ni ya magufuli sio ccm basi waache kuitia doa serikali Kwa mbinu chafu,na za kizamani.
 
Mkuu hata maccm hayafai kabisa na hayakubaliki
 
Nilikuwa na Imani na Serikali ya Magufuli lakini katika hili ni wapumbavu na upumbavu mkubwa na sina tena Imani naye kwenye suala la demokrasia ya vyama vingi.
Mkuu kuielewa ccm inaitaji uwe na PhD ya upumbavu na ubabaishaji ndio utawaelewa hiki chama cha machafuko
 
Dah sikukosea njia kuwa chadema with smart people nakupenda saba cdm nakupenda ukawa
 
kwa ccm kushindwa kwao ni dhambi kubwa sana. kuna ushirikiano wenye mashaka kati ya jeshi la polis na ccm. ni vizuri magu akajifunza kuheshimu sheria na maamuzi ya umma. kwa wakati huu wananchi wa dar es salaam wameamua waongozwe na meya toka ukawa.
 
HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe amesema, hekaheka zinazofanywa na Serikali, Jeshi la Polisi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi yao ni kutaka kutwaa Umeya wa Jiji la Dar es Salaam lakini wataachia, anaandika Faki Sosi.

“Watake wasitake wataachia, hapa ni Ukawa tu. Yote haya yana mwisho lakini wajue kuwa namba ‘zinatufeva’ na si vinginevyo,” amesema Mdee.

Mdee, Mwita Waitara ambaye ni Mbunge wa Ukonga na washitakiwa wengine watatu leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu na kisha kuachwa kwa dhamana.

Washitakiwa hao wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumjeruhi Terresia Mmbando ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika Jumamosi wiki iliyopita na baadaye kuhairishwa na kuibua malumbano ya kisiasa.

Washitakiwa wengine kwenye tuhuma hizo ni Shafii Juma, Alfonce Kinyafu, Manase John pamoja na Diwani wa Kimara Stop-Over ambapo kila mmoja amejidhamini mwenyewe kwa Sh. 2,000,000.

Mawakili wa wanasiasa hao ni Peter Kibatala, John Malya, Omari Msemo na Fredrick Kiwelo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mdee amesema, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imedai kuwa, hakukuwa na sababu ya kuwakamata isipokuwa ni amri kutoka kwa viongozi wao.

Mdee amesema, jeshi hilo linaendeshwa kinyume cha sheria na kwa matakwa ya wanasiasa na watawala.
“Rais John Magufuli atake asitake ni lazima ataongozwa na Ukawa kwenye Jiji la Dar es Salaam na uchaguzi huu ni lazima Ukawa itashinda kwasababu namba haziwezi kubadilika,” amesema.

Amesema, mahakama imeweka wazi zuio la uchaguzi wa uchaguzi walilopeleka CCM sio halali na kwamba, (CCM) walikua wanatafuta njia ya kuiba kura katika uchaguzi huo.

Waitala ambaye ni Mbunge wa Ukonga amesema hatishwi na kuwekwa rumande na kwamba, wao kuwekwa huko ni sawa na simu iliyoisha chaji na kuchajiwa upya.

“Msimamo umeongezeka, wasimamizi wajipange kwani ukweli upo wazi sasa hakuna figisu,” amesema.
Wafuasi wa Chadema waliofika mahakamani hapo walishangilia kupewa dhamana kwa viongozi wao huku wakiimba ‘Peoples Power.’

Salum Mwalimu, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema amewapongeza watuhumiwa hao na kusema kuwa, hiyo ni moja ya changamoto za ukombozi.

“Tayari tumesikia kuwa wanabuni mbinu mpya ya kuwakamata madiwani ili kuitisha uchaguzi kwa kushtukiza,” amesema.
Mwalimu amesema, chama hicho kimepoteza wanachama wengi kwa kuuawa na wengine wamesingiziwa kesi hatimaye kufungwa.

Kesi hiyo iliyo chini ya Hakimu Mfawithi Mwanaamina Kumbakono, imepangwa kusikilizwa tena tarehe 16 Machi mwaka huu.
HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe amesema, hekaheka zinazofanywa na Serikali, Jeshi la Polisi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi yao ni kutaka kutwaa Umeya wa Jiji la Dar es Salaam lakini wataachia, anaandika Faki Sosi.

“Watake wasitake wataachia, hapa ni Ukawa tu. Yote haya yana mwisho lakini wajue kuwa namba ‘zinatufeva’ na si vinginevyo,” amesema Mdee.

Mdee, Mwita Waitara ambaye ni Mbunge wa Ukonga na washitakiwa wengine watatu leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu na kisha kuachwa kwa dhamana.

Washitakiwa hao wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumjeruhi Terresia Mmbando ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika Jumamosi wiki iliyopita na baadaye kuhairishwa na kuibua malumbano ya kisiasa.

Washitakiwa wengine kwenye tuhuma hizo ni Shafii Juma, Alfonce Kinyafu, Manase John pamoja na Diwani wa Kimara Stop-Over ambapo kila mmoja amejidhamini mwenyewe kwa Sh. 2,000,000.

Mawakili wa wanasiasa hao ni Peter Kibatala, John Malya, Omari Msemo na Fredrick Kiwelo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mdee amesema, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imedai kuwa, hakukuwa na sababu ya kuwakamata isipokuwa ni amri kutoka kwa viongozi wao.

Mdee amesema, jeshi hilo linaendeshwa kinyume cha sheria na kwa matakwa ya wanasiasa na watawala.
“Rais John Magufuli atake asitake ni lazima ataongozwa na Ukawa kwenye Jiji la Dar es Salaam na uchaguzi huu ni lazima Ukawa itashinda kwasababu namba haziwezi kubadilika,” amesema.

Amesema, mahakama imeweka wazi zuio la uchaguzi wa uchaguzi walilopeleka CCM sio halali na kwamba, (CCM) walikua wanatafuta njia ya kuiba kura katika uchaguzi huo.

Waitala ambaye ni Mbunge wa Ukonga amesema hatishwi na kuwekwa rumande na kwamba, wao kuwekwa huko ni sawa na simu iliyoisha chaji na kuchajiwa upya.

“Msimamo umeongezeka, wasimamizi wajipange kwani ukweli upo wazi sasa hakuna figisu,” amesema.
Wafuasi wa Chadema waliofika mahakamani hapo walishangilia kupewa dhamana kwa viongozi wao huku wakiimba ‘Peoples Power.’

Salum Mwalimu, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema amewapongeza watuhumiwa hao na kusema kuwa, hiyo ni moja ya changamoto za ukombozi.

“Tayari tumesikia kuwa wanabuni mbinu mpya ya kuwakamata madiwani ili kuitisha uchaguzi kwa kushtukiza,” amesema.
Mwalimu amesema, chama hicho kimepoteza wanachama wengi kwa kuuawa na wengine wamesingiziwa kesi hatimaye kufungwa.

Kesi hiyo iliyo chini ya Hakimu Mfawithi Mwanaamina Kumbakono, imepangwa kusikilizwa tena tarehe 16 Machi mwaka huu.
Wanaweza kutumia mbinu kama ile iliyotumika kule morogoro,wapiga kura wanawekwa jera kwa muda afu mshindi wao anatangazwa kwa ushindi wa kura moja.
ukweli hali hii ikiendelea,basi namimi napoteza matumaini yangu kwa magu,maana mazingaombwe haya ndo yalitufanya tuichukie serikali ya ccm
ila tulidhani serikali ya magufuri itakuwa tofauti.
 
Mkuu nilimwelewa alivyosema swala la Zanzibar hawezikuliingilia kulingana na Katiba ya wazanzibar .je na hili la mwenyekiti wa jiji nalo hatuwezikuliingilia kutokana na katiba ya wadaresalamu.
 
TANZANIA NA DEMOKRASIA YA KWELI:
Hivi wale wajumbe kule kilombero waliokamatwa na kuwekwa ndani ndiyo majibu yakawa chama chetu tawala kimeshinda kwa kura 19 na ndg zetu wapinzani wameshindwa kwa kura moja kwa maana wamepata kura 18?. Kwa mtindo huo si wajumbe 86 kwa 76 tukiwafungulia kesi wajumbe 11 na kuwaita mahakamani bila kukosa tarehe.ya uchaguzi au na wakishindwa kuja tukija kuwakamata siku ya uchaguzi kwa kushindwa kutii amri ya mahakama situtakuwa tumeshinda na huu wa umeya kama wa kilombero? Jamani mniwie radhi nilikuwa napita tu najaribu kuwaza mwenyewe kimya kimya...!!!
 
Wanaweza kutumia mbinu kama ile iliyotumika kule morogoro,wapiga kura wanawekwa jera kwa muda afu mshindi wao anatangazwa kwa ushindi wa kura moja.
ukweli hali hii ikiendelea,basi namimi napoteza matumaini yangu kwa magu,maana mazingaombwe haya ndo yalitufanya tuichukie serikali ya ccm
ila tulidhani serikali ya magufuri itakuwa tofauti.
Mbinu hiyo kwa Dar imeshabuma
 
Hibi kama polisi wako serious, kwanin wasimkamate aliye danganya kwamba kuna zuio la mahakama?? Maana hiyo ni jinai.
 
TANZANIA NA DEMOKRASIA YA KWELI:
Hivi wale wajumbe kule kilombero waliokamatwa na kuwekwa ndani ndiyo majibu yakawa chama chetu tawala kimeshinda kwa kura 19 na ndg zetu wapinzani wameshindwa kwa kura moja kwa maana wamepata kura 18?. Kwa mtindo huo si wajumbe 86 kwa 76 tukiwafungulia kesi wajumbe 11 na kuwaita mahakamani bila kukosa tarehe.ya uchaguzi au na wakishindwa kuja tukija kuwakamata siku ya uchaguzi kwa kushindwa kutii amri ya mahakama situtakuwa tumeshinda na huu wa umeya kama wa kilombero? Jamani mniwie radhi nilikuwa napita tu najaribu kuwaza mwenyewe kimya kimya...!!!
Mbinu Chafu zote zimeshajulikana
 
Back
Top Bottom