Mdee na wenzake waruhusiwa kuwasilisha pingamizi la kufutwa uanachama

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,357
8,079
Mahakama Kuu imeridhia mawakili wa wabunge 19 wakiongozwa na Halima Mdee kuwasilisha mapingamizi yao ya awali ili yasikilizwe kabla ya kuendelea na kesi ya msingi.

Uamuzi huo imetolewa leo Septemba 2, 2022 na Jaji Cyprian Mkeha wakati akitoa uamuzi kuhusiana na mapingamizi yaliyowasilishwa na wapeleka maombi

Jaji Mkeha baada ya kutoa uamuzi huyo, mjibu maombi wa kwanza, Wakili Pater Kibataka aliiomba mahakama hiyo iwape dakika 15 ili aweze kujadiliana na wenzake.

Jaji Mkeha alikubaliana na ombi la Kibatala na kauhirisha kesi hiyo kwa muda.

Kabla ya kuahirisha shauri hilo kwa muda, Jaji Mkeha alimtaka Kibatala ashauriane na mjibu maombi namba mbili ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Time ya Tafa ya Uchaguzi, kama watakubaliana kuendelea na kesi hiyo kwa muda huu au watakubaliana kuiahirisha.

Idadi ni kubwa ya wafuasi wa pande zote mbili, waliojitokeza katika Mahakama kusikiliza uamuzi huo.

Tofauti na wiki iliyopita wabunge hao walikuwepo mahakamni hapo, lakini leo wabunge hao hawajafika mahakamani hapo.
 
Kikchwa cha samaki kikioza na mkia wake pia huwa unaoza. Hivi mnanielewa kweli?
 
Back
Top Bottom