Mdee na wenzake wanayo kesi ya kujibu, isifanyike mizengwe haki ikapindishwa

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Kwanza kabisa kabla sijashusha nondo niweke wazi kuwa mahakimu wengi huwa wanatumia mwanya wa uhuru walionao kisheria kutoa adhabu kupendelea watu.

Ni wazi kuwaa Halima Mdee na wenzake walifanya mkusinyako usio halali na kuleta vurugu na hii ni kinyume na kifungu cha 89 sheria ya adhabu ya Tanzania.

Hivyo kama mtu alifanya kosa hili ni wazi anatakiwa afungwe mwaka mmoja jera, sababu kosa limefanyika mchana. Na mantiki hii Halima Mdee na Esther Bulaya watapoteza ubunge wao walioupata kimazabe. Sababu mbunge akifungwa zaidi ya miezi sita huwa anapoteza ubunge kama ibara ya 67(2)(c) ya katiba ya JMT.

Lakini kwa kuwa mahakama na mahakimu huwa wanatumika kisiasa huenda haki ikapindishwa na kuona watuhumiwa wanapata conditional discharge. Maana mahakimu wa kitanzania hutumiwa na wanasiasa.

My take; hakuna aliye juu ya sheria hapa Tanzania. Kama walifanya vurugu mchana kweupe wapate haki yao inayostahili.
 
Duh,We kiboko, Kesi ushaimaliza na hukumu umetoa!

Kuwa na kesi ya kujibu ni sehemu tu wa muendelezo wa kesi...mwisho wa siku je wamepatikana na hatia au la..?
 
Halima and co. Wasiwe na wasiwasi, sasa hivi wako upande wa CCM.

Simu moja tu ya Mhimili wa Ndugai na waachiwa huru.

Ndugai dare not miss them in the Bunge.
 
Kuna tofauti kati ya kufanya vurugu na kufanya vurugu kwa " kukusudia"

Halima Mdee na wenzake walifika gerezani kumpokea mwenyekiti wao Freeman Mbowe aliyekuwa anatoka jela!
Bwashee umekunywa mbege? Maelezo yaliyosomwa mahakamani ni kuwa walifanya vurugu makusudi.
 
maxresdefault.jpg
Vipi hii kitu haijajirudia tena KISUTU?
 
Back
Top Bottom